DOKEZO Waziri Dkt. Gwajima, fanya yafuatayo ili kuwakomesha wahuni (beach boys) wote katika fukwe zetu za Dar es Salaam

DOKEZO Waziri Dkt. Gwajima, fanya yafuatayo ili kuwakomesha wahuni (beach boys) wote katika fukwe zetu za Dar es Salaam

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Salaam Mheshimiwa, kwa nini fukwe zote zinazotumika na wananchi zisiwe na Life Guard Officers? Naamini katika hawahawa Beach Boys wapo wenye tabia nzuri ambao wakiwa trained wanaweza kufanya kazi hiyo Vizuri tu kwa kulipwa pesa kidogo either kwa masaa, siku au Wiki. Kwa namna moja au nyingine serikali pia itakuwa imetoa ajira kwa vijana wengi wanaoranda randa kwenye fukwe zetu nzuri. Nipo tayari kusaidia ushauri na mbinu mbalimbali iwapo nitahitajika kwa kazi hiyo.
Asante.
Haya ndiyo maoni ya kwenda kuwasilisha kule kwenye timu yetu ya kisekta Ili waone Jinsi ya kufanya kupitia wizara husika yenye dhamana na maeneo haya na huduma za maeneo haya.
 
..beach boyz ni kero.

..kwenye nchi za wenzetu hakuna mambo ya kusumbuliwa na wachuuzi wa bidhaa mbalimbali wakati umepumzika beach.

..pale beach panatakiwa pawe na watu wa uokoaji na watalii wanaopumzika au kuogelea. Mtembeza bidhaa asiruhusiwe kufika ufukweni na kuisumbua wateja.

..ng'ambo ya beach ndio kunapaswa kuwe na maduka ya bidhaa mbalimbali na migahawa.
 
Nadhani Kuna umuhimu wa kumuanzishia UZI maalum wa Dr. Dorothy Gwajima kwa ajili ya kujibu hoja zetu.

Nadhani ingesaidia sana na ingeacha legacy kubwa sana Maxence Melo
 
..beach boyz ni kero.

..kwenye nchi za wenzetu hakuna mambo ya kusumbuliwa na wachuuzi wa bidhaa mbalimbali wakati umepumzika beach.

..pale beach panatakiwa pawe na watu wa uokoaji na watalii wanaopumzika au kuogelea. Mtembeza bidhaa asiruhusiwe kufika ufukweni na kuisumbua wateja.

..ng'ambo ya beach ndio kunapaswa kuwe na maduka ya bidhaa mbalimbali na migahawa.
Mkiyataka hayo nendeni beach ambazo watu wamewekeza pesa zao kuifanya sekta ya beach kuwa na hadhi nchini.
Mnaenda changanyikeni cocobeach ambapo hadi mbwa coco wanaogelea mnategemea nini?
Vitu vingine ni kujiongezaga tu.
 
Tatizo la huyu bibi ni udini, ungekuwa dini yake ungepewa kila aina ya sifa.

Labda noseme kidogo;.Ukiwa KIONGOZI ni vyema ukajifunza kuyasikia usiyotaka kuyasikia.

Ukosoaji wa FaizaFoxy japo uko very harsh lakini ukiukubali inaweza kukusaidia kufanya kitu.

pokea sifa pokea na ukodoaji.

mimi binafsibnakushukuru kuna vitu kadhaa niliwasilisha kwako uli respond vizuri...asante kwa hayo.

pia siachi kukishauri uongeze bidii kwa ubunifu kuifanya jamii yetu kuwa bora..
Asante

Nimefika ndugu yangu. Ingawa ukifika tabu, usipofika tabu kama kwa Hawa ndugu zetu akina FaizaFoxy[emoji28]. Utasikia... Reactive siyo Proactive... Sasa sijui mambo ya dharura tuyaache tu nchi ya watu million 60 na changamoto zetu utakosa vipi dharura mbalimbali.... Na utapata wapi mifumo ya [emoji817] kukinga? Hata huko kwenye sekta kongwe Wana emergency services. Sijui shida ni Sababu mm ndiyo nawahi kuona au tabu wapi? Si ndiyo kidigitali hiki jamani? Au nawaza vibaya...

