afisakipenyo
JF-Expert Member
- Sep 1, 2020
- 450
- 785
Muktasari:
Miongoni mwao alikuwepo wakati Aweso akiwasilisha hotuba yake ya bajeti, ni Babu Ali ambaye ni mdogo wa Waziri huyo aliyeongozana na wanafamilia wengine kumsindikiza na kujionea tukio hilo.
Dodoma. Kifo ni fumbo. Hivi
ndivyo unavyoweza kusema kwani
kinaweza kumtokea mtu mahali na
wakati wowote kama ilivyo kwa
Babu Ali,
Wakati Waziri wa Maji, Jumaa
Aweso akiwasilisha hotuba ya bajeti
kwa mwaka wa fedha 2025/26
bungeni jijini Dodoma, kwenye
majukwaa ya wageni kulikuwa na
ndugu na wageni mbalimbali
waliokuja kumsindikiza
Miongoni mwao alikuwepo Babu
Ali, ambaye ni mdogo wa Waziri
huyo aliyeongozana na wanafamilia
wengine kumsindikiza na k ujionea
tukio hilo.
Hata hivyo, mara baada ya Aweso
kuwasilisha bajeti yake na shughuli
za Bunge kuahirishwa, familia
walitoka nje na kupiga picha ya
pamoja kabla ya kukutana kwenye
tafrija ndogo kumpongeza Waziri
huyo ambaye pia ni mbunge wa
Pangani.
Ndani ya Ukumbi wa Bunge, Spika
Dk Tulia Ackson aliwatambulisha
kila mtu kwa jina lake na Ali
alisimama akionekana mwenye
furaha kama ilivyokuwa kwa ndugu
wengine,
Baada ya tukio hilo, kila mmoja
alikwenda kujipumzisha akiwemo
Ali aliyefikia katika moja ya hoteli
jijini hapa
Sherehe hiyo ndio kama ilikuwa ya
kuagana na ndugu zake kwani Ali
hakuamka na walipokwenda
chumbani kwake kumuamsha ili
wawahi bungeni kumsikiliza Aweso
akijibu hoja za wabunge, alikuwa
tayari amefariki dunia.
Hata hivyo, leo mapema Aweso
alihitimisha hotuba yake bungeni
baada ya wabunge kupitisha bajeti
yake,
Mpaka sasa sababu za kifo chake
hazijafahamika na taratibu za
kwenda Pangani, Tanga kwa
mazishi zinaendelea nyumbani kwa
Aweso eneo la Ilazo jijini Dodoma,
Kama kifo kingeweza kusema
huenda Ali asingesafiri kutoka
Pangani kwenda Dodoma lakini siri
hiyo imefanya aende Dodoma akiwa
mzima na kurudi Pangani akiwa
amelala usingizi wa milele,
Akizungumza kwa niaba ya a
familia, msemaji katika msiba huo,
Rashid Shangazi amesema hakuna
aliyejua na anayejua hadi sasa nini
chanzo cha kifo cha ndugu yao
Shangazi ambaye ni Mbunge wa
Mlalo, amesema Ali na ndugu zake,
jana Alhamisi, alikuwa bungeni
wakati Waziri Aweso alipokuwa
akisoma bajeti yake na hadi usiku
alikuwa mzima.
"Kama mlivyomuona jana
akitambulishwa pale bungeni,
baadaye jioni walikutana
wanafamilia wakakaa pamoja
katika halfa ambayo Mheshimiwa
(Aweso) alikuwa amewaandalia na
kisha wakaagana kila mmoja
akaenda kulala alipokuwa
ameandaliwa," amesema Shangazi
Shangazi ambaye ni Katibu wa
Wabunge wa CCM, amesema leo
Ijumaa Mei 9, 2025 asubuhi
walianza kukumbushana ili waende
bungeni na wengine kwenda
kwenye majukumu yao, ndipo
wakagundua kuwa simu yake
haipatikani.
"Iliwastua ndugu na walipofuatilia
katika chumba alicholala,
walimkuta amepoteza maisha, hana
historia ya ugonjwa wala tatizo
lingine lolote katika maisha yake,
isipokuwa tunasema Inna Lillah
Wainna Illaih Rajiun," amesema
Shangazi.
Amesema taratibu za kusafirisha
mwili wa marehemu zinaendelea
baada ya waombolezaji kupata
chakula, safari ya kuelekea Pangani
itaanza.
Kwa mujibu wa Shangazi, kesho
Jumamosi baada ya swala ya
adhuhuri watakwenda kuusitili
mwili wa Ali katika nyumba yake ya
milele mahali ambapo familia
itakuwa imeandaa.
Hata hivyo, amesema suala la nini
kilikuwa kinamsibu itabaki ni
fumbo kati ya marehemu na Mungu
wake kwani hajawahi kusema
chochote kama kuna shida katika
afya yake.
Kwa upande wake, Waziri Aweso
amesema ni mpango wa Mungu,
hakuna wa kulaumiwa
Kwa upande wake, Waziri Aweso
amesema ni mpango wa Mungu,
hakuna wa kulaumiwa.
Wabunge wengi wamefika
nyumbani kwa Aweso ambapo
wanafamilia waliokuwa wamekuja
bungeni walikuwepo huku
watumishi wa Wizara ya Maji
wakionekana kwa wingi
Wengine waliofika ni Waziri Mkuu
na Makamu wa Rais mstaafu, John
Malecela ambaye aliongozana na
mkewe, Anne Kilango Malecela.
wakiwa wamefuata na Mbunge wa
Buchosa, Erick Shigongo
Miongoni mwao alikuwepo wakati Aweso akiwasilisha hotuba yake ya bajeti, ni Babu Ali ambaye ni mdogo wa Waziri huyo aliyeongozana na wanafamilia wengine kumsindikiza na kujionea tukio hilo.
