Waziri Gwajima atangaza kumchukulia hatua za kisheria Masha Love na wanaochochea kuharibu maadili

Waziri Gwajima atangaza kumchukulia hatua za kisheria Masha Love na wanaochochea kuharibu maadili

Shikilia hapo hapo mama angu. Hawa wapuuzi wanataka tusiwe na taifa baada ya miaka michache
Yaani maadam Sheria zipo, watazijua kwa kuwa tunaelimisha na wataamua sasa kuzifuata au kutofuata, maana hata wao maamuzi wanayo. Mimi ni mwelimisha jamii tu na mfikisha taarifa mahali sahihi Ili jamii ilindwe na hasa watoto na Makundi Maalumu maana wana haki ya kulindwa hata kama wengine wanaona wao hawahitaji kulindwa. Jamii ni Pana sana siyo wao tu hao ambao wanaona hawana uhitaji huo. Wavumilie maana ni ndani ya utaratibu tu hatuko nje.
 
Mshulikieni huyo lakini

Ova
 
Mkuu ukimalizana na Masha Love mtafute na Zuchu mwambie zile tabia zake anazozifanyaga kila anapokua jukwaani apunguze au aache maana anatuharibia watoto huku mikoani
Mbona tumeanza na wengi tu, mbona watu wanajisahaulisha. Je hatukuanza na wale wavaa majoka mwilini na wakaanza promo eti wakilala nayo wanapata hela? Tulikemea. Je hatukukemea kuhusu babu wa TikTok? Je hatukukemea kuhusu mambo ya uongo uongo mengine mengi tu? Vipi hili liwe keleleeee nyiiiingiiii ...

Watuache tufanye kazi za nchi, hakuna ubaguzi ni Kila mmoja na muda wake ukifika anaibuliwa anatengenezwa kuwa mwema.

Hakuna lingine, tushirikiane
 
Komaa nao. Hii nchi ina wajinga wengi sana. Na mbaya zaid hawajui wanayofanya wao pia yatawaathiri pakubwa kwa namna moja au nyingine
Hawajui kabisa kuwa huu ujana na kujipotezea njia ya haki fainali uzeeni. Wanataka Kila mmoja aje akumbukwe kwa kutoisadia jamii? Mimi simo kati ya hao, nitatimiza wajibu kadri niwezavyo
 
Mwizi akiiba akikamatwa na mali ya wizi anahukumiwa kifungo. Kwanini asiambiwe arudishe alichoiba halafu akaachiwa huru?
Haya mambo hayataisha bila kuonyesha mfano.
Halafu kipengele cha ushoga umekwepa kukijibu maana unajua kabisa serikali haipo serious kutokomeza ushoga zaidi ya kuongea tu.🤣🤣
Usijisahaulishe, aliyepambana na yule mtuhumiwa wa Ramada hoteli alikuwa nani? Kama siyo mimi. Ulinipongeza?
 
Hawajui kabisa kuwa huu ujana na kujipotezea njia ya haki fainali uzeeni. Wanataka Kila mmoja aje akumbukwe kwa kutoisadia jamii? Mimi simo kati ya hao, nitatimiza wajibu kadri niwezavyo
Hivi na hili ambalo niliuliza hapa chini, nalo vipi.. Sababu binafsi hilo ndio bomu kubwa kuliko na mwanzo wake ni huu wa sasa, ifike wakati tuwe proactive na sio reactive....

Hivi na hili ambalo niliuliza hapa chini, nalo vipi.. Sababu binafsi hilo ndio bomu kubwa kuliko na mwanzo wake ni huu wa sasa, ifike wakati tuwe proactive na sio reactive....

Salaam. Bahati mbaya sikuona mapema, kuna mijadala mingine huwa inanipita. Ngoja nitasoma, ila kwa ufupi, tumeshakamilisha mapitio ya sera ya Wazee mtasikia siku si nyingi ikitangazwa. Aidha, kwenye vision 2050 mtaona pia future ya kundi hili. Nakushukuru kwa uliyoandika, tutasoma tutachukua ya kuchukua kwa ajili ya kujumuisha kwenye mwelekeo wa kundi hili.
 
Ilienda mahakamani baadae Dpp akaifuta hapo waziri angefanya nini? Let us be fair
Nashangaa. Inashangaza Sana kuona mtu wa ulimwengu huu wa Leo tena wa kidigitali anakuwa hafahamu kuhusu majukumu ya wizara na tofauti yake na mahakama. Je wasio kidigitali huko, bado tunasafari ndefu Sana Afrika yetu
 
Mimi siwezi kuwa mchumia tumbo. Halafu wewe huna uwezo wa kuadress kiongozi. Kwa sababu nimeona uwezo wako wa kufikiri ni mdogo sana
Na sijui kwa nini anakuita hivyo wakati umemwelimisha vema kabisa. Anyway, muache tu. Art ya mawasiliano humu huwa Iko katika mazingira kwamba, ukosee Ili mtu akate kipande akaanze Uzi mpya wa kupotosha tena. Hivyo, muache tu, moyoni kaelewa.
 
