Waziri Gwajima atangaza kumchukulia hatua za kisheria Masha Love na wanaochochea kuharibu maadili

Wapi umeona nayafurahia?
Mimi naishangaa serikali ilivyo na unafiki kusema ushoga ni kosa wakati wakosaji hawakamatwi wala hawashtakiwi. Na wakishtakiwa wanaachiwa huru. Huo unafiki ndio ninao uhoji hapa.
Kujifanya wana maadili sana lakini hawafato sheria walizo ziweka wao.

Binafsi sina tatizo na mashoga, naendana na sera za kimarekani kila mtu apewe haki yake. Mtu awe shoga au asiwe mimi naona sawa tu.(nashukuru wanangu hawawezi kuwa mashoga😀). Kila mtu alinde watoto wake kwa jinsi anavyoweza.
Nina Imani tarehe 17 Mei, 2024 mchana, wewe ni kati ya ambao hawakusikiliza kipindi cha bunge ambapo, hii hoja yako ilijibiwa na Mhe Waziri wa Mambo ya ndani na takwimu kutolewa. Hili ndiyo tatizo, hatufuatilii, halafu tunakuja na maswali. Rejea online maana ilikuwa live tafadhali
 
Sasa ndiyo unaongea vema. Shida za nchi yetu ni huu utaratibu wa watu kuomba Sheria itungwe, halafu wakati wa kutoa maoni hawaji na wito hutolewa online pia siku kadhaa, halafu sheria ikishatungwa na kusambazwa ikiwemo online humu, hawafuatilii. Ikianza kutekelezwa wanaanza kumlaumu mtekelezaji na kudhani amekuja na yake tu. Niwaambie ukweli, Hali hii huvunja mioyo watu wenu wengi wenye Nia ya kusimamia hayo mabadiliko. Hubaki wenye mioyo migumu tu na kama kawaida huwa ni wachache Sana. Hivi hasara hupata nani hapo?

Mfano hebu soma hicho kifungu cha 14. Je hapa nani wa kumshangaa mwenzake?

Haya, umesema vema, hata hao mashoga wanajiuza humo online na picha zao, kifungu Chao cha kwanza hicho hapo, mimi na wewe na wote tunatakiwa kuwa walalamikaji. Tutalalamikaje na Sheria hatuzijui na hatufuatilii Ili tutoe taarifa wenye Sheria husika wafanyie kazi? Sasa tunaanza kuinua Sheria husika, tayari anayeinua anashambuliwa.

Hivi huwa tunatakaje? 🇹🇿
Sidhani kama wananchi wana tatizo na hiyo sheria iliyotungwa bali wananchi wanashangaa kwanini sheria haifatwi.
Kama sisi wananchi tunaziona hizo pages miaka na miaka ina maana wahusika wakufatilia hizo sheria wao hawaoni?
Ni lazima wananchi walalamike ndo hatua zichukuliwe?

Tangu hiyo sheria itungwe ni shoga gani amewahi kuchukuliwa hatua? Au hakuna watu kama hao hapa nchini?

Vyombo husika vifanye kazi yake kuonyesha kwamba kweli hilo ni kosa na sheria inafuatwa. La sivyo haya mambo yanaendelea kuonekana ya kawaida tunajidai kupiga kelele maadili wakati hakuna lolote linalofanyika...ni maneno tu vitendo zero.

Ni mara ngapi videos za wanawake zimekuwa exposed kwa lengo la kuwadhalilisha, ingawa na wao walifanya kosa kuruhusu kupiga picha/video za hivyo lakini zimewekwa wazi bila idhini yao. Hakuna kesi hata moja iliyowahi kufunguliwa na mtu akahukumiwa.
Ile ya afande ya juzi wewe ni shahidi umeona wameachiwa huru. Mambo kama hayo yanakatisha tamaa.
 
