Waziri Aweso ampokea Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Rose Zakaria Ambrose baada ya uapisho

Waziri Aweso ampokea Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Rose Zakaria Ambrose baada ya uapisho

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameongoza mapokezi ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Bi Rose Zakaria Ambrose aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hasaan mapokezi yaliyofanyika mapema leo Februari 9, 2026 katika ofisi za DAWASA Mkoani Dar es salaam.
WhatsApp Image 2026-02-09 at 17.37.09.jpeg

WhatsApp Image 2026-02-09 at 17.37.10 (1).jpeg

WhatsApp Image 2026-02-09 at 17.37.10.jpeg
Katika mapokezi hayo, Waziri Aweso aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Mwajuma Waziri, Menejiment ya Wizara, Wakuu wa Taasisi chini ya Wizara ya Maji na Viongozi waandamizi kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) na kueleza mipango mikakati ya kuimarisha huduma za Maji Nchini sambamba na miradi inayoendelea.
​
“Menejimenti na Watumishi wa Wizara ya Maji tunakupongeza kwa nafasi uliyopata na tunaahidi ushirikiano katika kufanikisha shughuli zako za kuwapatia huduma bora na ya uhakika ya Majisafi na Salama kwa Watanzania” alisema Waziri Aweso

“Pia tumempitisha katika mipango ya muda mrefu na mfupi na mwelekeo wetu kama Wizara katika kusimamia maono ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan ya kumtua Mama ndoo kichwani sambamba na kusimamia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050,” alisisitiza Waziri Aweso.
 
Halafu wanasema hateui wagalatia, haya huyu hapo mwenzenu tumemkaribisha
 
Back
Top Bottom