Normal chanel na zenyewe zipo call center tumetangaza Kila Leo... [emoji28] ahsante Sana .. twende kazi sisi... Wanadamu watasema tu....

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
1. Tangaza haraka Kuzuia vile Vijiwe vyote vya Kukodisha Mapira / Matairi ya Kuogelea

2. Kisha amrjsha wanaotaka Kufanya hiyo Biashara Kwanza wajisajili Kwenu (Serikalini) na wekeni Ada / Tozo Kubwa ili kama kuna Watakaojitokeza basi wawe ni Watu Serious na siyo hawa Wahuni walioko

3. Kwa kila atakayejitokeza mlazimisheni awape Picha zake na mjua Makazi yake na taratibu zingine za Kiusalama dhidi yao zifanyike kama njia ya Kuwadhibjti.

4. Kuwe na Chama chao Beach Boys ambacho Kitatambulika nanyi Mamlaka na walazimishenj Wanachama wao (nikimaanisha Vijana wao Wanaofundisha Watu Kuogelea Baharini) wawe ni Watu very Professional na Ethical pia

5. Serikali (Mamlaka) iweke Matangazo katika Beach zote (tena yawe Makubwa) kuwa Mabinti / Wanawake ambao watafanyiwa Ukatili huo wapige Simu upesi kwa Mamlaka zenu ili Wahusika wakamatwe.

6. Himizeni kwa Beach Goers Wote hasa Wanawake / Mabinti kuwa kama wanataka Kufundishwa Kuogelea na Beach Boys basi wawachukue wale ambao ni qualified na kutoka sehemu husika.

7. Beach Boys wote watakaowepo iwe ni AMRI lazima wawe na Vitambulisho na Uniform ili irahisishe hata Kujulikana mapema wakifanya huu Uhuni wao.

8. Katika Beach zote wekeni Eneo Maalum (ndani ya Maji) la Watu Kufundishwa Kuogelea kwani moja ya Mbinu Kubwa itumikayo na hawa Wahuni (Beach Boys) ni kwenda na Wahusika katika Directions ambazo hakuna Watu Wengi na kwenye Kina Kirefu kisha wanafanya huo Uhuni wao.

9. Mkazo uwekwe zaidi kwa Watu Kujifunza Kuogelea katka Vituo Maalum au Shule za Uogeleaji (hasa Swimming Pools) ili basi wakiwa wanaenda Baharini wawe ni Wajuzi na siyo Watafuta kujua Kuogelea ambako hukutana na hawa Wahun

10. Tungeni Adhabu Kali na isiyo na Huruma dhidi yao ili Kulimaliza hili tatizo na kuleta Nidhamu katika hayo Maeneo husika (Beaches)

11. Ili Kuwakamata tumieni huu Mtego wa kuwatafuta Mabinti (Wanawake) Watatu tu ambao wanajua kweli Kuogelea au mkiweza Wachukueni wa pale Navy Kigamboni kisha Wapandikizeni katika kila Beach.

Wakiwa huko Wahimizeni wajifanye hawajui kabisa Kuogelea kisha wavalie Nguo za Kutamanisha na wawe Wanajibebjsha kwa hao Beach Boys.

Wakati mnapanga hili pia mnawapanga Watu (huku nchi Kavu) wakiwa na Camera za Ujasusi wanawachukua ili kuwa na Ushahidi very Vivid ambao hawataweza Kuruka.

Pia hakikisheni mnawatafuta Wavivu na Mitumbwi yao ili wakati mnazifanya hizi Oparesheni nao Wawe wanajifanya kama vile wako Baharini wanaendelea na Shughuli zao za Uvuvi.

Kisha hawa Mabinti / Wanawake ambao mtawapanga Wajirahisi kwa Beach Boys (ambao napendekeza lazima Wawe ni Wajuzi wa Kuogelea hasa) mtawaambia wakishaingia tu kwenye Maji na kupelekwa Maji Marefu na kuanza Kuombwa Ngono au kutaka Kubakwa upesi sana watoe Ishara kwa wale Wavivu mtakaowapanga watakaokuwa Eneo Jirani na kwa Askari wengine ambao mtakuwa mmewapanga huku nchi Kavu.

