Kwa ufahamu wangu, sekta ya kilimo hapa nchini, pamoja na matatizo yake meengi mengine, sekta hii pia iko "inadequately financed".
Hivyo basi, jitihada zozote zile za kukitafutia fedha kilimo, kwangu mimi jitihada hizo ni njema.
Yeye Bashe kama mtu anayesimamia sekta hii, anapofurukuta kutafutia mianya ya ku inject hela kwenye kilimo, mimi ninamuelewa. (Hata kama anatumia njia ambazo pengine hazijazoeleka sana).
Sina mashaka kabisa na utaalam wa mambo ya fedha na masuala ya uchumi wa watu wa BOT, lakini tusifunge milango kwa any possible suggestions (hata kama zinaweza ku sound unusual) kwa kivuli cha kwamba "eti" wao watu wa BOT ni wataalam.
Mtazamo wangu ni huo, sijaona kama waziri amejaribu "kuwapanda kichwani" BOT au ameleta "ukilimo" kwenye mambo ya fedha.
NB: Sekta ya kilimo kwa muda mrefu ilitawaliwa na "uzamani pamoja mazoea", angalau naziona jitihada za viongozi wa sasa (kwa ngazi ya wizara), kuki commercialise na kukipa usasa kilimo. Pengine jitihada zao hizo zinanipofusha kuona makosa makubwa (terrible mistakes) ambayo Waziri Bashe anayafanya, kama mnavyoyaona wenzangu.