hii vita inakua ngumu kwasababu ya demand and supply, unless watumie nguvu kubwa kwa operation endelevu. kuhusu mmomonyoko imegeuka fashion usipoenda nayo hii hii jamii yenyewe inakuona mshamba mshamba. huyu waziri kama kweli ana nia afanye kazi kwerikweri
Maoni yako mazuri kabisa. Ila sasa, pamoja na ugumu wake, Hali inakuwa mbaya zaidi iwapo hakuna wa kusema, na kukemea na kuwasogezea Sheria wahusika. Kuna vita aina mbalimbali siyo hii tu, kuna vita dhidi ya madawa ya kulevya, tumezaliwa tumeikuta na hata Leo watu wanapigana, kuna magonjwa mbalimbali tumeyakuta, watu wanapigana na hayajaisha, na mengine yamepungua. Mimi na wewe tusipoanza vita hii kumbe duniani tumekuja kufanya nini sasa? Kupunguza tatizo au kuliongezea?

Kila mmoja atafakari achukue hatua anazoona zinafaa kati ya kupunguza au kuongeza. Tutalipwa na Mungu kwa wakati wake
 
Wapi umeona nayafurahia?
Mimi naishangaa serikali ilivyo na unafiki kusema ushoga ni kosa wakati wakosaji hawakamatwi wala hawashtakiwi. Na wakishtakiwa wanaachiwa huru. Huo unafiki ndio ninao uhoji hapa.
Huwez kamata shoga, shoga infact ni victim, aidha alipenda au alilazimishwa, kitendo cha kuwa shoga wewe tayar ni straight and first victim wa ushoga. So umkamate umfanye nini.
Ndio maana ni sahihi kupambana na ushoga kwa kuweka sheria inabana watu wanaotengeneza mazingira ya kuongeza na kusababisha mashoga kama huyo dada anavyofanya.
Au walawiti pindi wanapodakwa hawa ni sahihi kuchuliwa sheria na shria zinachukuliwa kama wale jamaa wa 4 juzi
Kujifanya wana maadili sana lakini hawafato sheria walizo ziweka wao.
Kwa namna yoyote iwayo, suala la maadili sio kujifanya. Watieni moyo watu wanaoshughulika na suala hili, ni kwa nia njema tu, mengine kama yapo bas ni mapungufu ya kibinadamu tu but dont attack watu walio kwenye wajibu wa kushughulika na hiz kitu.
Binafsi sina tatizo na mashoga, naendana na sera za kimarekani kila mtu apewe haki yake.
ndio maana nikasema wewe ni mdau wa ushoga. Wengine tunaposikia tu hizi habar tuna tetemeka, haiwezekan wewe ukawa unacheka cheka halaf ukasema hauna tatizo na ushoga.
Mtu awe shoga au asiwe mimi naona sawa tu.(nashukuru wanangu hawawezi kuwa mashoga😀).
kwakua huna shida na ushoga, hata akiwa shoga hutakua na shida na hilo suala ndio maana halikuumizi kichwa, si ni haki yake itakua kupigwa pipe za mnduku
Kila mtu alinde watoto wake kwa jinsi anavyoweza.
Tunapozima moto nyumba ya pil jirani yako ikiwa inateketea sio kwasababu unampemda sana, HAPANA. ni kwasababu moto unaweza hamia na kwako ukaleta majanga. Hatuwez lea watoto wetu vyema na kuwekeza muda kuwafunza halaf wakitoka nje wanakutana na jamiii iliyooza unafikiri chance za wao kupona ni kubwa??
WAziri Dkt. Gwajima D shikilia hapo hapo
 
Sidhani kama wananchi wana tatizo na hiyo sheria iliyotungwa bali wananchi wanashangaa kwanini sheria haifatwi.
Kama sisi wananchi tunaziona hizo pages miaka na miaka ina maana wahusika wakufatilia hizo sheria wao hawaoni?
Ni lazima wananchi walalamike ndo hatua zichukuliwe?

Tangu hiyo sheria itungwe ni shoga gani amewahi kuchukuliwa hatua? Au hakuna watu kama hao hapa nchini?