Mkishawakamata hawa Wachache watataja Mtandao wao Wote na Kutajana (huku mkiruhusu na Sisi Raia tuwatje Adabu kidogo kwa Vipigo vya kishalubela) pale pale Baharini ili kutoa Signal kwa Wenzao wengine kuwa sasa Serikali kwa Kushirikiana na Raia Wema (akina GENTAMYCINE) mmeamua / tumeamua Kuwadhibjti.

Na baada ya hapo tu mnaondoka nao kwenda Polisi ili kuanza taratibu zingine za Kisheria ila naomba Adhabu ya Viboko ama 6 au 12 isikosekane na Kifungo kirefu

12. Na katika Vijiwe vyao vyote hao Beach Boys huko Baharini baada ya Kuwasajili Kisheria kama nilivyoshauri hapo mwanzoni pia himizeni / lazimisheni kila Kijiwe kiwe na Utambulisho wa Namba na Jina Kubwa lililoandikwa

13. Ikiwapendeza himizeni / lazimisheni kila Binti / Mwanamke aendae Kuogelea Baharini aende na Pila / Tairi lake kutoka Kwao / Kwake kwani Wengi Wao wakati Mwingine hujikuta wanajngia Majaribuni hadi Kulalwa kwa Kukosa tu Vifaa hivi.

14. Tangazeni kabisa Binti / Mwanamke ambaye kwa Upumbavu na Uwoga wake bila kusahau Tamaa zake za Mwili akikubaliana na huu Uhuni wa hawa Wahuni Beach Boys na likampata la Kumpata asije Kulaumu Mtu au Serikali

15. Mwisho tengezeni Vipindi Maalum katika Redio na Television vya Kutoa Elimu na Kuonya juu ya Ukatii huu mkubwa huku mkihimiza kila Beach Goer (Mpenda kwenda Kutembea Baharini) awe ni Mlinzi wa Mwenzake pasipo kujali ni Ndugu yako au si Ndugu yako

Ni haya tu Mheshimiwa Waziri Dkt. Gwajima D nakuomba yafanyie Kazi yote na GENTAMYCINE nakuhakikishia hapa hapa JamiiForums kuwa Tatizo hili utalimaliza na Kuokoa wengi.

Nimekuheshimu sana kwakuwa navutiwa na Utendaji wako mzuri wa Ushirikishaji wa Wadau na nakuahidi kukupa Ushirikiano zaidi kwa Mambo / Masuala mengine ya Kijamii ukihitaji kwani 97% ya Maisha yangu ya kila Siku ni kuwa na Jamii na kuwa na Uwezo mkubwa wa Kuchunguza Jambo, Kulifuatilia, Kulijua, Kulirekodi katika Ubongo wangu, Kulikabili Kifikra na Kimatendo na kutoa Suluhisho la Dharula, la Kati na la Kudumu.

Mheshimiwa Waziri Dkt. Gwajima D tafadhali kama utakuwa na Zawadi yoyote ile Kwangu GENTAMYCINE (itakayokupendeza) kwa hiki nilichokuandikia hapa basi utakitangaza hapa hapa JamiiForums kisha utaipeleka katika Ofisi za JamiiForums Kawe Avocado na utampa JamiiForums Founder Mtani wangu wa Kihaya na Kaka Maxence Melo na yeye atajua wapi atanipata na Kuiwasilisha Kwangu kwa Niaba yako.

Na nikutoe Hofu Dada (Mheshimiwa Waziri Dkt. Gwajima D) hata kama hutonipa Zawadi yoyote ile bado nakuhakikishia nitaendelea kukupa Ushirikiano wangu mkubwa bila Kinyongo na Usununu.

Kila la Kheri Mheshimiwa

Tupo pamoja.

Akhsante.

Wako GENTAMYCINE Nahodha wa Kudumu wa wana JamiiForums wote duniani.

Mkuu umetoa ushauri makini! Nakuunga mkono!
 
Back
Top Bottom