Waziri Bashe acha kuchezea Kodi zetu kwa maono mfu! Kilimo siyo filamu

Wangehimiza hata kilimo cha organic food crops ili tupate uhakika wa masoko ya nje ambapo organic crops zinauzwa kwa bei kubwa sana , hapo ningewaelewa, au wangehimiza kwa nguvu ulimaji wa maua kule Arusha na njombe hapo ningeelewa, dunia iko mbele na viongozi wako nyuma
 
Mwandishi wa andiko ktk ubora wako. Sasa kwann wizara isiweke nguvu ktk kuondoa hizo changamoto kwa wakulima badala yake inaanzisha BBT?
Changamoto zote ziko covered kwenye huu mradi. Ni vile tu mnapenda kukosoa bila kujiridhisha na mnachokosoa. Mradi unahusisha from production, processing to marketing and selling. Narudia tena tatizo la wakulima wa Tanzania ni uduni wa kinachozaliwa, uchache wa kinachozalishwa na kutokuwa na muendelezo wa kinachozalishwa. Tunaolima ndio tunajua, unaweza kujifanya unalima maharage, na kutafuta soko nje, wakikuambia wanataka container 10 kila mwezi (sawa na container 120 kwa mwaka), je tutaweza kukidhi soko hilo throughout? Yes, kama kilimo chetu ni cha gunia 10, lazima tupate shida ya soko maana utaishia kwenda kumuachia dalali mzee "Juma" pale Kariakoo. Atakupiga kiswahili kiasi hutarudi hata na mtaji. Imagine umepata soko la mchele kwa maduka ya Walmart. Walmart ana stores zaidi ya 10,000 duniani na anataka bidhaa hiyo iwepo katika stores zake zote kuwa quality iliile, utaweza kweli order hiyo kwa kutegemea kilimo cha Dua za mvua?? No way!

Kwa miaka mingi tumekuwa tukidhani kilimo na mpira ni kazi za walioshindwa na kuangukia huko by chance. That's totally wrong. Samia na Bashe wanachokifanya ndicho kinachotakiwa kufanywa. Kuifanya sekta ya kilimo ni kama sekta nyingine za kitaalam na rasmi. Kwa kufanya hivyo pekee ndio tutakuwa na takwimu sahihi za kilimo, tija, ajira na ndio kitachangia pato halisi la uchumi.

Binafsi natamani wakulima wooote Tanzania wawe na mfumo huo wa Kilimo. Scheme kama hiyo ikifanywa kwenye mifugo na michezo, hakutakuwa na tatizo la ajira Tanzania. Kufeli kwa mradi itakuwa ubovu wa vichwa vya watanzania lakini si tatizo la wazo lenyewe.
 
Loo! Hata mahindi usipowaona madalali pale soko la Tandale utarudi nayo.
Ndiyo maana mnasema mradi utafeli cause mnazungumzia ukulima wa kuvuna kwa gunia na debe, huko sio kulima anakokusudia Samia na Bashe. Hivi Dalali wa Kariakoo anaweza kupokea mahindi Tani 2000 tu kwa mfano? (Container 500). Ataishia kupokea fuso Tani 5 (Tena kama amejitahi saaana).
 
Umeangalia Kwa angle yako

Ukosefu wa mitaji ni Kweli na ukosefu wa Masoko ni Kweli pia

Let’s be comprehensive and holistic
 
Nimechukua kipande hiki kwa muktadha wa "tujadili kidogo". Kwanza nashukuru kwamba umechanganua vizuri sana dhana ya QQC, kwamba Q+Q=C. Kwa nachojua mimi, unless otherwise, BBT inahusisha makundi yote mawili (waliokuwepo na wapya).

Hebu tujiulize, kwanini tuna tatizo la ubora na wingi, na je matatizo haya yanaweza kutibiwa vipi? Sababu ya msingi niionayo mimi ni kudhani kilimo ni kazi isiyo rasmi na hivyo ufanyikaji wake hauhitaji usimamizi, uangalizi wala utaratibu wowote unaoeleweka. Mfano mzuri wa Kilimo chetu ni kama ujenzi wa mji wa Dar es Salaam. Kwa sehemu kubwa umejengwa bila usimamizi, uangalizi wala utaratibu. Matokeo yake tija ya makazi Dar es Salaam haipo.

