Waziri Gwajima atangaza kumchukulia hatua za kisheria Masha Love na wanaochochea kuharibu maadili

Hapa ndio wakati sahihi somo la uraia litiliwe mkazo ili kuondoa mikanganyiko kama hii
Nakubaliana na wewe. Kwani tunapigana mishale tu hata hatusogei kisa wengine hata hawajui siyo muundo wa serikali, siyo Sheria na siyo majukumu ya wizara na miundo mingine ya nchi.

Yaani unakuta yule anayejitoa afanyie kazi mambo sugu yaliyoshamiri kinyume na sheria ndiye anayeshambuliwa kisa tu watu baadhi walizoea tofauti wakadhani mazoea ndiyo kawaida. Ukiacha kufanya wengine wakuhoji tena, usipokuwa na msimamo uyumbe yumbe.

Kumbe hapa ni elimu ya uraia... Ngoja nitafute wadau waje watoe elimu watu wajue, vinginevyo Sheria hizi tunazitaka Sana ila kutakuwa hakuna utekelezaji, na miundo hii tutaunda na bila majukumu kufahamika itakuwa hakuna ushirikiano, ukweli usemwe Ili twende sawa pamoja ndugu katika 🇹🇿

Ahsante Sana
 
Shikamoo mama
 
Nonsense,cheap popularity,Dkt. Gwajima D una mambo mengi ya kufanya na watanzania tuna shida nyingi sana kuliko huu upuuzi ,mfatilie pia yule mkuu wa mkoa aliye Binti wa chuo kikuu sauti ,ukimalizana na Nawanda

Ukifanya haya nitajua uko siriazi na kazi yako
Bila kumsahau Afande aliyeamuru Binti wa Yombo Dovya abakwe. Fuatilia hao kwanza ambao wengi tunashanga mbinu zenu za kupindisha sheria.. Mko double standard sana Mungu anawaona!!!
 
Ni kweli kabisa mkuu,nimekumbushia hoja hii Dkt. Gwajima D kaniletea chawa wake wote na yeye mwenyewe kunishambulia vibaya sana kama vile siruhisiwi kutoa hoja humu jukwaani.
 
Katika jambo ambalo sina ni hilo Sasa. Mimi hapa natosha kujibu hoja zote na kuelimisha hadi wote muelewe.

Wakija waliokuja hao ni kama wewe tu ulivyokuja kivyako, na hutuwezi kusema eti wewe unamtumkia fulani .... Badilikeni na mjiamini
 
Cheap popularity sasa Mimi inipeleke wapi kwa mfano? Yaani inisadie nini hasa wewe unavyodhani. Si usinipe tu hiyo popularity yaishe😀

Mimi nasimamia Yale ambayo nyie watanzania mmeyawekea Sheria ambazo zinatakiwa kusimamiwa kwa ajili ya kujenga maadili na kuwalinda watoto wenu. Ni hilo tu. Sheria ya mtandao kifungu cha 14 kasome Kiko online. Hii habari ya kuuliza serikali ina mkakati gani na mpango gani na Sheria ziko wapi, muwe mnakumbuka kuwa vyote vipi, na tukianza kusimamia tupeane ushirikiano rafiki.
Shikilia hapo hapo mama angu. Hawa wapuuzi wanataka tusiwe na taifa baada ya miaka michache
 
Nakubaliana na wewe. Kwani tunapigana mishale tu hata hatusogei kisa wengine hata hawajui siyo muundo wa serikali, siyo Sheria na siyo majukumu ya wizara na miundo mingine ya nchi.

Yaani unakuta yule anayejitoa afanyie kazi mambo sugu yaliyoshamiri kinyume na sheria ndiye anayeshambuliwa kisa tu watu baadhi walizoea tofauti wakadhani mazoea ndiyo kawaida. Ukiacha kufanya wengine wakuhoji tena, usipokuwa na msimamo uyumbe yumbe.

