Waziri Godfrey Mwambe kama hauwezi kuthibitisha uongo wa Hayati Magufuli basi unapaswa kujiuzulu mara moja

Waziri Godfrey Mwambe kama hauwezi kuthibitisha uongo wa Hayati Magufuli basi unapaswa kujiuzulu mara moja

Fumadilu Kalimanzila

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2016
Posts
1,770
Reaction score
5,423
Inasikitisha sana!

Tuna viongozi wa ajabu sana Nchi hii ! CCM iko wapi?

Aliyelieleza Taifa kuhusu " madudu" ya mkataba wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo alikuwa ni Rais wa JMT, Amiri Jeshi Mkuu, Mkuu wa Nchi, Raia namba moja mwenye taarifa zote muhimu 24/7 kuhusu Nchi yake kuliko raia mwingine yeyote!

Hayati Rais Magufuli aliyasema hayo mchana kweupe tena bila kumung'unya maneno na makofi mengi akapigiwa !!!! Nadhani hata huyu Waziri Godfrey Mwambe alikuwa kwenye hadhira hiyo kama Boss wa TIC !! Clip zipo YouTube!

Sasa swali kwako Ndugu Waziri Mwambe, umesema hakukuwa na mkataba wowote uliosainiwa!! Je iliwezekanaje Rais wa Awamu ya NNE Mhe. Kikwete kuzindua mradi na kuweka jiwe la msingi katika mradi ambao ulikuwa hauna mkataba?

Clip za uzinduzi huo zipo YouTube na ilikuwa covered katika taarifa ya habari TBC.

Kama kweli Mhe.Kikwete alizindua mradi ambao haukuwa na mkataba bado basi Matatizo ya Nchi yetu ni makubwa kuliko tunavyoelezwa au tunavyofahamu!

Cha kusikitisha ni kuwa viongozi wote hawa wenye ndimi tofauti wanatokana na Chama Cha Mapinduzi!!

Bunge liko wapi?! Kwa nini wabunge msiombe taarifa rasmi kuhusu mradi wa Bagamoyo na sisi kama wananchi tuliowatuma Bungeni tujuwe KUNA NINI UJENZI WA BANDARI YA BAGAMOYO?

Kama kuna madudu wahusika wawajibike!! Kwa kweli wananchi mnatuchanganya sana!

Huyu anasema hili, yule anasema kile! CHAMA KIMOJA, SERIKALI MOJA , SCRIPT TOFAUTI.
 
Sasa swali kwako Ndugu Waziri Mwambe, umesema hakukuwa na mkataba wowote uliosainiwa!! Je iliwezekanaje Rais wa Awamu ya NNE Mhe. Kikwete kuzindua mradi na kuweka jiwe la msingi katika mradi ambao ulikuwa hauna mkataba !??!!!!
Hata kama hutaki huo ndo ukweli wenyewe ambao hata mimi nimeuleza hapa mara 100 kidogo...

HAPAKUWA NA MKATABA WOWOTE ULIOKUWA UMESAINIWA

Ambacho kilisainiwa ni Initial Agreement Framework, na baadae ikasainiwa MoU kwa kuhusisha Oman's State General Reserve Fund, ambao wangewekeza kwenye Bagamoyo Special Economic Zone.

Hiyo Framework Agreement ilitaja ni mambo gani Mwekezaji aliyata kwa upande wake, na uliwekwa muda wa serikali kupitia framework na kisha baada ya hapo wakutane na Mwekezaji kwenye meza moja ili kujadiliana ni kipi na kipi serikali wanakubaliana nacho na kipi hawakubaliani!!

Baada ya hiyo hatua, ndipo mkataba ungesainiwa!

Ni kutokana na hilo, ndo maana huwezi kusikia popote pale habari za kuvunja mkataba kwa sababu huwezi kuvunja mkataba ambao haupo! Utakachosikia ni kuendelea kwa majadiliano!

