#COVID19 Waziri Gwajima: Marekani imechanja 2.4% ya watu wake na J&J

#COVID19 Waziri Gwajima: Marekani imechanja 2.4% ya watu wake na J&J

Chanjo haizuii kupata corona, Wala haizuii usife kwa corona. Hilo unapaswa kulifahamu
Kweli lakin chanjo zinaupa mwili nguvu zaid za kupigana na corona,ivo unaweza ukapata lakin usiumwe au ukaumwa kidogo.
 
Khalafu Marekani waipuuze kwa asilimia 38 ya walio chanjwa. Ujanja ujanja wa kutumia jargons hausaidii. Mungu wa mbinguni atuepushie mbali na maambukizi baada ya kuchanjwa.
Hoja yako hapo haijajaeleweka
 
Hilo la uvaaji glovu nimesha kutoa elimu yake ya kisayansi. Ninairudia tena hapa kama ulikuwa hujaisoma huko juu:

Sababu kubwa ya watoa huduma ya afya kuvaa gloves ni kujikinga kuambukizwa virusi vya hiv na vya hepatitis ikitokea wakashika au kugusa damu ya mtu ambaye ana virusi hivyo. Kabla ya ujio wa virusi vya ukimwi mwaka 1984 walikuwa hawavyai gloves isipokuwa wakati wa operesheni huko theatre ambako walivaa surgical sterile gloves kwa ajili ya kutompandikizia bacteria au fungus mgonjwa wanayemfanyia upasuaji (surgical site infection prevention), kitu ambacho ni hatari sana kwa maisha ya mgonjwa anayefanyiwa surgery. Surgical gloves hizo ziliwakinga wanaofanya operesheni pia wasiambukizwe na virusi vya hepatitis virus kutoka kwenye damu ya mgonjwa wanayempasua. Hata kwenye kuzalisha huko labour ward (delivery rooms) walikuwa hawavyai gloves. Manesi na madaktari walikuwa wanawazalisha mama wajawazito bila kuvaa gloves. Walivyaa surgical gloves tu pale ilipobidi kuongeza njia ya uzazi (vagina) kwa kuichana kwa mkasi (episiotomy) na baadaye kuishona.

Gloves zilizokuwapo ni surgical sterile gloves kwa ajili ya operesheni na non sterilr examination gloves kwa ajili ya examination kwenye maeneo maalum ya mgonjwa mgonjwa kama (i)per rectal examination ambapo daktari anaingiza kidole chake kimoja (index finger) ndani ya mkundu wa mgonjwa na (ii) per vaginal examination ambapo daktari au muuguzi anaingiza vidole viwili au vitatu kwa pamoja ndani ya uke wa mgonjwa.

Examination zingine za mgonjwa au utoaji wa huduma kama kuchoma sindano na kufunga kidonda hakukuhitaji kuvaa gloves ila mtoa huduma alinawa mikono kwa sabuni au antiseptics (hizi antiseptic ndiyo leo mnaziita sanitaizer) kabla na baada ya kumuhudumia/ kumgusa mgonjwa ili kuzuia kusambaza (transmission) vidudu hatarishi kama vya bacteria, virus na fungus (pathogenic microorganism) -- nasocomial infections aka hospital infections. Mbinu nyingine anayotumia mtoa huduma bila kuvaa glovu inaitwa non touch technique - mtoa huduma anahakikisha hagusi damu ya mteja wake. Kwa mfano akishakudunga hiyo sindano ya chanjo, anaweka kipamba (swab) kwenye hiyo sehemu na mgonjwa mwenyewe ndiye anaigandamiza hiyo pamba kwa kidole chake mwenyewe hadi damu itakapoacha kutoka. Hivyo mtoa chanjo hagusi damu ya huyo mteja wake bali mteja ndiye anashika damu yake na baada ya hapo anapewa sehemu ya kuitupa.

Huu uvaaji holela wa gloves zisizo sterile na wala si examination gloves kwa kila mtu ni kwa sababu la kujikinga na janga la ukimwi ingawa pia vinasaidia kukinga kupata virusi vya hepatitis.
 
