Waziri Doto Biteko kapelekwa Nishati kuangushiwa jumba bovu

Ndio mjue kuwa tatizo sio mtu binafsi ni mfumo mzima.

Mnaanza kujihami mapema?!

Pambaneni!

Mlimkalia kooni Januari ,

Haya sasa wachawi mmepewa mwana mumlee [emoji3][emoji28]
Safi sana
 
Mbona makamba alianza kulaumiwa wiki hiyo hiyo alivyoingia ofisini? Mbona yeye hakupewa mwaka mmoja mabadiliko yaonekane
Ndio nasema lawama nyingine zimekaa kisiasa hazijengi chochote.

Nimekuwa kwenye Energy Sector, najua namna Magu alivyoharibu hii sector. Leo hii hatukupaswa kuwa watu wa kulalama kuhusu upatikanaji wa umeme.
 
Ni jumba bovu ndiyo maana
 
Mteuzi wake mwenyewe ni Jumba bovu sasa jumba lipi litamwangukia.
 
Kuna kitu hakija kaa sawa.
HAingii akilini kuwa mwenyekiti wa kijiji pia awe balozi wa nyumba kumi.

Naibu Waziri mkuu, mwenye mamlaka ya kukaimu uwaziri mkuu tena awe waziri wa kawaida.

Hivyo wakikemewa mawaziri naye yumo???
WIzara ikivurunda naye yumo??

Rais anawaza nini?
Mbona kama kuna kuaibishana?

.....huwezi kunielewa hadi umenielewa...
 
Mbona makamba alianza kulaumiwa wiki hiyo hiyo alivyoingia ofisini? Mbona yeye hakupewa mwaka mmoja mabadiliko yaonekane
Lakini kinachoshangaza wengi ni kwamba mbona katika kipindi cha mwendazake na Kalemani wake katikakatika ya umeme haikuwa hivi ??!
Tuseme ukweli tu !!
 
Acha uongo makamba kachukua wizara chini ya Mh Kalemani na umeme ulikuwa wa kumwaga kaingia yeye ndio kavurunda
Sio kweli, mgao ulianza rasmi june 2020, toka wakati ule tatizo la mgao limekuwa likiongezeka kila muda unavyoenda. Nakumbuka wakati wa kampeni ya uchaguzi wa 2020 kulikuwa na mgao wa kila mara.
 
Sasa si ndio anatakiwa kurekebisha au? Kwani nini maana ya kuwa Kiongozi? Sukuma gang mbona mna nongwa sana nyie?
 
Amelazimishwa? Hana akili? Kwa nini asikatae?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…