Waziri Bashungwa atoa maagizo kuhusu malalamiko ya wananchi katika stendi ya Magufuli Dar Es Salaam

Sio Makalla viongozi wengi tu elimu zao niza kuunga unga mtu Kama waziri wa mambo ya ndani Simbachawene ambaye ni mwanasheria sijui kutoka chuo huria ukisikia argument zake za kisheria alafu ujaribu kuweka na argument kama za Lissu utabaki kushangaa tu

Waziri wa pesa naye jina tu sio lake ukimuuliza alilipata vipi ni blabla tu alafu PhD toka chup Cha dump according to kabudi

Ceo wa kampuni yetu nae ukisoma cv kuhusu background ya elimu utaishi kushangaa tu mara short course yaani majanga tu.
 
Big up Mh. Waziri. Jana ndugu yangu alishushwa Mwenge na bus tupu likaelekea Shekilango
 
Aisee enzi za maisha hizo acha kabisa!gari nyingi zilikua zikiondoka kuanzia saa 11 jioni hadi saa 3 usiku.hiyo ni nyanda za juu na kanda ya kati..
Moshi,arusha ilikua mara nyingi asubuhi
Kwacha transport,TRC (Relwe)Dar,Iringa,Mbeya...saa 2 usiku kuondoka..mnazi mmoja


Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Kazi iendelee...

Itawezekana kwa uzuri tu kuzidi kuwa stendi yenye faida kwa wasafiri na wasimamizi.. hayo mabasi why lazima yalale yanapokwenda kwa haraka. Wapewe time wapaki bila kutoka hapo, waone kama abiria watasubiria..

Sio abiria wote lazima wafike mjini, tabu ni wengi tu kutaka kufika katikati ya jiji waseme wameiona Dar...

Maeneo hayo wapewe vibali vya mahoteli, guest houses, bars, shopping malls, night clubs etc patapendwa na itasaidia kupunguza watu kufika mjini. uwe sent mpya ya biashara jijini Dar.

Transportation ya kwenda kona zote iboreshwe na kufikiria abiria wana mizigo... Bajaji zipper parking kuwe kama zile taxis za Airport ila hapo kwa bajaji kizaidi kuliko cars..
 
Waziri amekua na busara tumpongeze
Sisi watu wa mbagala tuamke saa ngapi kuliwahi bus linaloondoka magufuli terminal saa 12 asubuhi?

Popote gari zitakapopakia zipitie Magufuli zishushe/zipakie safari iendelee

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Makala hafai kuwa kiongozi. Very deep ila kwenye kijiko. Yaani Dar imemshinda.
 
Kwa vile wao wanapelekwa na maV8 hadi milangoni mwao hawajawahi kuonja adha tunayoipitia raia wa kawaida..

Juzi natoka mkoa tumeingia jijini usiku, bahati mbaya nikawa nimeshamuandaa mpokeaji pale stand maeneo ya (Shekilango/Manzese) matokeo yake tukashushwa kilazima pale Mbezi stand na hapo nilikuwa hovyo kiafya, ikabidi tukutane na mpokeaji kimara , sasa bodaboda hadi kimara mwisho wanalazimisha elfu 6 nikalazimika kukokota begi kubwa la mgongoni hadi nje ndio nikapata bodaboda kwa elfu 4... IMAGINE HII PESA INAYOTUPWA NJIANI haikidhi hata robo ya umbali wa eneo la ukaazi..

Kama swala ni ushuru wa kuingilia stand lilokuwa ni swala la kuitisha hizo 200 zao ingawa mathematically abiria wanaoingia na basi huwa wanakuwa wameshakata tiketi za kusafiria tayari.

Ukimwambia huyo Boss wa mkoa apande basi kama abiria wa kawaida kutoka Mwanza tena apewe na nusu kiroba tu cha mahindi, then aingie usiku ashuke Mbezi akapande daladala aunge zimpeleke hadi kwake Masaki atapiga chenga kibao.

