TANZIA Waziri Celina Ompeshi Kombani afariki dunia

TANZIA Waziri Celina Ompeshi Kombani afariki dunia

‎TANZIA‬ Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani amefariki dunia wakati akipatiwa matibabuhuko nchini India.Mungua ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi
 
RiP Mama kombanii tutakukumbuka kwa Mema na Kejeli ulizokua unatumulikia nazo..

Ulale pema Mama kombaniie
 
Sasa kama hawa ma CCM hawataki kujenga hospitali nzuri hapa Tanzania na wanakwenda kutibiwa nje sio ndio kusema hawajali maisha yetu na wanatuona sisi kama wanyama…umeenda pale Mwananyamala au Muhimbili watu wanavyokufa kwa kukosa dawa za msingi??Hela alizotumia marehumu zingeokoa maisha mangapi ya walala hoi??? Au maisha ya walala hoi hayana thamani kama hao "wateule"!!!Mbona wanatuambia kuwa CCM inaamini kuwa watu wote ni sawa sasa huu usawa uko wapi wakati viongozi wakatibiwe nje na sisi wengine tutibiwe hapa Mwananyamala??!! Inasikitisha jamani
Hao unaowaita walalahoi si ndo hao hao wanajazana mpaka kufia kwenye mikutano ya ccm wakishangilia upuuzi wa ccm? HAWASITAHILI KUPATA HUDUMA BORA ZA AFYA WALA ELIMU BORA.
 
Ni kweli Celina Kombani amefariki, ila kiungwana hatutakiwi kuwashutumu wala kuwasemea mabaya waliotangulis mbele ya haki.
Hiyo ni njia yetu sote.

Inna Lillahi Wainnaa Ilayhi Raajiuun.
 
May God rest your soul in eternal peacee mama Celina Ompeshi Kombani
Hakika wote tutarejea kwake
Mungu akusamehe makosa yako yote na akuhifadhi mahala pema
 
Nimepokea kwa masikitiko sana kifo cha Mh Celine Kombani aliyekuwa pia mgombea ubunge. Kifupi sikutegemea kuwa kuna mwanaccm atakufa kabla ya Lowasa maana wamekuwa wakipita majukwaani na kumtangaza Lowasa kuwa ni mgonjwa sana kana kwamba ndiye mgonjwa namba moja nchini kumbe mawaziri na wabunge watarajiwa kupitia ccm wapo india na hawatuambii. Wakati mkipita kusema Mh Lowasa mgonjwa mbona hamkupita kutwambia kuwa Mh Celine Kombani naye ni mgonjwa tusimpe ubunge au mlitaka tumchague hivyohivyo? CCM jifunzeni kuna wagonjwa wengi ccm japo hawatetemiki!
 
Wewe unaejifanya mzima sana ujifunze na zaidi ujiulize yakikutokea leo hii watu watasema mangapi na nani atakusikitia zaidi ya hao wanaojipendekeza ili tu kesho uwape vyeo endapo utafanikiwa.
 
Hata Mtoi alifariki kabla ya mamvi
Celina Kombani alikuwa mgombea wa CCM, na kwa mujibu wa makada wa CCM hapa jamvini, na wale walioko field, wanasema Watanzania hawapaswi kumchagua LOWASSA kwa sababu LOWASSA ni "mgonjwa"{kwa mujibu wao}, Lakini hawakuwahi kuwaambia wana ULANGA, wasimchague Marehemu Kombani kwa sababu ni mgonjwa na amelazwa INDIA! Mungu sio mjinga kama nyie akina Boko haram huu ni mfano tu amewapa! Msipoweza kujifunza hapa! Hamtajifunza tena!
 
Last edited by a moderator:
Tangu wiki iliyopita taarifa ya kifo chake zilisikika, rip mama, nakumbuka mara ya mwisho tulikuwa wote kwenye kikao mwezi wa 7 kisikiliza kero zetu
 
R.I.P mama yetu C.Kombani. C.C.M acheni roho mbaya kuwachuria wengine kifo. Kila mmoja wetu anatembea nacho.
Hivi Lowasa na timu ya UKAWA watazuiwa kuhudhuria mazishi kama walivyofanya kwa mzee Kisumo?
 
Back
Top Bottom