Kwa kweli katika mimi ku interact na watanzania walio wengi online, huwa kuna wakati BAADHI yao nawashangaa kuwa, hivi huwa hawajui majukumu ya wizara mbalimbali na Sheria zake au huwa inakuwaje mtu anakushangaa kwa jambo ambalo ni kwa mujibu wa majukumu yako na kwa mujibu wa sheria za nchi yetu ambazo Kila siku wanasema zitungwe na zisimamiwe kikamilifu. Halafu Sasa, akatokea mmoja akaanza kusimamia, inainuka mtu kupinga na kushangaa kulikoni.
Awali nilidhani, wanaomiliki simu janja na siku zote wako online humu wote huwa basi walau wanajua kila kitu, kumbe nilijidanganya.
Ukienda kwa watanzania wengine pamoja na wasio online kule wanakuambia, mbona hamchukui hatua maadili yanazidi kuporomoka? Ukianza kuchukua hatua, BAADHI ya wa online wanasema ndiyo kitu gani hiki cha hovyo huyu anafanya?
Yaani msimamo sasa ni Bora tu uwe kwamba, Kila mmoja ashike la kwake, wa kusimamia majukumu na Sheria asimamie na wa kulaumu naye alaumu tu kwa bidii, pia aelimishwe tu kwa bidii na upole wa hekima, alitaka aelewe alitaka asielewe napo sawa kwani, Kipimo cha haki kitakuja kwa wakati wake.