Waziri ataka wanaume wanaobaka wahasiwe

Waziri ataka wanaume wanaobaka wahasiwe

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Zanzibar, Riziki Pembe Juma amesema ili kukomesha vitendo vya ukatili na udhalilishaji kwa wanawake na watoto, ipo haja wanaume wanaofanya vitendo hivyo kuhasiwa.

Amesema licha ya sheria kuwapo na serikali na wadau wengine kupambana dhidi ya vitendo hivyo lakini bado vinaendelea kushamiri.

Ametoa kauli hiyo leo Novemba 25, 2022 wakati wa kufungua siku 16 za uanaharakati kupinga vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa wanawake na watoto katika ukumbi wa Abdulwakil mjini Unguja, Zanzibar, ambapo mgeni rasmi ni Mke wa Rais wa Zanzibar, Mariam Mwinyi.

“Niombe ombi maalumu kwako utufikishie ombi hili kwa Mheshimiwa Rais (Hussein Mwinyi), tunajua sheria zipo na zinafanya kazi yake lakini bado wanaofanya vitendo hivi wanaona kama sheria zinawachombeza,” amesema.

“Tungalie namna bora ya kuwapo na adhabu mbadala badala ya mtu kufungwa miaka 30 kwenda kuitia hasara Serikali kule ndani bado afikirie wote wanaodhibitika kufanya hivyo, wahasiwe,” amesema.

Huku akiwahoji washiriki wa mkutano huo wanasemaje na wao kumuitikia ndiyoooo…Waziri Pembe amesema “kwakweli tumechoka, tumechoka tumechoka, wenzetu, ukifanyika mfano wa wabakaji watatu tunaamini wanaume wote itakuwa funzo kwao na wataacha tabia hiyo,” amesema.

Ameongeza kuwa “Tunaomba sana, kama wanaona kubaka ni haki basi na kuhasiwa iwe ni haki,” amesema.

Hata hivyo amesema wizara imeanzisha kitengo maalumu cha kuratibu vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto kwa kushirikina na wadau na wanaharakati na jumuiya za wanawake na wanaume kuona wanasimama pamoja kupinga vitendo hivyo.
Vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto vilishamiri mwaka 1991.

Kutoka na hali hiyo, lianzishwa kampeni ulimwenguni kote ambayo ilitokana na mkutano wa wanaharakati kufuati mkutano uliofanyika Kolombia Amerika kati ya Novemba 18 hadi 21 mwaka 1991 na kuweka maazimio ya kupinga vitendo vya ukatili.

Mkutano huo uliazimia na kuchagua siku 16 za kila mwaka kuanzia Novemba 25 hadi Desemba 10 ambayo ni siku ya kimataifa ya Haki za binadamu kwa lengo la kuhusisha ukatili na ukiukwaji wa haki za binadamu ulimwenguni kote kuwa siku ya kimataifa dhidi ya vitendo vya ukatili na udhalilishaji.

Katibu mkuu wa wizara hiyo, Abeida Rashid Abdalla amesema faraja imepotea miongoni mwa jamii kutokana na vitendo hivyo.

MWANANCHI
 
Mmmmh, kwa hii hii Nchi yenye wenyeviti wa vyama vya wanaume wanaopigwa na wake zao?
 
Mbunge kaongea kisiasa tu. Je, akikata rufaa ikaonekana hukumu haikuwa ya haki na mmeshamhasi? Sheria zibaki tu zilivyo maana haya makosa yanayohusisha ngono huwa yana mambo mengi mno. Kuna watu wako jela kwa kusingiziwa.
Na wanaohukumiwa kunyongwa ama kwa hukumu za makosa mengine nao vipi kwa mfano wako huo?

Mi nadhani sheria itungwe tu kama zilivyo sheria zingine ili mtu akitiwa hatiani bila kuacha shaka yoyote zing'olewe tu maana hakuna namna.

Akiona haridhiki na hukumu akate rufaa mahakama kuu mpaka mwisho wa ngazi za mahakama kama kulivyo kwa sheria zingine zote.

Na rufani yake ikitupiliwa mbali zinang'olewa na kung'olewa.

Maana watu wengine katili wanaona kubaka kama ni silaha ya kudhalilishia wanyonge wao.

Adhabu hiyo ikipitishwa heshima itarudi.
 
