Waziri Bashungwa aagiza ukamilishaji wa ujenzi wa vituo vya afya 233 kabla ya Aprili 2022

Waziri Bashungwa aagiza ukamilishaji wa ujenzi wa vituo vya afya 233 kabla ya Aprili 2022

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2021
Posts
19,582
Reaction score
14,167
Twende kwenye mada.

Unaweza mbeza na kumchukia na ukamfanya vyovyote unavyojiskia ila ukweli itabakia pale pale kwamba rekodi anazoweka mh.Rais SSH hazijawahi kuwekwa na Rais yeyote aliyemtangulia.

Afya ikiwa ni moja ya kipaumbele chake, Serikali inajenga jumla ya vituo vya afya vipya zaidi ya 233 Kwa mpigo.

Hii ni sekta moja tuu ya Afya, ukienda sekta ya maji hivyo hivyo, barabara hasa za Tarura kote mambo ya bam bam.

Licha ya wenye chuki nae kuwa busy kutunga uongo na uzushi lakini ukweli wa kwenye Takwimu unambeba.

Mungu mbariki Rais wetu, huyu sasa ndio anafaa aongoze hadi achoke kama Angel Markel.

Kazi iendelee 👇

=============

BASHUNGWA AAGIZA UKAMILISHAJI WA UJENZI WA VITUO VYA AFYA 233 KABLA YA APRILI 2022

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa ameziagiza Halmashauri zote nchini zilizopokea fedha kuanzia mwezi Oktoba – Disemba 2021 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya 233 kuhakikisha vinakamilika ifikapo tarehe 30 Aprili, 2022.

Akiongea na Waandishi wa Habari leo tarehe 16 Machi, 2022 baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya cha Igawilo Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mkoani Mbeya Waziri Bashungwa amesema halmashauri ambazo haitakamilisha ujenzi hawatapewa fedha za kuendeleza ujenzi.

Bashungwa amesema kwa Halmashauri zitakazoshindwa kukamilisha ujenzi kwa wakati uliotolewa na Serikali, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri watachukuliwa hatua za kinidhamu, hivyo amewaagiza Wakuu wa Mikoa yote nchini kuhakikisha wanasimamia ukamilishaji huo.

Ameagiza majengo yote ya kutolea huduma yaliyokamilika katika maeneo mbalimbali nchini kuanza kutoa huduma kwa wananchi na sio kuyaacha na kuwa kama magofu, watakaobainika majengo yamekamilika na hayatumiki serikali haitasita kuwachukulia hatua.

Vilevile, Waziri Bashungwa amesema Jumla ya shilingi bilioni 243.9 zimetolewa katika kipindi cha mwezi Julai 2021 hadi Februari,2022 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya kutolea huduma ya msingi .

Amefafanua kuwa fedha kiasi cha shilingi bilioni 113.7 ruzuku ya ndani kwa mwaka 2021/22 zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali za Wilaya 104, shilingi Bilioni 66.3 kwa ajili ya kuendeleza na kukamilisha Ujenzi wa Hospitali hizo ambazo zilianza ujenzi katika mwaka wa fedha 2018/2019 na 2019/2020.

Waziri Bashungwa ameendelelea kusema jumla ya shilingi bilioni 21.8 kwa ajili ya ukamilishaji na ukarabari wa vituo vya afya 61, bilioni 22.6 kwa ajili ya ukamilishaji wa zahanati 141 na ununuzi wa vifaa tiba bilioni 3.1 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

Aidha, Jumla ya Shilingi billioni 44.5 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa Majengo ya dharura 80, Wagonjwa mahututi majengo 26, Kituo cha matibabu ya magonjwa ya mliopuko 1 na Nyumba za watumishi 150(3 in 1) ambazo zitachukua familia 450.

Chanzo: TAMISEMI
 
Professional neurosurgeon

With MpH

Endelea kuongelea upumbavu na vibando vyako vya kuhongwa

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Wewe utakuwa professional wa kukalia 👇

20220216_225742.jpg
 
Back
Top Bottom