FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 38,920
- 44,970
Labda nikusaidie kitu kimoja, ili tusiende in a vicious cycle.1. Mfano wako hauna uhalisia. Baba yangu na mama yangu wote ni waafrika, wabantu tena kabila moja (same specie, same genus). Kwahiyo hapo hakuna crossbreeding, hakuna genetic modification sababu wana sifa za kufanana. Nilikupa mfano wa mzungu na muafrika, wakizaa mtoto atakua chotara mwenye genes za kizungu na kiafrika. Huyu chotara anakua na baadhi ya sifa tofauti na wazazi wake sababu yeye amebeba genetic mixture ya mzungu na mwafrika. Tayari hii ni genetic modification, na huyo mtoto chotara ndio hybrid yenyewe.
Mzungu na mwafrika wote tuko specie moja, ila tuna baadhi ya sifa tofauti. Ndio maana nilisema hybridization ni kwa viumbe wenye baadhi ya sifa za kufanana (close related species or genus), na sio viumbe wanaofanana moja kwa moja (identical).
Kwahiyo mfano wako kuhusu wazazi wangu hauna mantiki!
2. Sijaelewa ni kipi unapinga na kipi unakubali. Yani mtu achukue shahawa za muafrika, arutubishe yai la mchina kwenye test tube ndani ya maabara alafu apandikize kwa surrogate mother, kwako hii sio genetic modification?
Mkuu, ovum (yai la kike) ina central nucleus ambayo ndiyo inabeba genetic material ya mwanamke. Hizi genetic materials za mwanamke zinapoungana na genetic materials za mwanaume zilizoko kwenye sperm, ndio zinaamua inherited characteristics of the offspring!
Sasa kama original parents, mmoja ni mchina na mwingine muafrika, na mtoto anaezaliwa ni chotara, maana yake ni kwamba amebeba genetic mixture ya mchina na muafrika. Hii ndio genetic modification yenyewe!
Ingekua kwamba mchina na muafrika wanazaa mtoto either mchina pure kama mama yake, au muafrika pure kama baba yake badala ya mtoto chotara, basi hapo kusingekua na genetic modification. Sababu outcome (mtoto) haina tofauti na moja kati ya original breeds (wazazi).
In short, ukiweza kufanya chochote kile kwenye genes za original breeds, then ukapata another breed mwenye genes tofauti na zile za original breeds, tayari unakua umefanya genetic modification. Haijalishi umeifanya naturally, au maabara!
Tofauti kuu ni hii:-
Hybridization hutumia ‘Fertilization’ inayoleta fertile offspring, na haihusishi ‘GENE SPLICING’, bali ‘Genetic Modification’ huusisha ‘GENE SPLICING’ na ‘GENE STITCHING’, then fertilization ndio hufuata baadae.
Nadhani sasa unaweza kutofautisha kwa urahisi sana process ya ‘hybridization’ na ‘Genetic Modification’ in a clear cut manner.