Ndugu tatizo la ubakaji ni kubwa mno. Hao wanaoripotiwa ni wachache kuliko ambao hawajapelekwa mahakamani. Wanawake wa Tanzania wakisema washtaki basi kwa sheria hiyo vijana wengi sana watahasiwa. Nadhani kila familia ielimishe vijana wake kwamba lile tendo sio la kulazimishana. Soma uzi wangu niliandika. Pia ukisoma ule uzi maarufu wa KULA TUNDA KIMASIHARA utaona jinsi vijana walivyo washenzi.
 
Pumba tu viongozi wenyewe wamekaa kiharakati zaidi badala ya uhalisia
 
Matamko ya hisia ni mabaya sana, sasa tutafakari

Kuwahasi itakuwa ni adhabu inayolenga nini hasa?, je hawa watu wakikata rufaa alafu wakashinda rufaa na wakiwa tayari wamehasiwa je wataweza kurudishiwa uwezo wao ulioondolewa kimakosa?.

Swala lingine ni je, mhusika akimaliza kifungo chake gerezani alafu akashindwa kuzalisha je ataweza kurudishiwa uwezo wake?,

Je, kosa hili litakuwa na adhabu ya maisha na kama ndio vipi kuhusu adhabu ya kifungo?, je kosa hili litakuwa na adhabu mbili swala ambalo sheria inakataza adhabu mbili kwa kosa moja.

Nadhani Mheshimiwa waziri na wanaomuunga mkono wawaze zaidi
 
Na wanaohukumiwa kunyongwa ama kwa hukumu za makosa mengine nao vipi kwa mfano wako huo?

Mi nadhani sheria itungwe tu kama zilivyo sheria zingine ili mtu akitiwa hatiani bila kuacha shaka yoyote zing'olewe tu maana hakuna namna.

Akiona haridhiki na hukumu akate rufaa mahakama kuu mpaka mwisho wa ngazi za mahakama kama kulivyo kwa sheria zingine zote.

Na rufani yake ikitupiliwa mbali zinang'olewa na kung'olewa.

Maana watu wengine katili wanaona kubaka kama ni silaha ya kudhalilishia wanyonge wao.

Adhabu hiyo ikipitishwa heshima itarudi.
Kun adhabu kubwa kuliko kunyongwa hadi kufa?!!lakini mbona sasa kila kukicha matukio ya mauaji ndio kwanza yanaongezeka?!!si yangekuwa yameishakwisha kutokana na ukali wa adhabu?!!Wala hakuna mnyonge anayedharirishwa kwa kubakwa ,Hao watoto wadogo ambayo ndio wahanga wakubwa wa vitendo hivyo ana unyonge gani zaidi ya ushenzi tu wa hao wabakaji na asilimia kubwa ni kutokana na imani potofu tu za kishirikina.
 
Watu waache ubakaji, uzinzi na ulawiti. Wajikite katika toba na kufuata misingi ya dini na tamaduni njema. Wakifanya kazi kwa bidii mawazo potofu yatawatoka kichwani mwao
 
Watu waache ubakaji, uzinzi na ulawiti. Wajikite katika toba na kufuata misingi ya dini na tamaduni njema. Wakifanya kazi kwa bidii mawazo potofu yatawatoka kichwani mwao
Kweli mkuu. Tatizo siku hizi mtu anafanya upuuzi hadharani ukiuliza unaambiwa una wivu fanya mambo yako. Kwa mfano vijana kuvaa mavazi ya hovyo ni janga. Wazazi wanachekelea na kudhani ndo usomi.
 
Katika vitu ambavyo huwa vinahitaji hekima na busara, akili na maarifa katika kuvijadili na kuvitolea maamuzi ni suala hili la ubakaji ambalo kimsingi limeanzishwa na uana harakati na sera za magharibi ambao pia ndio wanapromote ushoga kwa kiwango cha juu hapa nchini kwa sasa.

Tangia kutungwa kwa sheria ya ubakaji mwaka 2009 vipo visa vingi vya kukomoana hasa wapenzi wanapofarakana wametend kutumia upendeleo huu kwa jinsia fulani kukomoa jinsia nyingine.
Uendeshaji wa kesi hizi hasa zile zinazotokana na mifarakano ya mahusiano lifanywe kwa umakini sana na kwa uangalifu vinginevyo wanaume ambao kwa mujibu wa sensa ni wachache wataishia magerezani na hatimaye azima ya magharibi kudhibiti ongezeko la idadi ya watu Afrika lipate kufanikiwa!
 
Back
Top Bottom