"Kwakuwa hatupendi kuambiwa yasiyo ya kutusifia basi ni swala dogo tu la kuacha ubinafsi na kutojali.."
Kwenye makaratasi utakuta issue ya "stakeholders involvement" ila kwenye uhalisia ni tofauti


"Kama jela ni pazuri mpeleke mwanao" wahenga wa kisasa
 
Nakumbuka plan ilikuwa kwamba ziwepo stand 3.
1. Boko- kwa mabasi ya route ya kaskazini.
2. Mbezi- kwa mabasi ya route ya magharabi, nyanda za juu kusini, ukanda wa kati hadi kanda ya ziwa
3. Mbagala- kwa mabasi ya route ya kusini.
Wakalanguana hapo katikat
Wakaja na stand moja
 
umenikumbusha sharuks nikiwa ifakara tunatoka jioni asubuhi mapema tunashusha mizigo
 
Wanao tumia v8 masaa 24 ni wajinga na mazuzu maana wao huona mwazo yao ndo kila kitu, huduma lazima zitoa unafuu kwa watu huduma ikiwa kero basi Kuna sehemu mambo hayako sawa.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kariakoo imeoza anashindwa kuitawala ni kama hakuna serikali anarukia mabasi na abiria
 
Hili sio jambo la Waziri ila sababu ya kurushiana mpira na kutosimamia majukumu kwa idara na taasisi ndo tumefika hapo. Waziri ni ngazi kubwa atoe tamko na kupambana na usafi, kuondoka wapiga debe na stendi kukaa sawa kufika nyumbani yoyote atafika maana Dar es Salaam popote wafika usafiri upo, "binadamu hajawahi kuwa na shukrani ila mlalamikiwa kutafakari ubora na uovu wa malalamiko "
 
Kama sijakosea, kabla ya Makala kutamka ule ujinga wake huyu Bashungwa nae nakumbuka alishawahi kutamka kuwa ni LAZIMA tushushwe Mbezi, anyway business as usual, tengeneza tatizo tatua tatizo then jipongeze
 
Na hapo kachelewa. Utaratibu wa Vituo vya Mjini vya Mabasi ambavyo vimejengwa kwa fedha zetu kutumika kutunyanyasa wananchi ni utaratibu wa viongozi ambao hawana uwezo wa kufikiri. Huu ni utaratibu wa kuwatafutia biashara wenye daladala na vishughuli vidogo kwenye miji hiyo bila kujali kero wanayowaanzishia abiria ambao wametoka masafa marefu ya safari zao kuanza safari upya kwenye stendi hizo. Utaratibu huo ulikuwepo hata kituo cha Mabasi Igumbiro Iringa na hapa Dar ndiyo wanauanzisha sasa. Dodoma ujinga huo haupo. Aidha kuna wenye mabasi ambao pamoja na kupitisha mabasi kwenye stendi hizo na kulipa tozo za mji huaika, wamejenga vituo vyao vizuri tu katikati ya miji. Hayo majengo na shughuli hapo walipo haziifaidishi hiyo miji? Wanataka majengo hayo yatumikeje? Hili wazo ni sawa na lile wazo marehemu la Makonda la "car sales rooms" zote Dar kusitishwa ili wahame na kuanza upya Kigamboni ! bila kueleza hizo sales rooms zinazoachwa zitatumikaje na kama hazitumiki kwa amri yake kama atawafidia waliojenga kihalali? Ingefaa Serikali au CCM kama inapenda kuonekana ina viongozi itoe mwongozo wa ujumla na siyo majadiliano wakati athari za utaratibu huo unaotaka kujadiliwa na suluhu yake ni wazi.
 
Maagizo ya nini, ingia ground mwenyewe, piga kazi maliza tatizo in 15 minutes, nothing will be done, ni ujinga mtupu maagizo kama haya
 
Wa Ubungo, Magomeni, Kariakoo mkipaza sauti kihivyo kumbukeni wengine twaishi Mbezi, Mbweni, Gongolamboto, Kisalawe nk nk tuache kuwa wa binafsi.
 
Makala ni bomu kiutendaji.

Ni vile alibebwa bebwa ndani ya chama lakini sijawahi kuona kama anayo tija kiuongozi. Kilaanapowekwa ama kuteuliwa lazima headlines zake ziwe upande wa malalamiko dhidi ya serikali.

CCM imeishiwa viongozi ndo maana kila siku wateuliwa ni walewale hadi wafie madarakani. Dawa ni kuchagua chama mbadala ili nchi ipate uongozi sahihi.

Makala apumzike sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…