Waziri Bashungwa awataka waliojenga Barabarani kubomoa nyumba zao kupisha upanuzi wa barabara

Waziri Bashungwa awataka waliojenga Barabarani kubomoa nyumba zao kupisha upanuzi wa barabara

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Waziri wa ujenzi Innocent Bashungwa amewataka wananchi wote waliojenga ndani ya hifadhi za barabara katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kuanza kujiandaa kisaikolojia na kuondoka wenyewe kabla ya serikali kuanza kubomoa ili kupanua ujenzi wa barabara.
WhatsApp-Image-2023-10-28-at-5.47.52-PM-2048x1365.jpeg

Bashungwa aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua upanuzi wa barabara ya Rwamishenye _ kastamu maarufu kama Uganda road inayojengwa Kwa njia nne katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kwa gharama ya Sh bilioni 4.6.

Alisema kuwa ili mradi usikwame na mkandarasi kuanza kazi kwa wakati wananchi wanapaswa kupisha ujenzi na kuzingatia sheria za barabarani huku akipongeza wananchi ambao wamebomoa wenyewe na kusema kuwa ili kupunguza ajali za mara kwa mara ni lazima mradi huo utekelezwe kwa wakati na kuchochea maendeleo kwa wananchi.
WhatsApp-Image-2023-10-28-at-5.47.54-PM-780x470.jpeg

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Wakala wa barabara Mkoa wa KAGERA Mhandisi Ntuli Mwaikokesya alisema mradi huo unatekelezwa na mkandarasi mzawa ikiwa ni awamu ya kwanza lakini awamu ya pili itakuwa ni kutoka Mitaga Hadi stendi eneo la TRA mita 600 lakini Kwa hii awamu ya kwanza itatekelezwa Kwa muda wa miezi kumi na mbili.
 
Bukoba kumekucha sasa...huku stendi, huku bandari inapanuliwa, airport inawekwa taa, udsm campus ya Bukoba....
Mdogo mdogo tutafika tu

Wale wanaosema wahaya hawewekezi kwao
To let them know soon kuna hospital mpya inafunguliwa hapo Bukoba inaotwa cosad...imejengwa na wahaya wa bukoba wakiongozwa na smart na wale diaspora...ni gharama ya sh 5billion...

Na kuna mradi wa ujenzi wa uzio wa secondary za wasichana Bukoba na Omumwani...ambayo inajengwa kwa michango wa wananchi wa Bukoba
 
Nani anawaruhusu mjenge kwenye road reserve? Ondokeni ninyi watu msiofuata sheria.
Kati ya watu na road reserve kipi kimeanza kuwepo Mahalia??
Kifanya papala mtawalipa Wahaya Fidia ya kufilisi nchi![emoji854][emoji854]
 
Ni vile tu mna wasomi wengi...lakini hawarudi kusaidia kwao.

Huenda mnarogana sana.
Hawarudi kusaidia kwao?

Disemba hapa kuna hospital ya Cosad yenye gharama zaidi billion tano inafunguliwa hapo Bukoba tena imejemgwa na mzawa wa hapo Bukoba...

Hata hawajasumbuka kupata mkandarasi maana makampubi ya ujenzi ya hapo Bukoba ndo yamechukua tender zote..upanuzi wa bandari, barabara na stendi zote ni makampuni ya wazawa kwa gharama ndogo tu..


Wahaya wako wanachangishana kujenga uzio wa shule za sekondari za wasichana omwani na Bukoba secondary...

Sasa wajengeje kwao...wajenge barabara?
Mnawaonea tu bure...


Watu wa Bukoba wakirogana basi watz wote ni wachawi sasa...
 
Wale wanaotakiwa kulipwa,walipwe kwakuzingatia thamani husika ya ardhi,waondoke wapishe upanuzi wa barabara husika.Anyway,serikali iwage macho muda wote, haiwezekani mtu anajenga,anakaa happy miaka hata 20+,halafu unakuja unasema umejenga kwenye road reserve,utadhani kipindi anajenga,hakukua uongozi.
 
Kilimanjaro
Kilimanjaro mmeendelea? Lol!...tena hakuna mkoa uliostuck kimaemdeleo kama Kilimanjaro...
Tukianza na mji wa moshi...barabara zake nyingi hazina sidewalks na nyingine vumbi kabisa kama ile ya majengo...
Mji uliokuwa na daladala sasa una mibajaji hadi kero..kimsingi unarudi nyuma baada ya kwenda mbele

Hii barabara ya machame ishawekwa lami?au haya ndo maendeleo?

1697861952104~2.jpg
 
Hawarudi kusaidia kwao?

Disemba hapa kuna hospital ya Cosad yenye gharama zaidi billion tano inafunguliwa hapo Bukoba tena imejemgwa na mzawa wa hapo Bukoba...

Hata hawajasumbuka kupata mkandarasi maana makampubi ya ujenzi ya hapo Bukoba ndo yamechukua tender zote..upanuzi wa bandari, barabara na stendi zote ni makampuni ya wazawa kwa gharama ndogo tu..


Wahaya wako wanachangishana kujenga uzio wa shule za sekondari za wasichana omwani na Bukoba secondary...

Sasa wajengeje kwao...wajenge barabara?
Mnawaonea tu bure...


Watu wa Bukoba wakirogana basi watz wote ni wachawi sasa...
Bas safii...👏👏
 
Back
Top Bottom