Kwavile muda wa JK unaenda ukingoni, Framework na kufanya majadiliano ya mwisho a hatimae kusainiwa mkataba kungefanyika na serikali ambayo angefuata!

Hilo suala la kuzindua mradi zilikuwa ni siasa za uchaguzi mkuu tu!

Hata SGR walizindua vile vile!! Kila mtu anafahamu jinsi ambavyo Lowassa aliwakalia kooni CCM!! Na ndo maana hata ukifuatilia, utakuta miradi yote hiyo "imezinduliwa" dakika za majeruhi... September 2015 to October 2015!!
 
Umehoji kwamba bunge liko wapi?? Hapo unataka kusemaje mkuu maana nchi hii inajulikana kwamba mhimili ulioenda chini sanaa ni mmoja tuu.
 
Tanzania kuna wananchi bana au misukule?!!kwani jpm aliposema mkataba una madudu, mbona hamkuutaka kuuona kama ni kweli alichokuwa akikisema?

Wakati nguvu nyingi zinatumika kuhakikisha kuwa hakuna mpinzani anarudi bungeni mlikuwa mnashangila tu , kuwa wanawachelewesha!!ikiwapendeza hata nchi nzima iuzwe tu!!!
 
Kuna sheria inayosema mikataba na siri?

Kama ndivyo hatuna haja yakuwa na vikao vya bunge.

Mradi mkubwa kama huo inakuwaje wabunge hawajui nahawakuupitia?

Hadi 2025 tutakuwa tunasikiliza hili bunge
 
Unasema wabunge waliotumwa na wananchi, una uhakika kule bungeni kuna wabunge waliotumwa na wananchi?

Robo tatu ya wabunge wote waliopo bungeni, hawakupita kwenye kura za maoni ndani ya CCM. Kwa hiyo hawakuteuliwa na wajumve wa CCM. Katika hao ambao hawakupitishwa na wajumbe, zaidi ya nusu walipitishwa eti bila kupingwa. Walioenda kwenye uchaguzi, kura za kutangazwa waligawiwa na wakurugenzi wa wilaya. Sasa wananchi waliwatuma hao maharamia wa uchaguzi bungeni kwa njia gani?

Tujue tu kuwa tupo chini ya laana. Tunatawaliwa na watu ambao hatukuwachagua. Wabunge ambao wanajua kuwa hawakuchaguliwa na wananchi, aliyewateua hayupo Duniani, hawawezi kuwa na ujasiri wa kumhoji yeyote maana wanajua hakuna wanayemwakilisha zaidinya matumbo yao na mfumo haramu uliowaweka.
 
Tanzania kuna wananchi bana au misukule?!!kwani jpm aliposema mkataba una madudu, mbona hamkuutaka kuuona kama ni kweli alichokuwa akikisema?wakati nguvu nyingi zinatumika kuhakikisha kuwa hakuna mpinzani anarudi bungeni mlikuwa mnashangila tu , kuwa wanawachelewesha!!ikiwapendeza hata nchi nzima iuzwe tu!!!
Mambo ya wapinzani kurudi bungeni yameingiaje hapa sisi tunaongelea mkataba sio wapinzani wenyewe wanapigania matumbo yao kurudi bungeni hao
 
Sio kwasababu Jiwe alisema basi yeye ndie mwenye haki ya kuwa sahihi na alisema ukweli.

Hata jiwe mwenyewe hajatuthibitishia kwa kutuonyesha huo mkataba bali alisema tu public kama ambavyo Wazir Mwambe nae amesema.

Jiwe alisema mengi tu ambayo si sahihi kama "yule Jamaa aliesingiziwa kuingiza Million 7 kila dakika"

Akasema uongo pia "serikali inaidai Acacia Trillion 450 ambapo tukilipwa kila mtanzania atapatiwa Noah".

Kwa hio kuwa Rais hakukupi uhalali wa kuwa msema ukweli na wengine wakawa wanasema uongo.