Hoja yako hapo haijajaeleweka

Marekani wamechanja asilimia kama 40 ya watu wao/Raia. Kumbuka sio kuwa chanjo haiko ila hao 60% waliobaki wanakataa kuchanjwa.

Kati ya 40% walioochanjwa 2.4% ndio walitumia JJ na ilikuwa kabla ya madhara yake kujitokeza. Na yalipojitokeza ndio wale walio sita kuchanjwa wakawa wanakataa katakata kuchanjwa. Serikali yao inafanya kampeni za kulazimishia kuchanjwa. Moja ya silaha ni kutishia kusitishwa kwa ajira yako kama wewe ni muajiriwa..

Hivyo takribani 38% ya waliochanjwa hawakutumia JJ wanatumia nyingine ambazo wanalazimika kuchwanjwa mpaka mara tatu. Hii si mitandao tunaongea na wanaoishi huko.

So unaposikia mtu anasema JJ kuchwanjwa ni mara moja tu 'one shot only' tunabakia kushangaa anazo taarifa za uhakika huyu? Aliye kuletea hiyo ya kuchanjwa mara moja yuko radhi achanje watu wake ya kurudia rudia hadi mara tatu. Hujiongezi tu! Na kusema kulikoni? Hatuwasaidii kwa sababu kwao waliochanjwa taarifa hii is too late.
 
Vp hapa
JamiiForums-2093755274.jpg
 
Wakati akitoa hotuba ya uzinduzi wa chanjo ya Covid 19 aina ya Johnson and Johnson. Waziri wa Afya, Dr. Dorothy Gwajima amesema kuwa Serikali ya Marekani imetumia chanjo hiyo kuwachanja raia milioni 8 wa Marekani.

Sasa ukiangalia population ya USA ni watu 332,915,073.

Ambapo hao milioni 8 ni sawa na 2.4% ya raia wa Marekani wote.

Kwa mtazamo wangu hii chanjo hata Wamarekani wenyewe hawaiamini sana na ndio maana idadi ya watu wake waliochanjwa ni ndogo sana.

Ningependa kujua ni chanjo gani ambayo USA wamechanja asilimia kubwa ya raia wake? Je, kwanini wasingetupatia hiyo?

Sisi tukiweza kuchanja hii yote waliyotupa tutakuwa tumechanja zaidi ya asilimia 6 ya watanzania. Lakini kwao wamekomea tu 2.4%. Hapa kuna mambo ya kujiuliza na kujiridhisha.
Hawaiamini wakati ndio aliyochanjwa joe biden,rais wao?

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Sometimes in life, it worth to be sceptical when the rest or majority are optimistic, and to be optimistic when the rest or majority are sceptical/pessimistic.

Gwajima anaepinga chanjo anaweza kuja kuwa sahihi siku moja.

Mimi binafsi kwa sasa sijui nisimame upande gani, ila muda ndio utanipa jibu
Mwenyekiti wenu alisema chanjo iwe lazima.

Unapingana nae???
 
Experiment ya wapi? millions wameshachanjwa kutumia hiyo chanjo, na mmeletewa za Johnson kwa sababu zile za moderna au Pfizer itakuwa changamoto kutumika Africa maana zinahitaji kuwekwa kwenye baridi 2 - 5 centigrade kwa siku tano tuu la sivyo ni ya kutupa, pigeni chanjo nyie acheni conspiracy za kina Gwajima na ngano zao za kutunga , US at the peak walikuwa wanakufa watu 6000 kwa siku leo wanaokufa ni chini ya 500 kwa siku baada ya chanjo, na wanaokufa 99% hawakupiga chanjo, ni hiari yenu na corona bongo inaua vibaya sana ila tatizo data hazitoki kwa ajiri ya umaskini wetu, piga chanjo uwe salama especially kama umri mkubwa na afya sio nzuri
Wewe unaishi bongo??
 