Kumbe hapa ni elimu ya uraia... Ngoja nitafute wadau waje watoe elimu watu wajue, vinginevyo Sheria hizi tunazitaka Sana ila kutakuwa hakuna utekelezaji, na miundo hii tutaunda na bila majukumu kufahamika itakuwa hakuna ushirikiano, ukweli usemwe Ili twende sawa pamoja ndugu katika 🇹🇿

Ahsante Sana
Chapa kazi mama hata kwenye sherehe wavulugaji hawakosekani
 
Mashalove hatapewa adhabu yoyote zaidi ya kupewa onyo na kuambiwa aombe radhi.
Mbona ameshafuta na mambo yote huko online ambayo ameshajua yalikuwa hayafai. Unajua watu wengi hawajui lipi ni kosa, na Sheria ni ipi. Pale unapomwambia hili ni kosa, akajua akajuta akaondoa, una Sababu gani kwa mfano ya kutomkanya? Mabadiliko yanahitaji hatua nyingi Sana na mojawapo muhimu, ni mtu kutambua na kujutia kosa lake. Alikuwepo babu wa TikTok, alijua na akajutia na akabadilika.

Mnataka kubadilika au kubadilisha jamii iwe vita ya mtu na mtu binafsi na siyo ya JMT 🇹🇿, hapana. Anayeshupaza shingo dhidi ya sheria ndiyo huyo huenda hatua ya pili......

Tushirikiane, wanaoharibika ni watoto na wajukuu zenu JMT 🇹🇿 siyo wangu peke yangu
 
Mwizi akiiba akikamatwa na mali ya wizi anahukumiwa kifungo. Kwanini asiambiwe arudishe alichoiba halafu akaachiwa huru?
Haya mambo hayataisha bila kuonyesha mfano.
Halafu kipengele cha ushoga umekwepa kukijibu maana unajua kabisa serikali haipo serious kutokomeza ushoga zaidi ya kuongea tu.🤣🤣
 
Kwan wewe mbona unayafurahia sana haya mambo wewe ndio mdau pia au??
 
Upo sahihi mheshimiwa.
Lakini sheria nyingine zilizowekwa zina ukakasi, mtu anaweza kukamatwa ushahidi upo na sheria ipo wazi lakini baada ya muda anaachiwa huru anaendelea na mambo yake yale.
Mfano ni sheria ya ushoga.
Kwenye mitandao wamejaa mashoga wengi hata hawajifichi.
NI kwamba serikali haioni au mtu kuthibitika ni shoga ni mpaka tutumie kigezo gani? Maana kwa macho tunawaona.

Ile issue ya askari wa zenji najua unaikumbuka. Kulikuwepo hadi na ushahidi wa video lakini mwisho wa siku alionekana hana hatia.

Kuna mambo yanashangaza na kukatisha tamaa hizi juhudi za kuleta maadili.

Hata hao kina mashalove and the like sjui kama watashtakiwa zaidi ya kupewa onyo, na baada ya mwaka au miaka miwili tutawaona wakiendelea na mambo yao.

Nakupongeza kwa kuwa karibu na wananchi na kufatilia matatizo yao.
Ahsante Sana, jamani ngoja mimi nitimize majukumu yangu ya huku uraiani, kule mahakamani nako hutimiza yao kwa mujibu wa Sheria zao na kanuni zao, tufuate utaratibu wa Kila mahali husika kwa mujibu wa majukumu, miongozo na Sheria husika. Ahsante Sana
 
Cheap popularity sasa Mimi inipeleke wapi kwa mfano? Yaani inisadie nini hasa wewe unavyodhani. Si usinipe tu hiyo popularity yaishe😀

Mimi nasimamia Yale ambayo nyie watanzania mmeyawekea Sheria ambazo zinatakiwa kusimamiwa kwa ajili ya kujenga maadili na kuwalinda watoto wenu. Ni hilo tu. Sheria ya mtandao kifungu cha 14 kasome Kiko online. Hii habari ya kuuliza serikali ina mkakati gani na mpango gani na Sheria ziko wapi, muwe mnakumbuka kuwa vyote vipi, na tukianza kusimamia tupeane ushirikiano rafiki.
Kwenye jambo lolote la watu wengi,lazima utegemee maoni has i,uko sahihi chapa Kazi.
 
Back
Top Bottom