Vyombo husika vifanye kazi yake kuonyesha kwamba kweli hilo ni kosa na sheria inafuatwa. La sivyo haya mambo yanaendelea kuonekana ya kawaida tunajidai kupiga kelele maadili wakati hakuna lolote linalofanyika...ni maneno tu vitendo zero.

Ni mara ngapi videos za wanawake zimekuwa exposed kwa lengo la kuwadhalilisha, ingawa na wao walifanya kosa kuruhusu kupiga picha/video za hivyo lakini zimewekwa wazi bila idhini yao. Hakuna kesi hata moja iliyowahi kufunguliwa na mtu akahukumiwa.
Ile ya afande ya juzi wewe ni shahidi umeona wameachiwa huru. Mambo kama hayo yanakatisha tamaa.
Kuwa shogani amewahi kuchukuliwa hatua, ni jibu lililotolewa tarehe 17 Mei, 2024 bungeni, rejea online, ilikuwa mchana tena kuelekea jioni, nilipokuwa nahitimisha hotuba yangu ya bajeti, sina hakika kama ulifuatilia
 
Huwez kamata shoga, shoga infact ni victim, aidha alipenda au alilazimishwa, kitendo cha kuwa shoga wewe tayar ni straight and first victim wa ushoga. So umkamate umfanye nini.
Ndio maana ni sahihi kupambana na ushoga kwa kuweka sheria inabana watu wanaotengeneza mazingira ya kuongeza na kusababisha mashoga kama huyo dada anavyofanya.
Au walawiti pindi wanapodakwa hawa ni sahihi kuchuliwa sheria na shria zinachukuliwa kama wale jamaa wa 4 juzi

Kwa namna yoyote iwayo, suala la maadili sio kujifanya. Watieni moyo watu wanaoshughulika na suala hili, ni kwa nia njema tu, mengine kama yapo bas ni mapungufu ya kibinadamu tu but dont attack watu walio kwenye wajibu wa kushughulika na hiz kitu.

ndio maana nikasema wewe ni mdau wa ushoga. Wengine tunaposikia tu hizi habar tuna tetemeka, haiwezekan wewe ukawa unacheka cheka halaf ukasema hauna tatizo na ushoga.

kwakua huna shida na ushoga, hata akiwa shoga hutakua na shida na hilo suala ndio maana halikuumizi kichwa, si ni haki yake itakua kupigwa pipe za mnduku

Tunapozima moto nyumba ya pil jirani yako ikiwa inateketea sio kwasababu unampemda sana, HAPANA. ni kwasababu moto unaweza hamia na kwako ukaleta majanga. Hatuwez lea watoto wetu vyema na kuwekeza muda kuwafunza halaf wakitoka nje wanakutana na jamiii iliyooza unafikiri chance za wao kupona ni kubwa??
WAziri Dkt. Gwajima D shikilia hapo hapo
Yaani siachi ndugu yangu, wasubiri tu hii kazi sitaishi nayo milele, nikitoka Mimi atakuja mwingine ataendeleza. Ila kwa wakati wangu huu nitafanya ninachodhani kuwa ni sahihi kwa mujibu wa majukumu, miongozo mbalimbali ikiwemo hizo Sheria.

Kama wao wako salama, wako watoto na wazazi hawako salama. Sauti yangu hii ikitokea, inaenda mbali na inaalika wapinzani kama Hawa wakidhani wanazima sauti kumbe ndiyo wanaipaisha. Na kwa kufanya hivyo, mtoto mmoja huokolewa na hii ni heri kuliko sifuri kabisa.
 
