Waziri adaiwa kumwaga noti kununua Kawe beach, NHC yasema haijauzwa ni mali yake na kampuni ya Dubai

Waache ku report tu, wana report nini wakati hawapo tayari ku ripoti?
 
Wachukue hizo hela waondoke! Mwisho wake watakosa kila kitu!
 
mr Saguya yupo sahihi kabisa na binasfi naunga mkono hayo maamuzi ya kukodisha hiyo sehemu maana palikuwa tishio kwa USALAMA!!!!! ILA HILI LA KUSEMA ENEO LINAMILIKIWA KAMBUNI YA DUBAI SIJAELEWA KABISA !!!!! maana najua eneo lote la Tanganyika Packers hayati Magufuli aliwapa NHC , Sasa hiyo kampuni ya DUBAI imengia vipi kwenye umiliki??? naomba jibu Mr SAGUYA.
 
Rushwa, Rushwa, na Rushwa
Hayo ni maneno ya mwanahudhuri mmoja humu kuhusu R tatu za Serikali ya Muungano.

Pamoja na kuwa Serikali huwa inasemekana kuwa na mkono mrefu kwa utumiaji wa nguvu zake za Dola, Serikali hii imekuwa ikitumiwa na Waarabu kutunisha misuli yake pasipo haki kabisa, sasa wanakosa uhalali, ni Kimabavu mabavu tu.

Ngorongoro, Serikali na Wananchi walipimwa, tumenyamaza, kwa hali hiyo, tutegemee mengi ya kudhalilishwa na Uwekezaji huu wa Mwarabu na hayo yote yanaviashiria vya Rushwa, kunanuka Rushwa.

Tutanyukana kweli kweli, ni suala la Muda.
 
Dunia imejaa uonevu, pale ilipojengwa nyumba ya mstaafu JK zilibomolewa nyumba za msajili ikiwemo ya hayati Mbughuni, aliteswa sana yule mzee na JPM mpaka akafa kwa mawazo mengi wakati ni muanzilishi wa magazeti binafsi nchini.
 
Hii ni JF where people dare to speak openly sijui peno hasegawa unaogopa nini kutaja majina? Inapunguza hata quality ya ulichokiandika, kinaonekana ni uzushi
 
Naunga mkono hoja..hili andiko ni sawa na shairi la taarabu naona mods waliifute
Kweli mkuu, hili andiko halikutakiwa kuwepo mpaka sasa hivi.
Kama lingeandikwa na sisi tusiokuwa na hakimiliki hapa JF basi andiko hili lingekuwa lishafutwa au kuunganishwa na uzi mungine ambao mleta mada hauujui.
 
Tusipoangalia inawezakana tunapokaa makazi yetu yalishapigwa mnada siku nyingi bila sisi kujua!
 
Dunia imejaa uonevu, pale ilipojengwa nyumba ya mstaafu JK zilibomolewa nyumba za msajili ikiwemo ya hayati Mbughuni, aliteswa sana yule mzee na JPM mpaka akafa kwa mawazo mengi wakati ni muanzilishi wa magazeti binafsi nchini.
Huyo Mbughuni alikuwa nani?

Alikuwa na tishio gani nchini mpaka ikapelekea Magufuli kumtesa?
 
Wasiibinafsishe na beach sasa wakata ufuta tutakosa pa kwenda kupunguza stress.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…