Waziri Bashe: Hatujapokea taarifa rasmi kutoka Kenya kuhusu kuzuiwa mahindi yetu ila magari yetu yamezuiwa!

Waziri Bashe: Hatujapokea taarifa rasmi kutoka Kenya kuhusu kuzuiwa mahindi yetu ila magari yetu yamezuiwa!

Aliyekupa amekupa tu hata mkitia kila aina ya figisu hamtaweza kwa sababu aliyetubariki ni Mungu mwenyewe

Tuna madini
Tuna ardhi nzuri na tunalima sana tu
Tuna vivutio vya utalii kama vyote
Mungu ametuweka kijiografia kwenye eneo nzuri kuwahudumia nchi zilizoko mbali na bahari
Yaani sijui niseme nini
RAISI MAKINI TUNAE

Hebu mtuheshimu tu hizi figisu hazisaidii jamani ni Mungu huyu ambaye ametupatia vitu vyote hivyo
Kuleni tu mahindi yenu maana nyie mna kila kitu, lakini ukweli unabaki palepale uhifadhi wa mahindi Tanzania ni wa kichawi. Kati ya watu wanaokula mishahara bure ni maafisa ugani kilimo.
 
Ndo maana Mimi sili ugali
Kama kweli imedhibitika mahindi ya Tanzania yanao kiwango kikubwa cha aflotoxin basi afya ya Mtanzania mashakani. Aflotoxin husababisha kansa. Aflotoxin kwenye mahindi husababishwa na kuhifadhi kwenye ghala mahindi ambayo hayajakaushwa vizuri(moisture content must be below 13% dry basis for safe storage)
 
Au wakenya wanahasira na tz kwa sababu ya kufurusha nzige wakarudi huko kwao, yawezekana ndio waliowatuma hao nzinge waharibu mahindi yetu.
Huyu ni Mwenyekiti wa CCM mkoa, halafu kwa mawazo haya unategemea Tanzania kupata maendeleo??
 
Upo sahihi lakini kuna baadhi yao ushirikiano wao hauna jema nasi na wengi wa mataifa hayo wanasumbuliwa na kijicho
Akili za ajabu hizi! Hivi umewahi kwenda kwenye maghala ya shirika la hifadhi ya chakula wakati wananunua mahindi ukaona yanavyohifadhiwa au yanavyorudishwa kwa wakulima kwa kukosa ubora? Na yanaporudishwa huko kwa wakulima yanakwenda wapi? Si ndo haya yanayonunuliwa na wafanuabiashara wa kati kupelekekwa Kenya na DRC? Nani anaset kiwango cha uhifadhi wa mahindi kwa kutumia dawa za kuhifadhi ambazo nyingi hazina viwango? Unapomlaumu jirani kwa kumzuia mwanao kwenda kwake, chunguza kwanza tabia ya mwanao.
 
Huyu ni Mwenyekiti wa CCM mkoa, halafu kwa mawazo haya unategemea Tanzania kupata maendeleo??

Waziri Bashe: Hatujapokea taarifa rasmi kutoka Kenya kuhusu kuzuiwa mahindi yetu ila magari yetu yamezuiwa!.,........ Acha kupoteza ufahamu, ulipokuta mamia ya malori yamekwama kuingia Kenya, tayari hiyo ni taarifa, cha kufanya ni kuingia upande wa pili wa Kenya na kuanza kutafuta chanzo cha tatizo. Wakenya wako smart kwenye utendaji, huku ukiwa mwenyekiti wa ccm unapandishwa cheo unakuwa mkuu wa Mkoa,kenya ni opposite, lazima uwe professional ili update kazi za serikali. Ushauri wangu, Prof Adolf Mkenda na Balozi wa Kenya nchini Tanzania wakutane mara moja ,tatizo litamalizika. Pili Balozi ya Tanzania aliyeko Kenya apangiwe kazi nyingine, Tatu , DC wa Longido ni mpigaji na anaendekeza siasa mpakani ,apangiwe kazi nyingine. Prof Kabudi haeleweki, tatizo lipo manga yeye yuko Kigoma snapiga siasa.​

Hiyo ishu ilikua kimya kimya nadhani wakenya wameamua kulitangaza mwanzo ilikua wanasumbua vibali vyao na inakua rahisi kwa wakenya na truck zao kupeleka mahindi Kenya sasa hivi imekua kwa wote sijui biashara ya mbuzi ipoje maana nayo niliona imeingia mchanga ila haijatangazwa ipo kimya kimya...Nchi yeyote ili iendelee ni kutengenezwa urafiki na Nchi jirani kwa ajili ya biashara hata urafiki wa kinafiki tuu ili mambo yenu yaende sio sasa kila kitu uadui hata wao wakileta pipi tuu wanasumbuliwa mno utadhani sijui nini...
 