Tunafanyaje kutatua tatizo la Dar ( one day iwe kama New York?). Tuna option 3. Ya kwanza kurasimisha ( ila hii definitely haitatua mpangilio mbovu wa Dar). Ya pili kuvunja na kuanza upya kwa kupanga na kunyoosha mitaa na kujenga majengo tunayoyataka( utaratibu huu yumkini unaweza kuitengeneza Dar yenye mitaa kama New York au maeneo mengine duniani). Hii option huenda ni VERY EXPENSIVE maana ina maswali na interventions nyingi zinazotakiwa, kwa mfano, wakati wa utekelezaji wake hao wakazi wa Tandale, manzese, mabibo, Tabata etc etc watakaa wapi???

Option ya 3 ni kuanza na maeneo ya nje ya mji kuyapanga na kuyajenga kwa tunavyotaka kabla ya kutekeleza option ya 2 hapo juu. Kwa mtizamo wangu hiki pia ndicho kilichopo kwenye kilimo chetu. Wakulima waliopo wanaendesha kilimo chao bila uangalizi, bila usimamizi na bila utaratibu kiasi ni vigumu sana ukitaka kuwasaidia wazalishe kwa kiasi cha kufikia Q+Q=C. Wako scattered, kila mmoja ana eneo la ukubwa wake na analima anachotaka yeye. Katika eneo lenye ukubwa wa hekta 100, lina wamiliki 300, wapo wenye hekta 5, wengine 2, wengine 1 na wengine miguu 70 kwa 32, haitoshi ndani yake kuna anaelima mahindi, wengine ufuta, wengine mpunga, wengine kunde, wengine alizeti, wengine mbogamboga, wengine wanafuga mbuzi humo, wengine mabwawa ya samaki na pengine ndani ya eneo hilohilo kuna makaburi, nk nk nk.
Na zaidi, kila mmoja ana aina yake ya umiliki wa ardhi. Katika hali kama hiyo, ni interventions zipi utafanya kiwezaa kuwasaidia wakulima hawa ili waweze kuzalisha kwa msingi wa Q+Q=C? Mfano, Uukiamua uwajengee skimu ya umwagiliaji, walima mpunga watafurahi, vipi walima ufuta? Hiyo skimu utaipitishaje kwa mwenye shamba la ufuta ili imfikie mlima mpunga. Ni ngumu aana.

Kwa mifano hiyo ndipo binafsi naona namna nzuri ya kufanya interventions kwenye kilimo Tanzania ni kukifanya kiwe sekta iliyo rasmi na wanaojihusisha nacho watambulike, waaminiwe na wakopesheke. Kwa lugha nyingine, kuifanya iwe sekta yenye uangalizi, usimamizi na utaratibu kwa kuanzisha maeneo mapya na kuyapanga, kuyawekea miundombinu yote muhimu (ya uzalishaji, usindikaji, usambazaji na uuzaji). Ndiyo msingi wa BBT. Maeneo mapya hapa ima hayajawahi kulimwa kabisa au yametwaliwa kwa njia ya fidia kutoka kwenye kundi la wakulima wetu wa kikale.

Ni rahisi kwa wanunuzi kwenda kununua alizeti au kuweka kiwanda kwenye eneo moja lenye hekta 2000, kuliko kununua alizeti kwenye eneo la hekta 3000 zilizotapakaa katika mikoa 26. Hii ndiyo BBT.

Hata hivyo katika utekelezaji wa mradi huu, naamini una components za kusaidia wakulima walio nje ya mfumo huu ambao wana minimum qualifications za kuitwa wakulima wadogo na wa Kati lakini wanabanwa na changamoto kadha wa kadha zinazowafanya wasifikie (sina hakika kama component hii ipo na kama haipo natamani ijumuishwe). Kuna watu wana mashamba ya hekta 10 Hadi 100 na wanalima bila mifumo mizuri ya kilimo. Ni vema Serikali ikawatambua wakulima hawa na kubaini changamoto zao na kuzitatua kwa kadri ya kila mmoja. Kama mkulima ana shida ya trekta, apewe au akopeshwe kwa masharti nafuu. Kama ana shida na kisima achimbiwe, kama ana shida na godawn ajengewe, nk nk nk. Natamani kuona serikali inaondoa kodi kwenye mitambo ya kuchimba visima ili uchimbaji wa visima isiwe anasa. Natamani Serikali ipeleke umeme mashambani ili utumike kwenye shughuli za kilimo kwa ujumla wake. Natamani Serikali ijenge barabara za mawe kuelekea vijijini ili usafirishaji wa mazao uwe muda wote.