Dodoma. Kifo ni fumbo. Hivi
ndivyo unavyoweza kusema kwani
kinaweza kumtokea mtu mahali na
wakati wowote kama ilivyo kwa
Babu Ali,
Wakati Waziri wa Maji, Jumaa
Aweso akiwasilisha hotuba ya bajeti
kwa mwaka wa fedha 2025/26
bungeni jijini Dodoma, kwenye
majukwaa ya wageni kulikuwa na
ndugu na wageni mbalimbali
waliokuja kumsindikiza
Miongoni mwao alikuwepo Babu
Ali, ambaye ni mdogo wa Waziri
huyo aliyeongozana na wanafamilia
wengine kumsindikiza na k ujionea
tukio hilo.
Hata hivyo, mara baada ya Aweso
kuwasilisha bajeti yake na shughuli
za Bunge kuahirishwa, familia
walitoka nje na kupiga picha ya
pamoja kabla ya kukutana kwenye
tafrija ndogo kumpongeza Waziri
huyo ambaye pia ni mbunge wa
Pangani.
Ndani ya Ukumbi wa Bunge, Spika
Dk Tulia Ackson aliwatambulisha
kila mtu kwa jina lake na Ali
alisimama akionekana mwenye
furaha kama ilivyokuwa kwa ndugu
wengine,
Baada ya tukio hilo, kila mmoja
alikwenda kujipumzisha akiwemo
Ali aliyefikia katika moja ya hoteli
jijini hapa
Sherehe hiyo ndio kama ilikuwa ya
kuagana na ndugu zake kwani Ali
hakuamka na walipokwenda
chumbani kwake kumuamsha ili
wawahi bungeni kumsikiliza Aweso
akijibu hoja za wabunge, alikuwa
tayari amefariki dunia.
Hata hivyo, leo mapema Aweso
alihitimisha hotuba yake bungeni
baada ya wabunge kupitisha bajeti
yake,
Mpaka sasa sababu za kifo chake
hazijafahamika na taratibu za
kwenda Pangani, Tanga kwa
mazishi zinaendelea nyumbani kwa
Aweso eneo la Ilazo jijini Dodoma,
Kama kifo kingeweza kusema
huenda Ali asingesafiri kutoka
Pangani kwenda Dodoma lakini siri
hiyo imefanya aende Dodoma akiwa
mzima na kurudi Pangani akiwa
amelala usingizi wa milele,
Akizungumza kwa niaba ya a
familia, msemaji katika msiba huo,
Rashid Shangazi amesema hakuna
aliyejua na anayejua hadi sasa nini
chanzo cha kifo cha ndugu yao
Shangazi ambaye ni Mbunge wa
Mlalo, amesema Ali na ndugu zake,
jana Alhamisi, alikuwa bungeni
wakati Waziri Aweso alipokuwa
akisoma bajeti yake na hadi usiku
alikuwa mzima.
"Kama mlivyomuona jana
akitambulishwa pale bungeni,
baadaye jioni walikutana
wanafamilia wakakaa pamoja
katika halfa ambayo Mheshimiwa
(Aweso) alikuwa amewaandalia na
kisha wakaagana kila mmoja
akaenda kulala alipokuwa
ameandaliwa," amesema Shangazi
Shangazi ambaye ni Katibu wa
Wabunge wa CCM, amesema leo
Ijumaa Mei 9, 2025 asubuhi
walianza kukumbushana ili waende
bungeni na wengine kwenda
kwenye majukumu yao, ndipo
wakagundua kuwa simu yake
haipatikani.
"Iliwastua ndugu na walipofuatilia
katika chumba alicholala,
walimkuta amepoteza maisha, hana
historia ya ugonjwa wala tatizo
lingine lolote katika maisha yake,
isipokuwa tunasema Inna Lillah
Wainna Illaih Rajiun," amesema
Shangazi.
Amesema taratibu za kusafirisha
mwili wa marehemu zinaendelea
baada ya waombolezaji kupata
chakula, safari ya kuelekea Pangani
itaanza.
Kwa mujibu wa Shangazi, kesho
Jumamosi baada ya swala ya
adhuhuri watakwenda kuusitili
mwili wa Ali katika nyumba yake ya
milele mahali ambapo familia
itakuwa imeandaa.
Hata hivyo, amesema suala la nini
kilikuwa kinamsibu itabaki ni
fumbo kati ya marehemu na Mungu
wake kwani hajawahi kusema
chochote kama kuna shida katika
afya yake.
Kwa upande wake, Waziri Aweso
amesema ni mpango wa Mungu,
hakuna wa kulaumiwa
Kwa upande wake, Waziri Aweso
amesema ni mpango wa Mungu,
hakuna wa kulaumiwa.
Wabunge wengi wamefika
nyumbani kwa Aweso ambapo
wanafamilia waliokuwa wamekuja
bungeni walikuwepo huku
watumishi wa Wizara ya Maji
wakionekana kwa wingi
Wengine waliofika ni Waziri Mkuu
na Makamu wa Rais mstaafu, John
Malecela ambaye aliongozana na
mkewe, Anne Kilango Malecela.
wakiwa wamefuata na Mbunge wa
Buchosa, Erick Shigongo