Ndio kazi yake inayomuweka mjini, yaan wabongo wanafki jaman, sasa umelazimishwa kum'follow huyo masha love? Mmelazimishwa kuwafuata hao watoto wa 2000,? Yaan sijapenda kabisaa, kwa hiyo ndio mama ameanza kufunza adabu watu wote ataweza? Kwa taarifa yenu bora hao wanaojinengua kuliko hao wanaojifichaficha. Muacheni masha love afanye kazi yake inayomuingizia kipato ukiona unakereka tuliza mshono unfollow,. Mashalove hana shida yoyote mbona hao waimbaji wa nyimbo za bongo fleva mmewaona wanavyovaa? Jaman hebu angalieni na upande wa wasanii, Dunia imekuwa tusipomuangalia mashalove tutawasha youtube tutawaangalia wa mataifa mengine. Acheni wivu jaman
Fanya hivi, pendekeza sasa ile sheria iliyopo ifutwe. Vinginevyo, hapa unaongezea notice tu rafiki mpendwa. Halafu Sasa hizi kiki mnazisemaga, hivi huwa faida yake nini hasa? Wewe si uache tu kuzitoa hizi kiki😃

Maana kwa kuchangia tu mada unakuwa umesha kick hiyo ajenda, watu wanakuja kusoma na kuona yaliyomo
 
Dada yangu endelea na kazi zako hapa tuna vijana wa hovyo sana utajishusha hadhi kubishana nao,
Hakika, ujue umama ni mzigo Sana, yaani unakuwa unatamani na huyu naye aijue kweli.

Halafu, mimi huwa naona, kadri mtu anavyojitahidi kumshusha mwingine hadhi, ndivyo na hadhi yenyewe hupanda. Maana kimpandishacho mtu juu ni ile kweli iliyo ndani yake kuliko uongo ulio nje yake.
 
Huyu dada na mauchafu yake yote anaofanya bado wenye mabiashara wanampa ubalozi awatangazie bidhaa zao
Na ile media yenu pendwa ya wsf ndy wanamlea sana
Ndy role model wa vijana wengi sahv watu dizain hii

Ova
 
Huyo masha wanaandaga sex party humo ndani ni mwendo wa
Magroup sex gangbang kwa sana
Watoto wana 713 humooo

Ova
Halafu mimba za utotoni zikitokea, magonjwa na watoto wa mtaani na walevi wa madawa mabaya, tunakuja kuulizana kuna mikakati gani. Kweli heri waliofunuliwa katika kweli na haki.....
 
Huyu dada na mauchafu yake yote anaofanya bado wenye mabiashara wanampa ubalozi awatangazie bidhaa zao
Na ile media yenu pendwa ya wsf ndy wanamlea sana
Ndy role model wa vijana wengi sahv watu dizain hii

Ova
Dunia imepotoka na hekima imepotea na baadhi ya watu wazima waliopewa fursa ya kuishi duniani ndiyo wanaoiharibu Ili watoto waangamie wakidhani nao mwisho wao utakuwa wa baraka na heri. Heri aliyefunuliwa. Miaka 70 tu ya kuishi duniani vurugu hizi, je ingekuwa mia mbili.... Mungu shujaa
 
Nina Imani tarehe 17 Mei, 2024 mchana, wewe ni kati ya ambao hawakusikiliza kipindi cha bunge ambapo, hii hoja yako ilijibiwa na Mhe Waziri wa Mambo ya ndani na takwimu kutolewa. Hili ndiyo tatizo, hatufuatilii, halafu tunakuja na maswali. Rejea online maana ilikuwa live tafadhali
Sasa mheshimiwa...wananchi wote waache shughuli zao na kila kila wafanyacho wakae chini wasikilize bunge? Inawezekana vipi? Je kama nilikuwa mgonjwa hospitali hiyo siku hilo bunge ningeangaliaje?

Ulipaswa tu kunijulisha kwamba ilishaongelewa na ipo online nikatazame.
Kiufupi wananchi tunataka kuona sheria zikifatwa na sio watu kupewa onyo na kuomba msamaha haisaidii chochote yatajirudia tu.
 