Kwa kufanya hivi baadhi ya hawa wanaolima kimazoea wanaweza kuondoka kwenye maeneo wanayolima kienyeji na kwenda kuingia kwenye BBT block farms (kama inavyotokea kwa baadhi ya wakazi wa Tandale, manzese nk kuuza maeneo yao na kutafuta maeneo yalipangwa Kigamboni nk). Ofkoz, tunatatamani hawa wakulima wanaolima kienyeji wawa "phased out" softly.

Hivi ndivyo tunavyoweza kuondokana na takwimu feki za kila asiye na ajira kujiandika guest MKULIMA ilhali kazi yake ya kila siku ni kubeti kwenye draft. Ni kwa kufanya hivi ndio tunaweza kupunguza umaskini na kutengeneza Taifa lenye tija ulimwenguni.
 
Dan Zwangendaba Umeandika vizuri lakini ngoja tujadiliane kidogo.

Mwishoni mwa andiko langu nilihoji hao waliomo kwenye mradi kama ni wakulima maskini toka vijijini ama ni vijana wa kisiasa waliopelekwa huko kwenda kutumia fedha za umma kwa maslahi binafsi ya kisiasa. Lakini pia nilisema wanapelekwa kwenye Jaribio la Kilimo lisilo la kisayansi.

Maelezo yako kuhusu kuuboresha mji wa Dar es salaam, nimeyapenda ingawa hayasadifu uhalisia wa hiki tunachojadili. Hoja yangu iko hivi, leo hii huko vijijini kuna wakulima lukuki wanaoishi kwenye lindi la umaskini na wanaendesha kilimo cha kienyeji badala ya kuboresha kilimo chao wametelekezwa.

Wengine tuliposikia BBT tukajua waliolengwa ni wanaofanya kazi ya kilimo kila siku. Badala yake wamechukuliwa watu wapya kabisa na kwenda kufundishwa kulima na kufanya kilimo. Na labda nikwambie tu, siyo kwamba "Scheme" ya Bashe ndiyo ya kwanza kufanywa hapa Tanzania. Nyingi tu zimefanyika na nyingi kati ya hizo nyingi zimekufa.

Kwa nini Skimu nyingi za kilimo zimekufa? Kwanza ni kutokana na ulafi wa wanasiasa wanaoanzisha hizo skimu kutaka kufaidika nazo kibinafsi. Hakuna Skimu ya Kilimo yoyote ambayo wanasiasa hawaweki jinsi ya kufaidika nazo wakati wa skimu na baada ya Skimu. Ukichunguza kwa undani hata hiyo BBT ina usiri mkubwa sana jinsi itakavyoendeshwa kiasi kwamba mwisho wa siku hao waliomo kwenye Skimu watakuja kuona kwamba walidanganywa.

Nirudi kwenye hoja yangu. Kwa ivo wanachi maskini vijijini wanakuja kupambanishwa kwenye soko na mazao yaliyosimamiwa na Serikali kwenye Skimu ya BBT. Matokeo yake ni kwamba hao wakulima maskini watakuwa maskini zaidi kuliko walivyo sasa. Ninaposema soko namaanisha nini. Wakulima wadogo ili bei ya mazao yao iwe juu kidogo ni LAZIMA aina ya mazao wanayouza yauzwe nje ya nchi. Sasa kwa mfano kama BBT wana mahindi unadhani hao wateja toka nje ya nchi wataenda kuokoteza mahindi vijijini ama watakwenda kwenye Skimu ya BBT moja kwa moja??

Ukisoma jozi kwa jozi za vitabu kuhusu Kilimo na ushirika vijijini, wakati mwingine unaweza kujiuliza kama hivi tatizo huwa nini? Unasema kuna wakulima walifidiwa na ardhi yao kuchukuliwa kwa ajili ya SKimu ya BBT. Kwa nini badala ya kuchukua Ardhi yao hao wakulima wasijumuishwe kwenye Skimu ya BBT? Hao waliochukuliwa Ardhi yao hawataki kulima kilimo cha kisasa kinachofadhiliwa na serikali??

Kwa maana rahisi ni kwamba serikali imewatelekeza wakulima asili na badala yake imechukua vijana wa mtaani na kuwapeleka kufanya kilimo kwa kukusudia kubadili kilimo cha Tanzania. Jee serikali imeona haiwezi kubadili Kilimo cha wakulima asili badala yake imeamua kuchukua wakulima wapya??

Baadaye nitajadili kidogo kuhusu "Agriculture Production, Processing, Packaging, Storage, Marketing, Selling,na Agribusiness Information" kwa mtazamo wa serikali kuwatelekeza wakulima asili badala yake imechukua vijana wa kisiasa kwenda kufanya Jaribio la Kilimo lisilo la kisayansi.
 
