Waziri Bashe tafakari uwezo wako kabla hujaharibu kabisa sekta ya Kilimo


Bashe ana mipango mingi sana ambayo anataka avifanye kwa pamoja kitu ambacho kitamuangusha vibaya,huku alizeti,huku vijana, huku ngano,huku ku control soko,huku umwagiliaji vyote hivi wengi hawakuvipata kwa miaka michache walianza kimoja kimoja. Wakulima wa kweli sio sisi wa mitandaoni hawa vijana wanaomaliza SUA wangekuwa wanawezeshwa kwa kuwekwa pamoja na wakulima wakongwe basi wangesaidia sana then wajenge mabwawa mengi kwa ajili ya umwagiliaji then waone mambo yanaendaje kwa miaka miwili. Hii ya kuwafindisha vijana ukulima ambao wengi wameenda kwasababu ya kukosa ajira tu sio passion yao.b
 
Kwani unadhani ana mipango? Huyo mpigaji tu! Angalia vituko vyote anavyofanya, vinahusisha pesa nyingi. Aliamua kununua pikipiki kwa maafisa nchi nzima. Tangu lini pikipiki ikaleta mapinduzi ya kilimo? Kwa nini asingewapa matrekta wakulima?

Pikipiki zilishakuwepo miaka mingi iliyopita na zingine bado wanazo maofisini; Trail 90 na 110. Je, zilisaidia kilimo?

Naamini huyu Bashe na rais, lao moja. Waziri anatengeneza pesa zinatumika kwa mambo yao binafsi. Hakuna rais anayeweza kukubali ujinga kama huu unaoendelea ktk kilimo. Waziri anaacha mpango mkakati wa wizara, uliopitishwa na serikali, anafanya ya kwake na rais anashiriki kumshangilia, eti wanaoneshana pikipiki inavyozuiliwa kwa mtandao isiwake nje ya eneo la mfanyakazi. Hicho ndo kilimo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…