Kapuku Tanzania atamfanya nini Kenya ?
Mkuu hebu kua na kauli za kizalendo kwa hili la kenya ni fitna kama fitna zao nyingine na tukijibu mapigo hao wakenya pumzi itakata mapema sana subiri uone

Japo hatuukubali uongozi wa jiwe lakini Tanzania inapofanyiwa fitna lazma tumuunge mkono anapo deal na washindani wetu kiuchumi

Umesahau ni miaka ya juzi tu walitufanyia fitna kwenye utalii tulipojibu mapigo wakaanza kulia lia.

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Hizo akili labda umenyimwa peke yako kiongozi.
Kama kila kitu unadai unacho mwenzako anatumia advantage ya wewe kushindwa kutumia mali zako, kwa akili yako unadhani utakuwa umepungukiwa na nini.
 
Mkuu hebu kua na kauli za kizalendo kwa hili la kenya ni fitna kama fitna zao nyingine na tukijibu mapigo hao wakenya pumzi itakata mapema sana subiri uone

Japo hatuukubali uongozi wa jiwe lakini Tanzania inapofanyiwa fitna lazma tumuunge mkono anapo deal na washindani wetu kiuchumi

Umesahau ni miaka ya juzi tu walitufanyia fitna kwenye utalii tulipojibu mapigo wakaanza kulia lia.

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
Endeleeni kuchoma moto vifaranga vyao
 
Nainu waziri wa kilimo Hussein Bashe amesema serikali haijapokea taarifa rasmi kutoka Kenya juu ya kuxuiwa kwa mahindi ya Tanzania kuingia nchini humo.

Bashe amesema wakipewa taarifa watachukua hatua stahiki japo mkuu wa TRA Namanga amethibitisha mahindi ya Tanzania kuzuiwa kuingia Kenya kwa kuzuia magari yenye shehena.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!

====

Arusha. Naibu Waziri wa Kilimo nchini Tanzania, Hussein Bashe amewasili mkoani Arusha kutatua kile kinachodaiwa kuwa Mamlaka ya Mapato nchini Kenya (KRA) imezuia magari ya mizigo yenye shehena ya mahindi kuingia nchini humo.

Taarifa ya zuio hilo imesambaa katika mitandao ya kijamii kuanzia usiku wa kuamkia leo Jumamosi Machi 6, 2021 ikieleza kuwa magari yamekwama katika mpaka wa Namanga.

baashe malory

Akiwa katika eneo hilo lililopo Wilaya ya Longido mkoani humo, Bashe ambaye ni mbunge wa Nzega Mjini (CCM) amesema Serikali ya Tanzania inachukulia kwa uzito unaostahili mazao yao kuzuiwa.

"Serikali inafutilia kwa karibu zuio hili niwahakikishie wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kuwa serikali itaendelea kulinda maslahi yake," amesema Bashe.
Hatua stahiki ni kuhakikisha kuwa mazao yetu hayana sumu. Tunatakiwa kuwashukuru wakenya maana hayo mahindi hata sisi tunauziwa. Serikali inatakiwa kuanzisha utaratibu wa ku monitor mazao yetu kabla hayajaingia kwenye masoko ya ndani na nje. Hii sio mara ya kwanza kugundua kuwa watu wako tayari kuhatarisha maisha ya wenzao kwa tamaa za faida ya haraka haraka. Kuku wanalishwa dawa za ajabu ili wawe wakubwa, pombe zinachanganywa na uchafu wa kila namna ili zivutie wateja, samaki kuvuliwa kwa sumu na baruti n.k.

Hii tabia ya kila wakati kujiona sisi ni victims inatugharimu sana.

Amandla....
 
Nimekuelewa bwashee!
 
Badala ya kuyapima na kujiridhisha ili kubadilisha mfumo wa kuya hifadhi mambo yanakuzwa ili kuongeza tatizo. ivi Uganda wanasemaje.
 
Ndio inalipizwa? Subiri majibu atayapata soon
Badala ya kufanya ujinga ujinga wa kupayuka nadhani ingekuwa muhumu sana Tanzania ijiulize na iangalie ukweli kama mahindi yana kiwango cha juu cha hiyo sumu. Hiyo sumu ni mbaya na madhara yake yanaonekana baada ya muda mrefu. Na mbaya zaidi yanaweza kumpata mtu yeyote akiwemo wewe unayendika upumbavu hapa. Hatua ya kwanza ilikuwa na serikali kuwasiana na Kenya na pia kuhakikisha imefanya uchunguzi wa kina kuhusu haya madai. Na siyo mahindi tu. Tanzania kuna bidhaa nyingi ambazo zinaweza kuleta madhara kama serikali haitakuwa makini kupima viwango vyake. Vitu kama mboga mboga, nyama, kunde nk ni vitu ambavyo kama madawa yakitumika vibaya wakati wa kuzalisha athari yake inakwenda mbali.
 
Inasikitisha sana...

Mabeberu hao wanaitumia Kenya dhidi ya Tanzania...
 
Back
Top Bottom