Waziri Bashe: Hatujapokea taarifa rasmi kutoka Kenya kuhusu kuzuiwa mahindi yetu ila magari yetu yamezuiwa!

Waziri Bashe: Hatujapokea taarifa rasmi kutoka Kenya kuhusu kuzuiwa mahindi yetu ila magari yetu yamezuiwa!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema Serikali haijapokea taarifa rasmi kutoka Kenya juu ya kuzuiwa kwa mahindi ya Tanzania kuingia nchini humo.

Bashe amesema wakipewa taarifa watachukua hatua stahiki japo mkuu wa TRA Namanga amethibitisha mahindi ya Tanzania kuzuiwa kuingia Kenya kwa kuzuia magari yenye shehena.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!

====

Arusha. Naibu Waziri wa Kilimo nchini Tanzania, Hussein Bashe amewasili mkoani Arusha kutatua kile kinachodaiwa kuwa Mamlaka ya Mapato nchini Kenya (KRA) imezuia magari ya mizigo yenye shehena ya mahindi kuingia nchini humo.

Taarifa ya zuio hilo imesambaa katika mitandao ya kijamii kuanzia usiku wa kuamkia leo Jumamosi Machi 6, 2021 ikieleza kuwa magari yamekwama katika mpaka wa Namanga.

baashe malory

Akiwa katika eneo hilo lililopo Wilaya ya Longido mkoani humo, Bashe ambaye ni mbunge wa Nzega Mjini (CCM) amesema Serikali ya Tanzania inachukulia kwa uzito unaostahili mazao yao kuzuiwa.

"Serikali inafutilia kwa karibu zuio hili niwahakikishie wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kuwa serikali itaendelea kulinda maslahi yake," amesema Bashe.
 
Kuna taarifa pia kuwa madini ya dhahabu na almasi toka Tanzania Tanzania yanachenjuliwa na vimiminika sumu. Hayafai kwa matumizi huko duniani.

Biteko naye anasemaje juu ya hili?
 
Kuna taarifa pia kuwa madini ya dhahabu na almasi toka Tanzania Tanzania yanachenjuliwa na vimiminika sumu. Hayafai kwa matumizi huko duniani.

Biteko naye anasemaje juu ya hili?
Nasema kama wamezuia hayo magari yenye shehena za mahindi basi wamwagieni kuku wale. Sisi ndio dona kantri.

#Jiwe anapigwa mtungo safari hii.
 
Dona kantri bwana kila kitu inakanusha.

Korona hakuna
Mahindi hayana sumu
Kama kweli imedhibitika mahindi ya Tanzania yanao kiwango kikubwa cha aflotoxin basi afya ya Mtanzania mashakani. Aflotoxin husababisha kansa. Aflotoxin kwenye mahindi husababishwa na kuhifadhi kwenye ghala mahindi ambayo hayajakaushwa vizuri(moisture content must be below 13% dry basis for safe storage)
 
Aliyekupa amekupa tu hata mkitia kila aina ya figisu hamtaweza kwa sababu aliyetubariki ni Mungu mwenyewe

Tuna madini
Tuna ardhi nzuri na tunalima sana tu
Tuna vivutio vya utalii kama vyote
Mungu ametuweka kijiografia kwenye eneo nzuri kuwahudumia nchi zilizoko mbali na bahari
Yaani sijui niseme nini
RAISI MAKINI TUNAE

Hebu mtuheshimu tu hizi figisu hazisaidii jamani ni Mungu huyu ambaye ametupatia vitu vyote hivyo
 
Badala ya kuwasiliana na waziri mwenzake kwa upande wa Kenya anatuletea habari hizi.

Sasa anaposema hawajapokea taarifa rasmi inatusaidia nini sisi Watanzania?

Nia yetu ni kuuza mahindi Kenya na Waziri hatakiwi kuzubaa-zubaa ktk kulipatia ufumbuzi suala hili.
 
Prof. Adolf Mkenda, nenda kenya katie hili tatizo. Wewe kwenu Rombo ,na warombo na wakenya mnaelewana. Huyu Dogo hawezi hiyo kazi.
Dogo[bashe] anaenda kutembelea mpaka wa namanga, badala ya kuwasiliana na viongozi wenzake kwa upande wa Kenya.
 
Watakua washapata kwa msaada wa Marekani
 
Back
Top Bottom