Hili tatizo linahusu zaidi sisi Waafrika ni kwamba ukishaambiwa ni kiongozi mara unajitia ufahamu kichwani kuwa wewe una akili, hekima na busara katika kila jambo kuliko kila mtu unayemwongoza au ambaye hana cheo juu yako! Kwa maneno mengine ni kutokujua maana ya uongozi kwa sababu ya ama shule nyembamba, uzoefu finyu au kiburi. Ukitazama historia, utakuta watu hawa wanazidiwa hata na Ma chifu wa jadi au Sultani ambao walikuwa na jopo la washauri ambao waliwasaidia kuziba mapengo ya uwezo wao.Uzuri, hawa watu mwishowe huwa wanagundua tatizo lao lakini wanakuwa wamekwisha kosa fursa ya uongozi wakati huo. Nitatoa mifano hivi karibuni.
Sent from my ONEPLUS A5000 using
JamiiForums mobile app