Hizo za Pfizer na Moderna hatuna uwezo kuzitunza. Zinahitaji mnyororo wa ubaridi (cold chain) wa nyuzi joto minus 90 degrees centigrade (-90 degree C). Mnyororo wetu wa ubaridi wa chanjo hauzidi nyuzi joto minus 4 degrees centigrade ambayo ndiyo ulioko kwenye nchi zote duniani. Huu wa minus 90 degrees ni special, haukuwapo kabla ya ujio wa chanjo za Pfizer na Moderna.

Chanjo za Johnson & Johnson, AstraZenecca na Sinovac ya China zinatumia mnyororo wa ubaridi huu huu tulionao kwa chanjo zingine ambao uko mpaka vijijini kwenye kila zahanati na mobile services zake.
Pfizer -70°C storage nchi zetu hizi ni changamoto kuwa na hizo freezer kwenye kila kituo cha chanjo
IMG_20210729_070622_216.jpg
 
Wewe unauhakika gani ni chanjo wamechanjwa.?Uhiari hauwezi kuwa 100% hata siku moja. Geuzeni mseme kwa viongozi na watumishi wote wa serikali ni lazima. Ndio tutaamini kilichochwanjwa leo ni JJ.

Mchanjaji mwenyewe hajavaa gloves. Hiyo ni medical practice gani? Hilo tu la kutokuvaa gloves lakini kavaa barakoa linaongea mengi.
Ungeenda kwa walinzi wa Raisa uwaambie wakupe kile kichupa cha chanjo ukifanyie chemical analysis mwenyewe kama Chanjo yenyewe kweli.
20210728_125304.jpg
 
Vaccine efficacy ya asilimia 60 inamaanisha WOTE waliopatiwa hiyo chanjo uwezo wao kutougua ugonjwa unaolengwa ni asilimia 60 zaidi ya wale wasio na chanjo. Kwenye Corona wanapima kuugua serious hadi kulazwa na kuhitaji oksijeni pamoja na vifo.
Vaccine efficacy ni tofauti na vaccination coverage. Wewe unaongelea vaccination coverage - yaani asilimia ya watu wote marekani waliopata chanjo.

Mimi ninaongelea vaccine efficacy - yaani hiyo chanjo uliyopatiwa uwezo wake wa kukukinga na huo ugonjwa (yaani mwili wako kujenga kinga aka immunity dhidi ya gonjwa hilo). Tukisema efficacy ya chanjo ya J&J ni 60% tunamaanisha kati ya watu 100 waliopewa hiyo chanjo ni watu 60 tu ndiyo miili yao itapata kinga (immunity) dhidi ya huo ugonjwa. Hao wengine 40 waliobaki hakuna kitakachotokea - yaani ni sawa na wale ambao hawakichanja, hiyo vaccination certificate yao haina maana ye yote.
 
Wakati akitoa hotuba ya uzinduzi wa chanjo ya Covid 19 aina ya Johnson and Johnson. Waziri wa Afya, Dr. Dorothy Gwajima amesema kuwa Serikali ya Marekani imetumia chanjo hiyo kuwachanja raia milioni 8 wa Marekani.

Sasa ukiangalia population ya USA ni watu 332,915,073.

Ambapo hao milioni 8 ni sawa na 2.4% ya raia wa Marekani wote.

Kwa mtazamo wangu hii chanjo hata Wamarekani wenyewe hawaiamini sana na ndio maana idadi ya watu wake waliochanjwa ni ndogo sana.

Ningependa kujua ni chanjo gani ambayo USA wamechanja asilimia kubwa ya raia wake? Je, kwanini wasingetupatia hiyo?

Sisi tukiweza kuchanja hii yote waliyotupa tutakuwa tumechanja zaidi ya asilimia 6 ya watanzania. Lakini kwao wamekomea tu 2.4%. Hapa kuna mambo ya kujiuliza na kujiridhisha.
Pfizer.
 
