Bashe amesema sio dhambi kwa viongozi wa bodi ya pamba kufanya biashara ya pamba, na wala hakuna tatizo kwa wabunge kufanya biashara hiyo ya pamba.
Jana tar 2/9/2023 Lissu aliongelea jambo hili akiwataja viongozi wa CCM ambao akiwepo Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba kutawala biashara hivyo na hivyo kuwaminya wakulima linapokuja suala la kupanga bei.
Bashe ameyasema haya katika mkutano wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais na Waandishi wa habari leo 3/9/2023
Bashe kajibu kisiasa na kutoongelea mgongano wa maslahi kwa viongozji hao wa CCM kujiingiza kwenye biashara hiyo huku wakiwa kwenye uongozi wa bodi hizo.
Ni utetezi wa kijinga na kipumbavu toka Kwa waziri!!
Anawezaje kuhalalisha makosa yake Kwa utetezi wa mbona fulani naye alifanya hivyo?
Kwa ukiri huu, ni wazi sasa kuwa, kumbe Tundu Lissu yuko damn right na kamwe hajawasingizia wote aliowataja akiwemo yeye Hussein Bashe kumiliki kampuni ya ununuzi wa tumbaku na akiwakopa wakulima huko Tabora...
==============================================
Pia kumbe ni kweli, Mwenyekiti wa bodi ya pamba ni ndugu Christopher Gachuma mjumbe wa halmashairi kuu ya CCM taifa ambaye pia ni;
1. Nidiye mnunuzi mkuu wa pamba Tanzania..
2. Ni mmoja wa wamiliki wa vinu vya kuchambulia pamba (ginneries)
3. Ni Mwenyekiti wa bodi ya pamba, bodi inayopanga bei ya pamba ya wakulima na wakati huohuo huyu Gachuma na bodi yake ndiyo isimamie maslahi ya wakulima wa pamba..
=====hapa pana mgongano wa maslahi na ukiukwaji wa maadili ya utumishi wa umma=====
================================================
Kumbe naye huyu Hussein Bashe ni mmoja wa wamiliki wa kampuni za ununuzi wa tumbaku huko Tabora na anawakopa wakulima badala ya nipe nikupe..
Halafu wakati huo huo Hussein Bashe ndiye waziri mwenye dhamana ya kilimo na kusimamia maslahi ya wakulima wakiwemo hao wa tumbaku huko Tabora..
====Katika mazingira haya, tusemeje? Je, sio kwamba huu ni mgongano wa maslahi ya umma na ukiukwaji wa sheria na kanuni za maadili ya viongozi wa umma====?
Je, ni halali na inaingia akilini kwa waziri kujitetea kwa kusema mbona fulani naye alifanya kosa kama hilo?