Salaam. Bahati mbaya sikuona mapema, kuna mijadala mingine huwa inanipita. Ngoja nitasoma, ila kwa ufupi, tumeshakamilisha mapitio ya sera ya Wazee mtasikia siku si nyingi ikitangazwa. Aidha, kwenye vision 2050 mtaona pia future ya kundi hili. Nakushukuru kwa uliyoandika, tutasoma tutachukua ya kuchukua kwa ajili ya kujumuisha kwenye mwelekeo wa kundi hili.
Asante kwa jibu ila binafsi nadhani hili suala wala sio la kwako pekee bali ni la Wizara zote na nchi yote kwa ujumla mwisho wa siku kijana wa leo akipata ujira na kuweza hata kujiwekea akiba kama pensheni hio kesho ikifika wala hatutahitaji kumpa pesa au kumtunza, sababu kile alichokichuma leo na kingine kuwekewa kitamtunza....

Sababu sidhani kama kutoa charity au kuwapa watu pesa na vijimisaada ni sustainable.... Kinachoendelea sasa tunashindwa kutumia nguvu kazi ya vijana (ujanani) ili uzeeni tuweze tena kuwalea hawa watu ambao by then watakuwa mzigo na aibu kwa nchi

What am trying to say kumuangalia mzee wa kesho ni kuhakikisha kijana wa leo anapata ujira wa kutosha...
 
Usijisahaulishe, aliyepambana na yule mtuhumiwa wa Ramada hoteli alikuwa nani? Kama siyo mimi. Ulinipongeza?
Siikumbuki hiyo ya Ramada mheshimiwa ngoja nifatilie. Hongera kwa hilo...
Basi tunaomba na mashoga wanaojionyesha waziwazi mitandaoni wapewe onyo pages zao zifungwe. Kama wanafanya hayo mambo wafanye sirini na sio waziwazi imeanza kuonekana ni kawaida.
 
Cheap popularity sasa Mimi inipeleke wapi kwa mfano? Yaani inisadie nini hasa wewe unavyodhani. Si usinipe tu hiyo popularity yaishe😀

Mimi nasimamia Yale ambayo nyie watanzania mmeyawekea Sheria ambazo zinatakiwa kusimamiwa kwa ajili ya kujenga maadili na kuwalinda watoto wenu. Ni hilo tu. Sheria ya mtandao kifungu cha 14 kasome Kiko online. Hii habari ya kuuliza serikali ina mkakati gani na mpango gani na Sheria ziko wapi, muwe mnakumbuka kuwa vyote vipi, na tukianza kusimamia tupeane ushirikiano rafiki.
Mh Wazir nakuomba uachane na huyo binti ujue Huwa anatusaidia sana sisi vijana mkimfunga wafuasi wake watageuka kuwa wabakaji sasa utakuwa umeruka na kukanyaga nini?
 
Kwan wewe mbona unayafurahia sana haya mambo wewe ndio mdau pia au??
Wapi umeona nayafurahia?
Mimi naishangaa serikali ilivyo na unafiki kusema ushoga ni kosa wakati wakosaji hawakamatwi wala hawashtakiwi. Na wakishtakiwa wanaachiwa huru. Huo unafiki ndio ninao uhoji hapa.
Kujifanya wana maadili sana lakini hawafato sheria walizo ziweka wao.

Binafsi sina tatizo na mashoga, naendana na sera za kimarekani kila mtu apewe haki yake. Mtu awe shoga au asiwe mimi naona sawa tu.(nashukuru wanangu hawawezi kuwa mashoga😀). Kila mtu alinde watoto wake kwa jinsi anavyoweza.
 
Siikumbuki hiyo ya Ramada mheshimiwa ngoja nifatilie. Hongera kwa hilo...
Basi tunaomba na mashoga wanaojionyesha waziwazi mitandaoni wapewe onyo pages zao zifungwe. Kama wanafanya hayo mambo wafanye sirini na sio waziwazi imeanza kuonekana ni kawaida.
Sasa ndiyo unaongea vema. Shida za nchi yetu ni huu utaratibu wa watu kuomba Sheria itungwe, halafu wakati wa kutoa maoni hawaji na wito hutolewa online pia siku kadhaa, halafu sheria ikishatungwa na kusambazwa ikiwemo online humu, hawafuatilii. Ikianza kutekelezwa wanaanza kumlaumu mtekelezaji na kudhani amekuja na yake tu. Niwaambie ukweli, Hali hii huvunja mioyo watu wenu wengi wenye Nia ya kusimamia hayo mabadiliko. Hubaki wenye mioyo migumu tu na kama kawaida huwa ni wachache Sana. Hivi hasara hupata nani hapo?

Mfano hebu soma hicho kifungu cha 14. Je hapa nani wa kumshangaa mwenzake?

Haya, umesema vema, hata hao mashoga wanajiuza humo online na picha zao, kifungu Chao cha kwanza hicho hapo, mimi na wewe na wote tunatakiwa kuwa walalamikaji. Tutalalamikaje na Sheria hatuzijui na hatufuatilii Ili tutoe taarifa wenye Sheria husika wafanyie kazi? Sasa tunaanza kuinua Sheria husika, tayari anayeinua anashambuliwa.

Hivi huwa tunatakaje? 🇹🇿
 
Attachments

  • Screenshot_2024-10-31-19-19-38-00_6012fa4d4ddec268fc5c7112cbb265e7.jpg
    Screenshot_2024-10-31-19-19-38-00_6012fa4d4ddec268fc5c7112cbb265e7.jpg
    183.5 KB · Views: 3
Back
Top Bottom