Ushauri kwa akina Doubting Tom kama wewe: subiri na kuwafuatilia wale waliodungwa hizo sindano leo hapo ikulu. Itakapotokea hata mmoja wao tu akaganda damu kwenye ubongo wake (Mungu apishe mbali) basi wewe kula nduki na wengi kwa kweli tutakufuata! Ila tatizo la akina Doubting Tom hilo lisipotokea bado watasema hizo chanjo walizopatiwa pale ikulu zilikuwa feki (sterile water for injection) za maigizo.
Tatizo wanadai wakishachanja wao wanakuwa salama baada ya hapo yy anakuwa na uwezo mkubwa wa kuambukiza kirusi kingine ambach ni variant wakali mwisho wasiku kinazunguka na kujaa tn kuambukiza waliochanjwa kwa maana hy tutalazimika kuchanjwa kilaa mara maana kirusi kinajibadili km dunia nafikiri ingegekuwa na chanjo mojaa tu kudhibiti hz variant sasa tutawezajee kudhibiti kama kilaa siku zinaibuka vipya
 
Wakati akitoa hotuba ya uzinduzi wa chanjo ya Covid 19 aina ya Johnson and Johnson. Waziri wa Afya, Dr. Dorothy Gwajima amesema kuwa Serikali ya Marekani imetumia chanjo hiyo kuwachanja raia milioni 8 wa Marekani.

Sasa ukiangalia population ya USA ni watu 332,915,073.

Ambapo hao milioni 8 ni sawa na 2.4% ya raia wa Marekani wote.

Kwa mtazamo wangu hii chanjo hata Wamarekani wenyewe hawaiamini sana na ndio maana idadi ya watu wake waliochanjwa ni ndogo sana.

Ningependa kujua ni chanjo gani ambayo USA wamechanja asilimia kubwa ya raia wake? Je, kwanini wasingetupatia hiyo?

Sisi tukiweza kuchanja hii yote waliyotupa tutakuwa tumechanja zaidi ya asilimia 6 ya watanzania. Lakini kwao wamekomea tu 2.4%. Hapa kuna mambo ya kujiuliza na kujiridhisha.
HIVI 1M NI ASILIMIA NGAPI YA 60M
Convert fraction (ratio) 1 / 60 Answer: Convert fraction (ratio) 1 / 60 Answer: 1.666666666667%
2.400000000000
LESS 1.666666666667
0.733333333​
 
Wakati akitoa hotuba ya uzinduzi wa chanjo ya Covid 19 aina ya Johnson and Johnson. Waziri wa Afya, Dr. Dorothy Gwajima amesema kuwa Serikali ya Marekani imetumia chanjo hiyo kuwachanja raia milioni 8 wa Marekani.

Sasa ukiangalia population ya USA ni watu 332,915,073.

Ambapo hao milioni 8 ni sawa na 2.4% ya raia wa Marekani wote.

Kwa mtazamo wangu hii chanjo hata Wamarekani wenyewe hawaiamini sana na ndio maana idadi ya watu wake waliochanjwa ni ndogo sana.

Ningependa kujua ni chanjo gani ambayo USA wamechanja asilimia kubwa ya raia wake? Je, kwanini wasingetupatia hiyo?

Sisi tukiweza kuchanja hii yote waliyotupa tutakuwa tumechanja zaidi ya asilimia 6 ya watanzania. Lakini kwao wamekomea tu 2.4%. Hapa kuna mambo ya kujiuliza na kujiridhisha.
Huyu mama namuona Kama comedian vile,hachukulii Mambo serious,amenishangaza Sana Jana,baada ya kuchanjwa tu aiaanza kurukaruka huku akijua side effects za dawa lolote laweza tokea.
Hi inanifanya niamini hakuchomwa dawa ila water for injection.
 
Ungeenda kwa walinzi wa Raisa uwaambie wakupe kile kichupa cha chanjo ukifanyie chemical analysis mwenyewe kama Chanjo yenyewe kweli.View attachment 1872408

Huyu kwenye picha ni nani? Barakoa imenitoa ushamba wa kutambua sura. Naonesha bado unashangila ushindi wa simba kule kigoma. Mjiongeze kwenye ujumbe uliobebwa na tai.
 
Back
Top Bottom