Waziri Bashe na wizara mnaandaa Watanzania kwa mipango ya upigaji

Omba basi wakuteue utende miujiza
 
Ni waziri ambaye ameua kilimo kabisa kazi yake ni kupiga kelele tu
 
Ni mwendo wa kuzindua tu, kabla hili halijafika popote wanafanya hafla ya kuzindua lingine, Ni hafla za uzinduzi kwa kwenda mbele. Ikitoka hafla inafata warsha inafata semina , afu tunarudi Tena kwenye hafla. Kukagua kwamba hili limefikia wapi hamna.
Umesahau kusema kote umo pesa zinatafunwa sio kwamba bure bure ni pesa za Kodi zinatumika
 
Ni waziri ambaye ameua kilimo kabisa kazi yake ni kupiga kelele tu
Kuna mbunge alimpinga bungeni huwezi ukaenda kumchukua kijana amesomea udaktari unamwambia eti kwa kua haujapata kuajiriwa Basi akalime au kijana kasoma Tehama unamwambia kwa kua haujapata kuajiriwa twende ukalime ingawa KILIMO kinalipa
 
Nguvu kubwa imewekwa nje ya kilimo chenyewe. Bahati mbaya raisi sio mjuzi sana na wala hana tatizo na Hilo
Wizara imenunua Land cruiser za kutosha kwa ajili ya block farming, inashangaza sana
Mkuu vipi na huko Norway, kuna upuzi na utopolo kama huu?
 
Yaani mradi ndo kwanza umeanza alafu unasema upigaji alafu wala huweki wazi huo upigaji with facts and figures.
Tz tuna safari ndefu sana kufika tuliko kila mtu mjuaji.
Au usikute nawe ndo wale wamekosa nafasi kwenye ilo kundi la vijana
 
Bashe maneno mengi nimekuja kumgundua kwenye deliverance yuko nyuma mno, anaweka viterm vyake vya uongo na kweli unaweza kusema ni akili kubwa kumbe kichwani hamna kitu
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] "It is very danger".Yule jamaa msanii sana!
 
kwa maono yangu naona bashe ndio moja ya mawaziri waliokuja kivingine katika suala la kilimo na kulibeba jukumu la waziri(kazi kuu ya waziri ni kuja na sera yenye utofauti na sio upuuzi wa kufokafoka na kutumbua au zima moto)
ni vyema kuwapa mtaji na kuwahakikishia soko wakulima vijana waliosomea au wenye uzoefu ili waajiri watanzania wengine.
Lengo la program hii liwe halisia na kweli tupu yaani lazima tuwe na "must made " multbillions farmers ambao watawezeshwa kuajiri watanzania,watakaozalisha malikilimo itakayouzwa nchini (food securitu purpose) na nje ya nchi(business purpose) .
zimepita dhana nyingi sana kuhusu kilimo hebu sasa tutengeneze "mafisadi" wa agro business ...ma settlers wa kibongo
wengi kila mkoa au kanda ambao wataenda "kutema" au kuvamia misitu iliyopo Africa .na pia tupate updates namna walivyoajiri na namna watakavyo -encroach soko la EaC na SADC.

TISS iwekee mkakati mahsusi katika hii dhana ya Bashe kikamilifu tunaweza kutoka hapa tulipo.


KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
 
Eti Kilimo kibadilishwe na kundi la vijana mia nane tu ambao hawana hata background ya kilimo.

Kesho siyo mbali itatupa majibu ya kusikitisha.
 
Sikia wataalamu wa Bashe kwenye kuandaa BBT project!
Your browser is not able to display this video.
 
Sikia wataalamu wa Bashe kwenye kuandaa BBT project!View attachment 2563647


Mwangalie huyo dada mwenye t-shirt ya njano, wapembeni yake mwenye kilemba na dada mwingine nae kavaa kilemba cha njano upande wa pili na miwani.

Kwa muonekano wao tu hao ni watu wakulima shamba la hector 10 peke yao. Sampuli hiyo imejaa kibao, yupo mmoja nimemuona kwenye video wakati wanawasili kwenye mafunzo ata kuburuza begi lake mwenyewe aliloenda nalo kasheshe ndio akalime heka 10.
 
'Mayor', unaweza kuua bila kukusudia. Nimecheka sana hadi machozi yakanitoka.

Hapana. Tunaweza kusema kwamba hawa ni ma-'agents' tu wenye kazi zao wapo mafichoni. Kwa hiyo kazi inaweza kuendelea kwa baadhi yao vizuri kiasi.
 
Bajeti ya wizara ya kilimo alisema imeongezwa Mara 3 ya mwanzo hadi kufikia bil 750, hebu sema nini kimebadilika hadi sasa?
Kwa uhakika kabisa naamini Rais anajua uchizi anaofanya Bashe, tatizo tunaendesha nchi kwa ushirika na urafiki. Huwezi kuruhusu Bashe aendeshe Wizara kwa ubinifu ambao haujapitishwa kitaifa, halafu unaancha taarifa rasmi ya kitaifa inayoeleza jinsi ya kuinua kilimo nchini. Halafu anatum,ia pesa kununua pikipiki na magari bila hata faida ya maana.

Bashe hajui chochote ktk kilimo, ina maana anategemea wataalamu wa Wizara. Mtaalamu gani ktk wizara atashauri mbinu za aina hii wakati anafahamu kulikuwa na ASDP I na sasa ni ASDP II.
 
Serikali iache blah blah ,kwanini wasiandae mashamba + mfumo wa kuwajengea kilimo cha umwagiliaji(irrigation schemes)kwa kila vijiji
Na huko wawepo mabwana shamba

Ova
 
Serikali iache blah blah ,kwanini wasiandae mashamba + mfumo wa kuwajengea kilimo cha umwagiliaji(irrigation schemes)kwa kila vijiji
Na huko wawepo mabwana shamba

Ova
Hilo pekee lingeleta transformation kubwa sana kwenye kilimo.

Siyo hizi blah blah za Bashe
 
Nchi zetu hizi viongozi hawapangi mambo kwa manufaa ya taifa au wananchi. Kila waziri anahakikisha anafaidika na wizara aliyopo, hata kama akiondolewa anakua amefaidika yeye binafsi. Ni wengi wa aina ya Bashe. Hata ujenzi wa kiwanja cha ndege Msalato waziri anaendesha biashara zake za kokoto.

Anayefahamu kilimo hawezi kubuni uhuni wa aina hii. Hii ni nchi ambayo tunaambiwa tatizo kubwa ni ukame na ufumbuzi ni umwagiliaji ktk maeneo ambayo wizara inayajua kwa miaka 60 iliyopita. Sasa waziri anaacha mipango yote inayoeleweka!

Aibu ni kwamba Rais yupo anaangalia tu! Wabunge nawalaumu kwa kutoliona tatizo la waziri, lakini siwalaumu kwa kutokataa maana hakuna mpango wa serikali ambao umewahi kukataliwa bungeni. Spika huhakikisha yote yanapita, kila semacho waziri ni jawabu hata matusi ya mawaziri kama Mwigulu yanavumiliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…