Kabisa, kumwambia mtoto usilete zero ndani kwangu ni kutokuwajibika? Kwahiyo anataka tukawafanyie quez mashuleni?
Leo nataka kutoa somo, kwa kutoa mfano ambao umenitokea, kwa hawa wapenzi wetu wa zamani ambao tumezaa nao na haikuwa riziki (yaani hatuishi wote)! Hasa wanaoitwa jina ambalo silipendi - single mothers.
Tunapokuwa wakali kwa Watoto wetu mnaoishi nao, msione tunawaonea. Mnapotumia mtoto kama fimbo za kutuchapa, msisahau anayeumia ni mtoto na wanaopata aibu ni wote tuliounganisha vikojoleo akatokea huyo kiumbe!
Imagine mtoto ambaye ana miaka 20 anasahau passport ndani ya ndege, katika nchi ya watu ambayo inapiga vita immigration na kuona Ngozi nyeusi ni wahamiaji haramu, lakini yeye anaona it’s okay! Haoni kusikitika chochote! Hii ni effect ya malezi. Unampigia mama yake, yeye anazidi kukueleza kuwa ni bahati mbaya tu! Na shobo za kujitetea ati amemlea vizuri mwanae ila tatizo hakupata malezi ya wazazi wote wawili wakiishi nyumba moja!!! Mtoto hajutii tendo hilo. Inaumiza na kuonesha unapoteza nguvu na financial resources bure!
Ubaya huelewi unaponitandika kwa kutumia mtoto wako, wewe unapata hasara mara mbili Kwani mimi pamoja na kupata hasara kwa huyu, ninao wengine. Mnadani mnamkomoa hilo jianaume, kumbe mnajikomoa wenyewe.
Chonde chonde, kila wakati kumbuka, kwa vile mtoto hakuwepo wakati mkifaidi kuunganisha vikojoleo, mnapokorofishana, mtoto mwekeni mbali. Baba akijaribu kumfundisha mtoto kuwajibika in hard way, kwa kumweleza kuwa ‘
ukifeli form four, basi wewe si mwanangu ’ kisiwe kigezo cha kumwonesha mtoto kuwa baba hakupendi. Siku Njema