Yaani umepotosha mno! Tena sana.
1.) Unapoitaje ‘Genetic Modification’ ni lazima ujue context inayohusika, unaposema ‘Cross breeding’ inayofanyika katika ‘Hybridization’ ni sawa na ‘Genetic Modification’, nami nitakuuliza, baba yako na mama yako walipounganisha mbegu zao na kukuzaa wewe, ni ‘Genetic Modification’? Kama sio kwanini? Au wewe ni exactly identical na baba yako? Au wewe ni exactly identical na mama yako? Ofcourse not, lakini hiyo haifanyi ile reproduction process waliyoifanya iitwe ‘Genetic modification’ although genes zako ni tofauti na zao, bado hatuwezi kuichukua out of context na kuita ‘Genetic Modification’, never. Nimefafanua vizuri maana ya ‘Genetic Modification’, sina haja ya kurudia.
2.)Kusema tofauti ya ‘Hybridization’ na ‘GM’ ni kwamba moja inafanyika naturally na nyingine inafanyika kwenye maabara si kweli, umepotosha. Mtu anaweza akachuku shahawa za muafrika na akachanganya na yai la mchina kwenye test tube ndani ya maabara na mtoto akapandikizwa kwa Surrogate mother na akazaliwa chotara wa kiafrika na mchina, je , hiyo utaita ni ‘Genetic Modification’ kisa imefanyika kwenye maabara??! Ofcourse not, sasa hata sikui kwanini umeamua kunichosha kuandika risala ndefu hivi.
1. Mfano wako hauna uhalisia. Baba yangu na mama yangu wote ni waafrika, wabantu tena kabila moja (same specie, same genus). Kwahiyo hapo hakuna crossbreeding, hakuna genetic modification sababu wana sifa za kufanana. Nilikupa mfano wa mzungu na muafrika, wakizaa mtoto atakua chotara mwenye genes za kizungu na kiafrika. Huyu chotara anakua na baadhi ya sifa tofauti na wazazi wake sababu yeye amebeba genetic mixture ya mzungu na mwafrika. Tayari hii ni genetic modification, na huyo mtoto chotara ndio hybrid yenyewe.
Mzungu na mwafrika wote tuko specie moja, ila tuna baadhi ya sifa tofauti. Ndio maana nilisema hybridization ni kwa viumbe wenye baadhi ya sifa za kufanana (close related species or genus), na sio viumbe wanaofanana moja kwa moja (identical).
Kwahiyo mfano wako kuhusu wazazi wangu hauna mantiki!
2. Sijaelewa ni kipi unapinga na kipi unakubali. Yani mtu achukue shahawa za muafrika, arutubishe yai la mchina kwenye test tube ndani ya maabara alafu apandikize kwa surrogate mother, kwako hii sio genetic modification?
Mkuu, ovum (yai la kike) ina central nucleus ambayo ndiyo inabeba genetic material ya mwanamke. Hizi genetic materials za mwanamke zinapoungana na genetic materials za mwanaume zilizoko kwenye sperm, ndio zinaamua inherited characteristics of the offspring!
Sasa kama original parents, mmoja ni mchina na mwingine muafrika, na mtoto anaezaliwa ni chotara, maana yake ni kwamba amebeba genetic mixture ya mchina na muafrika. Hii ndio genetic modification yenyewe!
Ingekua kwamba mchina na muafrika wanazaa mtoto either mchina pure kama mama yake, au muafrika pure kama baba yake badala ya mtoto chotara, basi hapo kusingekua na genetic modification. Sababu outcome (mtoto) haina tofauti na moja kati ya original breeds (wazazi).
In short, ukiweza kufanya chochote kile kwenye genes za original breeds, then ukapata another breed mwenye genes tofauti na zile za original breeds, tayari unakua umefanya genetic modification. Haijalishi umeifanya naturally, au maabara!