Lema yupo sahihi. Hizi ngonjera zimejaa unafiki, ubaguzi, na ufinyu wa mawazo. Hizo kauli za askofu gwajima kama angekuwa ametoa J.J. Mnyika au kiongozi yeyote wa CHADEMA, Sirro wala asingepoteza sekunde, angeshamteka, siku tano hajulikani yuko wapi, kisha angepigwa kesi ya ugaidi, na kesi ikitajwa mara moja, unaahirishwa mwezi mzima, ingawa Sirro atadai upelelezi umekamilika. Siku ya kesi tutaambiwa hakuna usafiri wa kumleta mtuhumiwa, japo magarivya kumpeleka Sabaya mahakamani kila siku yapo.
Lakini kwa kuwa hizi ngonjera zinasaidia kusahaulisha mambo ya msingi kama KATIBA MPYA, kombe limefunikwa wanaharamu wanapita.
Watanzania tunatekenywa, tunacheka kama mazuzu. Tozo za miamala tunazizoea na kuwashangaa wenzetu Wazambia walivyoizingua chama tawala yao, baada ya kuwazingua. Sisi tunazinguliwa kila uchao, tunachekelea.
Tunaambiwa tuko uchumi wa kati, tunachekelea. Mara oooh, uchumi wetu unapaa si kama kwa wenzetu walio lockdown, tunachekelea. Juzi Samia anatutega, uchumi umezorota, wacha ajenge uchumi kwanza, katiba baadaye. Tunachekelea tena. Huu uchumi wa kati tena unaopaa, lini ulianza kudorora? Hayo wala hatujiulizi. Tunacheka tu kama mazuzu.