Wala kusema maneno p3kee ya " msema kweli ni mpenzi wa Mungu",pia nako hakukupi uhalali huo.

Unaweza kuwa Rais na ukasema uongo ili kukidhi matakwa yako ya kisiasa kama ambavyo tunaona Mara nyingi tu Marais wetu wakisema uongo.
 
Mambo ya wapinzani kurudi bungeni yameingiaje hapa sisi tunaongelea mkataba sio wapinzani wenyewe wanapigania matumbo yao kurudi bungeni hao
Hayo ni matokeo ya kuwa na bunge la ovyo la chama kimoja , unafikiria juzi General ulimwengu aliposema kuwa inakuwaje bunge lina kuwa mtetezi wa serikali tena , badala ya kuisimamia!!

Kwani kipindi cha jk wapinzani mbona walikuwa na hoja zenye mashiko na kiasi fulani serikali iliweza kufanya kazi!na ndio maana sasa hivi mwananchi anashindwa ashike lipi, kila mtu anasema lake!!

Nenda kwenye umeme, maji wasikie mawaziri , na watendaji kila mtu ana kauli yake!!hayo ni matokeo ya kuwa na bunge la chama kimoja!!
 
#Fumadilu Kalimanzila!

Umefumguka ukweli mtupu

Tatizo la nchi hii waongo ndio wanapewa kipaumbele!

Mwambe hata body language yake wakati akiongea na Press media alikuwa anaonyesha wazi kuongea maneno ya kutumwa.
 
Sio kwasababu Jiwe alisema basi yeye ndie mwenye haki ya kuwa sahihi na alisema ukweli.

Hata jiwe mwenyewe hajatuthibitishia kwa kutuonyesha huo mkataba bali alisema tu public kama ambavyo Wazir Mwambe nae amesema.
...
Wewe una chuki za kupelekwa kijiweni shauri ya cheti fake.

Mtoa hoja amemtaka Mwambe athibitishe huo uongo ili kuondoa ujinga kama huu wa kwako.
 
Mbona haliitaji akili kubwa kutambua kuwa hakukuwa na mpaka sasa hakuna mkataba wowote uliosainiwa wa ujenzi wa bandari.

Kilichopo ni mapendekezo ya mkataba ambayo jiwe aliyagomea na kuwataka wachina waje na terms na conditions nyingine.

Hivi inawezekanaje uuvunje mkataba mliosaini tayari kisha mwekezaje akuangalie tu asikuchukulie hatua yeyote?
 
Serikali ya CCM imewekeza kwenye uongo mpaka wakaamua kutunga sheria ya kuhalalisha uongo.
 
Kiukweli inashangaza mno!!

Kwani kulikuwa na sababu waziri kushangaa kuhusu habari za kusainiwa kwa huo mkataba? Kwani angesema kuwa Rais Magufuli alidanganywa kungekuwa na ajabu ipi? Kauli yake imeonyesha Nature ya viongozi tulionao!!

Wananchi mnawachanganya, mbaya zaidi wananchi wenyewe wamejaa u team... Yani wale waliokuwa hawampendi Magufuli hawajishugulishi hata kidogo juu ya habari hizo as long as zinaonyesha mabaya yake wataunga mkono bila kujali hoja iliyozungumzwa.

Wale wanaohoji na kushangaa wanaishia kuitwa sukuma gang!!

Goja tuendelee kuona movie!!
 
Kwani Mstaafu J. Kikwete si yupo hapo hapo jirani au Msasani ajitokeze aweke hili wazi na bunge liweke msimamo pamoja na wizara husika.

Kwa kuwa aliyeukataa hayupo na baadhi ya hotuba yake iliyopigiwa makofi ipo basi waikanushe kwa ushahidi na mkataba mpya uje mezani.

Bandari tunaitaka kwa vyovyote!.
 
Back
Top Bottom