Inanibidi kujiuliza sana na hizi hatua wanazochukua hawa viongozi hii tabia ya kujiuza kama bidhaa huko nje. Bidhaa bora, ambayo kwa kila kigezo Tanzania ni bidhaa bora kabisa kati ya mataifa mengi duniani; kwa nini ijifanye kuwa bidhaa hafifu kiasi hiki cha kujitembeza kama malaya kila sehemu.
Hawa viongozi kama siyo kuwadharau na kuwaona wanachi wao kuwa chini ya viwango vya watu wengine duniani, kwa nini hawana imani na uwezo wa hawa waTanzania kuleta maendeleo ndani ya nchi hii?
Mpango huu wa mashamba, kwa mfano, kuna nchi yoyote duniani iliyowahi kuutumia kama model ya kuleta maendeleo, au ni mpango tu umebuniwa na kufanyiwa majaribio kwa Tanzania?
Ni nchi gani duniani ilileta mageuzi makubwa kwa kutegemea wawekezaji toka huko nje, huku wananchi wake wakiambulia makombo na hisani za hao wanaoitwa wawekezaji?
Mwigulu na wenzake wote, na hasa huyo mama anapashwa kutumia muda wake mwingi kufanya kazi na waTanzania, hapa hapa, na hasa huko vijijini kuliko kwenda kujitembeza kama malaya huko nje.
Wananchi wetu ndio wanaohitaji mazingira mazuri ya kuwezesha juhudi zao kuzaa matunda, siyo kwenda kutafuta watu watakaotuletea matatizo zaidi na kututawala nyumbani kwetu wenyewe. Mazingira ya kuwavutia hao wawekezaji ni mabadiliko yatakayoletwa na juhudi za waTanzania kwa kazi zao wanzozifanya.
Wachina hawakusubiri au kwenda kujitembeza kutafuta wawekezaji. Wawekezaji walipigana vikumbo wenyewe kwenda China walikuoona kuna kazi na na mazingira mazuri yaliyowahusu wananchi wa huko.
Hawa viongozi wana tabia za kitwana sana, na wanaifanya nchi hii iwe kama ya watwana.