Waziri Bashungwa atoa maagizo kuhusu malalamiko ya wananchi katika stendi ya Magufuli Dar Es Salaam

Waziri Bashungwa atoa maagizo kuhusu malalamiko ya wananchi katika stendi ya Magufuli Dar Es Salaam

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
BASHUNGWA ATOA MAAGIZO KUHUSU MALALAMIKO YA WANANCHI KATIKA STENDI WA MAGUFULI DAR ES SALAAM

Na OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla kukutana na wadau na wamiliki wa mabasi ili kuweka utaratibu mzuri ambao ni shirikishi wa utoaji huduma kwa wananchi kwenye kituo kikuu cha mabasi cha Magufuli Dar es salaam.

Bashugwa ametoa maelekezo hayo leo Agosti, 30, 2022 wakati akitoa ufafanuzi kuhusu malalamiko ya utoaji wa huduma kwa wananchi wanaoingia Mkoa wa Dar es salaam kupitia kituo kikuu cha Mabasi cha Magufuli.

Bashungwa amesema amekuwa akifuatilia kwa Ukaribu Malalamiko yanayotolewa na wananchi Kuhusu huduma zinazotolewa katika stendi ya Magufuli kwa abiria wanaoingia na kutoka katika mkoa wa Dar es salaam ambayo yanatafisiri vibaya malengo ya Serikali ya Kutenga bilioni 50 kujenga stendi hiyo.

“Kuna abiria wanaoingia mkoa Dar es salaam na kushushwa katika stendi ya Magufuli lakini wanahitaji mabasi hayo yawafikishe mjini kwenye vituo vya mabasi vilivyojengwa na sekta binafsi, kwahiyo Mkuu wa Mkoa akikuta na wadau hao wataona namna nzuri ya kusimamia suala hilo” amesema Bashungwa.

Aidha, Bashungwa amemtaka Mkuu wa Mkoa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) pamoja na wadau wengine ili kukubaliana na kuweka utaratibu utakaorahisisha utoaji wa huduma bora bila kuleta adha kwa wananchi wala kuadhiri malengo ya Serikali kujenga stendi hiyo.

Amesema Serikali inaweza kutimiza maelengo na Kusudi la Uwepo wa Stendi ya Magufuli bila kuwapa adha wananchi wanaolazimika kushushwa katika stendi na kuingia Kwenye gharama za kutafuta usafiri mwingine wa kuwafikisha mjini wakati yapo mabasi yanaweza kupita katika stendi na yakaendelea na safari ya kuwafikisha abiria Mjini.

Pia, Amefafanua kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi na kuendelea kuimarisha usalama wa wananchi na Wageni wanaoingia nchini kwa kutumia usafiri wa magari kwa kuwatambua kupitia stendi hiyo ambayo kuna idara ya Uhamiaji na vyombo vingine vya usalama.

Kwa kuondoa changamoto ambazo zimekuwa zikilalamikiwa bila kuathili uwekezaji uliofanywa na sekta binafsi nchini.
IMG-20220830-WA0185(1).jpg
 
Zamani kila basi lilikuwa na Stendi yake ila Kisutu ndio Moshi Arusha na Mnazi mmoja ilikuwa Nyanda za Juu kusini

Scandinavian walikuwa Congo st nyuma ya DDC

Bin Kleb walikuwa karibu na Yanga

Sharuks walikuwa Msimbazi

The Big Mayai walikuwa Kariakoo Sokoni
Nk...nk
 


Tunashukuru mheshimiwa kwa maamuz yako ya busara katika hili. Watu waache mambo ya kipumbafu.
 
Naunga mkono hoja,huwezi lazimisha watu kushuka Stendi ya Mbezi alafu bus hilo lina kwenda town tupu huu ni ujinga na uzwazwa wa viongozi wetu ambao muda wote wapo kwenye v8

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
makalla hata Elimi yake ni ya mashaka tu! mjinga mjinga anayefata upepo na kuroga sana.
alichokifanya ni KUPIGA DILI za Mabasi ya mwendokasi eti abiria washushwe wapande mwendokasi! mabasi 80 utegemee yahudumie watu elfu 70 kwa siku ni UPUMBAVU wa hali ya juu!

ufisadi hautaisha kwa kuchagua wahuni kama Makalla
 
Naunga mkono hoja,huwezi lazimisha watu kushuka Stendi ya Mbezi alafu bus hilo lina kwenda town tupu huu ni ujinga na uzwazwa wa viongozi wetu ambao muda wote wapo kwenye v8

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Mambo ya kijinga sana, mtu anakaa manzese, au anakaa upanga, au hata sinza, unamlazimisha ashuke mbezi ..hapo ana mamizigo,
jinga kabisa
 
Kama ndivyo, hiyo stendi ni ya nini sasa? Ukisikiliza malalamiko ya kila mtu huwezi kusonga mbele. Hilo likiruhusiwa naiona stendi ikigeuka kuwa white elephant.
 