Bashe anatafuta sifa binafsi na siyo tija ya kilimo.
 
Kwa kiasi kikubwa andiko langu lina majibu ya hoja zako zote hata hizo za wakulima wa vijijini na hawa vijana. Nimeeleza ugumu na changamoto ya kuboresha kilimo cha hao unaowaita wakulima wa vijijini. Na infact, kama tunahitaji kweli kilimo kiwe na mchango kwenye maendeleo yetu, hao wakulima wa vijijini hawatakiwi wawepo. Iwe kwa sasa au baada ya miaka 100. Lakini kwasababu wapo, kwa kutekeleza BBT, si kwamba Serikali imewatelekeza, hapana. Ndio maana nimetumia mfano wa jiji la Dar, kwani ikitokea Serikali ikaanzisha mji mpya nje ya mji ina maana maisha kwa Wana Tandale hayataendelea? Yataendelea. No wonder miradi kibao ya umwagiliaji inakarabatiwa na kujengwa kuwalenga "wakulima wa vijijini".

Lakini BBT ina window mbili, wapya na waliopo sasa hapo hofu iko wapi. Nimeeleza kuwa mradi unaweza kuwezesha wakulima wa vijijini ku-graduate. Kwamba as time goes, wakulima wa vijijini wataingia kwenye mfumo wa BBT (spillover effect).
 
Wakulima wadogo hawatakiwi kuwepo waende wapi ?
 
Watanzania hamjui mnachokitaka. Laiti haya anayoyaongea Hussein Bashe yangeongelewa na Bill Gates au Jack Ma au Elon Musk hakuna mtu angetia mashaka.

Anyway, Hussain Bashe ni akili kubwa na yuko creative, atawashangaza doubting Thomas's wake.
Ukiwasikikiza hao loosers hakuna kitu utafanya..

Hii Nchi Ina watu Wana mdomo.sana ila waambie wakuoneshe vitendo ni zero so sio wa kuwapa attention unawapuuza unaendelea na programu Yako.

 
Wakulima wadogo hawatakiwi kuwepo waende wapi ?
Naomba ungeelewa maana ya fact na supposition. Supposition ya kilimo kinachotakiwa ni kile kisichohusisha jembe la mkono wala kuomba dua za mvua. Ni mechanized agriculture. Ofkoz, kwa nchi yetu itachukua muda kuwaondoa wakulima hao, lakini for sure lazima waondoke (phased out not kicked out) as time goes. Hili neno la wakulima wa vijijini tumelitengeneza tu lakini kiuhalisia yapasa neno wakulima wa vijijini na mjini lisiwepo. Just wakulima tu.

Hao wakulima wa vijijini watakaposhindwa kuingia kwenye mfumo rasmi Wana hiyari mbili. Kuingia contract ya kuzalisha kwa kiwango cha wakulima rasmi na kuwauzia au kuwa vibarua/wafanyakazi wa kilimo watimize mahitaji yao . Simply hivyo.
 
Bashe huwa namuelewa sana ni miongoni mwa viongozi vijana wabunifu sana mimi nikiwa kama mdau wa kilimo naamini hajakosea na ninaamini kuna mambo mazuri yapo mbele. Kama ameweza kuhakikisha katika uongozi wake wakulima wanauza mazao ya kwa bei ya juu naami through block farming tutapata mazao bora sana na wanunuzi watakuja wa kutosha hivyo basi wakulima watashirikiana na blockfamer kupata mazao bora yatakayoendana na mahitaji ya soko.
 
Nyie loosers ni WA kupuuzwa tuu.

 
Kazi inaendelea huku 👇

 
Mambo yanazidi kunoga huku 👇

 
Waambie mapesa yanazidi kumimimika huku ajenda 10/30 strong legacy lazima iwekwe.

 
Mpango wa block farm ungefanikiwa kana ungehusisha wakulima wazoefu,bila ubaguzi wa umri!

Wakulima wenye uzoefu na mapenzi na kilimo ndio wanaweza kuvumilia suluba za kilimo!

Hawa wakulina wa kuchonga watamuangusha mno mh Bashe! Nia ya mh Bashe ni nzuri,lakini njia anayotumia ni mbaya!
 
Unafikri wakulima wadogo wakiondoka kwenye mfumo wa uzalishaji kundi kubwa kiasi gani la maskini litakuwa limetengenezwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…