Waziri Godfrey Mwambe kama hauwezi kuthibitisha uongo wa Hayati Magufuli basi unapaswa kujiuzulu mara moja

Mwambe ni kisemeo tu katumwa na Samia na snitch wa kwanza ni Samia, alikuwa makamu wa rais kavunja rekodi ya usaliti kwa kiwango kikubwa sana. Malipo yapo chini ya jua. Na 2025 ajiandae kulea wajukuu na haitatokea mwanamke kupata cheo cha umakamu wala urais mwisho wao utakuwa uwaziri mkuu tu ambao ianze kuwa ndoto yao.
 
Spika Ndugai na buñge lako kwa ujumla hebu lihurumieni taifa lenu, ni kweli hatuwezi kuwafanya lolote coz tayari nyie ni wabunge till 2025 lakini kumbukeni pia mnavizazi vyenu vya mbeleni wakati huo hamtakuwa hai. Hivi kweli mradi mkubwa kama huo buñge limekaa pembeni linausikilizia tu kama vile Sheria haiwaruhusu kuujadili?. Sasa kunahaja Gani ya kuwa na buñge ambalo mikataba yote yenye kuhusu matrilioni ya fedha kama SGR, Ununuzi wa ndege, bwawa la umeme, ujenzi wa bandari n.k haijadikiwi na buñge. Au kazi kubwa ni kupitisha bajeti ya waziri wa fedha isiyokuwa na uhalisia kwa kishindo na makofi mengi?
 
Kuna uwezekano mkubwa mkataba haukusainiwa.
JPM hakuvunja mkataba bali alikataa kutia saini kutokana na vipengele alivyo hisi vibaya kwa taifa.

Ungesainiwa na kusitishwa utekelezaji basi serikali ingeshitakiwa kwa kuvunja mktaba.
 
Umelielezea vizuri mkuu. Shida iko sasa kwa wasemaji official kuliweka sawa hili
Sidhani kama kuna tatizo akitokea waziri Mwambe au mtu yeyote akaliweka sawa kama ulivyofanya. Tatizo kubwa ni gossips nyingi kiasi kwamba tunabaki kwenye dilema, kulikuwa na mkataba/ hakukuwa na mkataba!
 
Vile MATAGA wanawahi kwenye uzi kuja kutetea legacy😁😁😁
Your browser is not able to display this video.
 
It was an intial agreement between the two parts. Baada ya makubaliano yale ndio usainishaji wa mkataba wenyewe ungefuata. Waziri yuko sahihi kuwa mkataba haukusainiwa na aliyeshindwa kutoa maelezo vizuri mbele ya wananchi ni Magufuli.
 
Kwani makamu wa Jpm,waziri mkuu wa Jpm, waziri wa fedha wa Jpm, na katibu mkuu wake wa wizara wanasemaje?
 
You're RIGHT lakini nadhani tatizo ilikuwa watu kuhofia kwenda kinyume na kauli ya Rais...

JPM sio mwanasheria... usikute alikuwa anadhani Agreement Framework au MoU ndo mkataba wenyewe!! Sasa kwavile Rais alishasema "Mkataba ni mbovu", basi ikawa taabu kwa wengine kusema vinginevyo!!

Lakini hata hao wengine, huenda nao hawafahamu tofauti kati ya Framework Agreement na Contract!

Lakini pia, kuna wengine waliamua kupotosha tu... ama kwa makusudi, au kwa kutofahamu! Au inawezekana labda wanafahamu Watanzania wanapenda kusikia lugha gani! Ukitaka uungwaji mkono, just say "Wezi tu wale" "Hiki na kile ni ufisadi mtupu"! Hapo utashangiliwa na kuonekana ni Mzalendo hata kama hutatoa ushahidi wowote, raia wataichukulia kauli hiyo ni UKWELI MTUPU KUTOKA KWA MZALENDO!

Mfano mzunri ni Marehemu Renatus Mkinga...

Huyu alikuwa Mjumbe wa TPA, lakini bila aibu kuna siku akasema "Wachina hawana pesa yoyote ya kujenga bandari, wamekuja kuiba tu. Mwenye pesa ni Oman"!

Watu walishangilia kweli kweli bila kujiuliza hivi inawezekana kweli Oman awe na pesa ya kujengea bandari ya kumzidi Mchina!!

Yaani wala sitaki kuamini kwamba uhusika wa Oman ulikuwa kwenye Bagamoyo Special Economic Zone... yaani Industrial Complex ambayo ilitarajiwa kujengwa ili "kulisha" bandari ambayo ingejengwa!!
 
Mtakoma nzi wa kijani nyie na bado!
 
Imefika mahali hapa nchini, huwezi kutofautisha baina ya mtu aliyesoma na yule ambaye hajasoma.
Kuna baadhi ya mambo watu wanayaunga mkono hadi unabaki mdomo wazi na unasikitika tu.
 
Katika watu ambao wasingeanza kutoa matamsha ya kumkebehi jpm ni mawaziri na wabunge wote wa ccm wa sasa maana bila jpm wasingetangazwa kuwa wabunge. Watu kama mwambe jpm aliwatoa jalalani kabisa.
 
Mwendazake alileta uthibitisho?
 
Mkataba upi? Wewe umewahi kuuona huo mkataba?
Mambo ya wapinzani kurudi bungeni yameingiaje hapa sisi tunaongelea mkataba sio wapinzani wenyewe wanapigania matumbo yao kurudi bungeni hao
 
Mwambe mtu mdogo kumlinganisha na aliyekuwa mkuu wa nchi, uwe unatumia akili kidogo.
 
Sasa nani angeingia bungeni kama li CHAMA lenu la kaskazini lilijifia siku makengeza alipobadilisha gia angani mwaka 2015 ?
 
It was an intial agreement between the two parts. Baada ya makubaliano yale ndio usainishaji wa mkataba wenyewe ungefuata. Waziri yuko sahihi kuwa mkataba haukusainiwa na aliyeshindwa kutoa maelezo vizuri mbele ya wananchi ni Magufuli.
Kweli kabisa kumbe mkataba ulikuwa bado haujasainiwa yale yalikuwa mapendekezo.
Nakumbuka Magufuli akisema tutaendelea kufanya majadiliano.
Na yule aliekuwa bosi wa Bandari alizungumzia mapungufu yaliyomo kwenye muswaada.
Magufuli alitafuta njia mbadala kwa kuzijengea bandari zote uwezo na kupuuza Bagamoyo project.

Na China ilivyogundua kuwa Magufuli hapendi kabisa mapendekezo ya mkataba, ndipo nao Wachina wakajiongeza kufanya lobbying kupitia watu mashuhuri mmojawapo ni Spika Ndugai alipoitembelea China.

Lakini asiyependa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo si Magufuli tu bali hata nchi jirani kama Kenya,Mozambique na hata South Africa,sababu ya maslahi kwa nchi zao.

Lakini kwa awamu ya uongozi wa SSH kuna uwezekano mkubwa Bandari ya Bagamoyo kujengwa baada ya kufikia makubaliano na wabia wa China.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…