Kama ndivyo, hiyo stendi ni ya nini sasa? Ukisikiliza malalamiko ya kila mtu huwezi kusonga mbele. Hilo likiruhusiwa naiona stendi ikigeuka kuwa white elephant.
wamesema lazma tu upite! hii ni sawa ila sio kulazmisha watu washuke
 
Zamani kila basi lilikuwa na Stendi yake ila Kisutu ndio Moshi Arusha na Mnazi mmoja ilikuwa Nyanda za Juu kusini

Scandinavian walikuwa Congo st nyuma ya DDC

Bin Kleb walikuwa karibu na Yanga

Sharuks walikuwa Msimbazi

The Big Mayai walikuwa Kariakoo Sokoni
Nk...nk
Mkongwe katika ubora wako

Waliokuja mjni juzI hawawezi kukuelewa
 
Ila haya ni matokeo ya kufanya miradi mikubwa bila kufikiri kwa kina, kulikuwq kuna haja gani ya kwenda kujenga stendi Mbezi badala ya kuinua stendi ya maana pale pale Ubungo?
Hii ndiyo point ya maana kuliko zote!!

Miradi mingine ni ya kijinga sana hata kama waimba pambio wanaipigia zumari.
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Innocent Bashungwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla kukutana na wadau na wamiliki wa mabasi ili kuweka utaratibu mzuri ambao ni shirikishi wa utoaji huduma kwa wananchi kwenye kituo kikuu cha mabasi cha Magufuli kilichopo Mbezi.

Bashugwa ametoa maelekezo hayo leo Jumanne Agosti 30, 2022 wakati akitoa ufafanuzi kuhusu malalamiko ya utoaji wa huduma kwa wananchi wanaoingia Mkoa wa Dar es salaam kupitia kituo kikuu cha Mabasi cha Magufuli.

Bashungwa amesema amekuwa akifuatilia kwa ukaribu malalamiko yanayotolewa na wananchi kuhusu huduma zinazotolewa katika stendi ya hiyo kwa abiria wanaoingia na kutoka katika Jiji hilo ambayo yanatafisiri vibaya malengo ya Serikali ya kutenga Sh50 bilioni kujenga stendi hiyo.

“Kuna abiria wanaoingia Mkoa wa Dar es salaam na kushushwa katika stendi ya Magufuli lakini wanahitaji mabasi hayo yawafikishe mjini kwenye vituo vya mabasi vilivyojengwa na sekta binafsi, kwa hiyo Mkuu wa Mkoa akikutana na wadau hao wataona namna nzuri ya kusimamia suala hilo” amesema Bashungwa.

Waziri huyo amemtaka Makalla kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra) pamoja na wadau wengine ili kukubaliana na kuweka utaratibu utakaorahisisha utoaji wa huduma bora bila kuleta adha kwa wananchi wala kuadhiri malengo ya Serikali kujenga stendi hiyo.

Amesema Serikali inaweza kutimiza maelengo na kusudi la uwepo wa stendi hiyo bila kuwapa adha wananchi wanaolazimika kushushwa katika stendi na kuingia Kwenye gharama za kutafuta usafiri mwingine wa kuwafikisha mjini wakati yapo mabasi yanaweza kupita katika stendi na yakaendelea na safari ya kuwafikisha abiria mjini.

Pia, amefafanua kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi na kuendelea kuimarisha usalama wa wananchi na wageni wanaoingia nchini kwa kutumia usafiri wa magari kwa kuwatambua kupitia stendi hiyo ambayo kuna idara ya Uhamiaji na vyombo vingine vya usalama.


Credit: Mwananchi
 
makalla hata Elimi yake ni ya mashaka tu! mjinga mjinga anayefata upepo na kuroga sana.
alichokifanya ni KUPIGA DILI za Mabasi ya mwendokasi eti abiria washushwe wapande mwendokasi! mabasi 80 utegemee yahudumie watu elfu 70 kwa siku ni UPUMBAVU wa hali ya juu!

ufisadi hautaisha kwa kuchagua wahuni kama Makalla
Unamuonea Makala .
 
Back
Top Bottom