Huwez kamata shoga, shoga infact ni victim, aidha alipenda au alilazimishwa, kitendo cha kuwa shoga wewe tayar ni straight and first victim wa ushoga. So umkamate umfanye nini.
Ndio maana ni sahihi kupambana na ushoga kwa kuweka sheria inabana watu wanaotengeneza mazingira ya kuongeza na kusababisha mashoga kama huyo dada anavyofanya.
Au walawiti pindi wanapodakwa hawa ni sahihi kuchuliwa sheria na shria zinachukuliwa kama wale jamaa wa 4 juzi

Kwa namna yoyote iwayo, suala la maadili sio kujifanya. Watieni moyo watu wanaoshughulika na suala hili, ni kwa nia njema tu, mengine kama yapo bas ni mapungufu ya kibinadamu tu but dont attack watu walio kwenye wajibu wa kushughulika na hiz kitu.

ndio maana nikasema wewe ni mdau wa ushoga. Wengine tunaposikia tu hizi habar tuna tetemeka, haiwezekan wewe ukawa unacheka cheka halaf ukasema hauna tatizo na ushoga.

kwakua huna shida na ushoga, hata akiwa shoga hutakua na shida na hilo suala ndio maana halikuumizi kichwa, si ni haki yake itakua kupigwa pipe za mnduku

Tunapozima moto nyumba ya pil jirani yako ikiwa inateketea sio kwasababu unampemda sana, HAPANA. ni kwasababu moto unaweza hamia na kwako ukaleta majanga. Hatuwez lea watoto wetu vyema na kuwekeza muda kuwafunza halaf wakitoka nje wanakutana na jamiii iliyooza unafikiri chance za wao kupona ni kubwa??
WAziri Dkt. Gwajima D shikilia hapo hapo
Niite vyote utakavyo. Kwa mtazamo wako its okay.
Kumbe wote tunakubaliana kwamba shoga ni victim (hapo tunafanana mawazo, nahisi na wewe ni mdau pia.

Kama ni victim basi hakuna haja ya kuweka sheria za kuwapeleka mahakamani. Sheria ibadilishwe wapewe msaada wa kisaikolojia zaidi.
 
Sasa mheshimiwa...wananchi wote waache shughuli zao na kila kila wafanyacho wakae chini wasikilize bunge? Inawezekana vipi? Je kama nilikuwa mgonjwa hospitali hiyo siku hilo bunge ningeangaliaje?

Ulipaswa tu kunijulisha kwamba ilishaongelewa na ipo online nikatazame.
Kiufupi wananchi tunataka kuona sheria zikifatwa na sio watu kupewa onyo na kuomba msamaha haisaidii chochote yatajirudia tu.
Kila bunge lakini hoja hii inatokea na inaelezwa. Aidha, hata mimi huwa nakuwa sipo kwenye baadhi ya mambo, baadae huwa narudi online nasoma na kusikiliza. Ilikuwa kukushauri tu kuwa, tuwe na mwamko wa kusikiliza na kufuatilia, kama siyo Leo hata kesho kutwa. Ahsante Sana
 
Dunia imepotoka na hekima imepotea na baadhi ya watu wazima waliopewa fursa ya kuishi duniani ndiyo wanaoiharibu Ili watoto waangamie wakidhani nao mwisho wao utakuwa wa baraka na heri. Heri aliyefunuliwa. Miaka 70 tu ya kuishi duniani vurugu hizi, je ingekuwa mia mbili.... Mungu shujaa
Ngono sahv tz imeaminishwa
Kama sehemu ya kuingiza kipato
Kukubwa kwa watoto wa kike
Si mnaona huko kwenye mitandao wadada wanavyoshindana kutingisha makalio yao wengine wanacheza wanakalia mpaka chupa...
Haya mamiziki na media zinawalisha sana watu ujngujng

Iwapo hawataki kusikia sauti ya mabadiliko, mwisho wa siku watavuna katika uharibifu wao wala hauchelewi. Sisi tuendelee kuelimisha na kuchukua hatua ipasavyo
 
Back
Top Bottom