Waziri Gwajima: Muswada wa sheria ya Bima ya Afya kwa wote kufikishwa bungeni hivi karibuni!

Waziri Gwajima: Muswada wa sheria ya Bima ya Afya kwa wote kufikishwa bungeni hivi karibuni!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Waziri wa afya mh Gwajima amesema muswada wa Bima ya afya kwa wote utawasilishwa bungeni hivi karibuni.

Waziri Gwajima amesema baada ya sheria ya Bima ya afya kupitishwa basi wananchi wote wataingizwa katika utaratibu huo na hivyo kuwapa uhakika wa tiba.

Source TBC

Maendeleo hayana vyama!

=====

Waziri wa Afya, Dkt. Dorothy Gwajima amesema Wizara hiyo inakamilisha Muswada wa Bima ya Afya kwa wote ambao utawasilishwa Bungeni

Ameeleza, hatua hiyo itachangia kwa kiasi kikubwa kumaliza matatizo ya Wananchi wengi wanaoshindwa kupata huduma stahiki mahali popote

Kuhusu upotevu wa Dawa Vituoni, Dkt. Gwajima amesema ukaguzi unafanyika na maamuzi yatachukuliwa kwa wanaopoteza Dawa na kuhujumu mapato
 
NHIF au ipi, kwa sababu bima hii kuna dawa hupewi na kuna matibabu hupatiwi,. Au unapeleka waraka na sina ya bima mpya?
 
NHIF au Ipi, kwa sababu bima hii kuna dawa hupewi na kuna matibabu hupatiwi,. Au unapeleka Muswada na aina ya bima mpya?
 
Sawa wa sawa.

Napendekeza kila dreva hasa hasa Hawa bodaboda.

Bima za afya iwe Ni lazima na iwekwe kabisa kwny checklist za matrafiki barabarani Kama zilivyo vyombo vya Moto.

Madereva wengi na Boda boda wengi wanafia mawodini kwa kashindwa kumudu gharama za matibabu.
 
NHIF au Ipi, kwa sababu bima hii kuna dawa hupewi na kuna matibabu hupatiwi,. Au unapeleka Muswada na aina ya bima mpya?
Ni kweli baadhi ya dawa hazipo lakini bado uhitajia wa bima ni muhimu sana.

Mfano kuna clinic nahudhuria kuna dawa mbili (moja ina 45-60k kwenye maduka ya madawa nyingine ni 18-21k )

Ya 45-60k sio combianation bima wanatoa.

Ila ya 18-21k ni combianation (hii haipo kwenye bima nanunua mwenywe)

Ila nikizingatia gharama nza hiyo ya kwanza tu naona umuhimu wa bima
 
Pelekeni hata mswaada wa kututoa roho zetu, mmeshatuchosha na unafiki wenu CCM.

Huo mswaada wa bima za afya raia wasifikirie watatibiwa bure, wajiandae kila raia kutozwa 100,000/= kila mwaka kulipia hio bima, na gharama za kujitibu kwa hela taslimu zitapanda mara kumi ili watu wakimbilie kwenye bima.

Utaambiwa kupima malaria Sh 15,000/= kwa hela taslimu, na kwa bima makato ni Elf 2,000/=.

Hii nchi kila kitu ni sinema tu, ila ukweli ni kwamba zinatafuta kila njia kumtapeli raia wa chini.
 
Ni kweli baadhi ya dawa hazipo lakini bado uhitajia wa bima ni muhimu sana.

Mfano kuna clinic nahudhuria kuna dawa mbili (moja ina 45-60k kwenye maduka ya madawa nyingine ni 18-21k )

Ya 45-60k sio combianation bima wanatoa.
Ila ya 18-21k ni combianation (hii haipo kwenye bima nanunua mwenywe)

Ila nikizingatia gharama nza hiyo ya kwanza tu naona umuhimu wa bima
Kusema tu watapeleka mswada wa bima kwa kila raia haitoshi. Na kila raia kuwa na bima tu haitoshi. Tusubiri tuone masharti ya hiyo bima na jinsi hospital zitakavyo-respond. Kwa kifupi tusubiri tuone kama kutakuwa na unafuu wowote kulinganisha na sasa. Nasema hivyo kwa sababu kuna member mmoja hapa alisema serikali yetu ina tabia ya kushughulikia matatizo kwa kutengengeneza matatizo. Nimekunukuu tu ila sijapingana na ulichosema. Nimejaribu kukazia.
 
Waziri wa afya mh Gwajima amesema muswada wa Bima ya afya kwa wote utawasilishwa bungeni hivi karibuni.

Waziri Gwajima amesema baada ya sheria ya Bima ya afya kupitishwa basi wananchi wote wataingizwa katika utaratibu huo na hivyo kuwapa uhakika wa tiba.

Source TBC

Maendeleo hayana vyama!
Kuwapa uhakika wa Tiba ? Au tuambiane ukweli ni kwamba kuhakikisha kila mtu anachangia / anakatwa pesa.....

Uhakika wa Tiba ni jambo lingine (as kuna mambo mengi, tiba ambazo hazipo kwenye Bima, Huduma kulingana na pesa uliyotoa n.k.) na kwa mwenendo wa hawa mabwana sidhani kama hapa kutakuwa na value for money...
 
Porojo tu, utasikia kila mtu ana bima ya afya, lakini utakuta magonjwa yote ya ghali hayatibiwi kwa bima.
Na siyo magonjwa ya ghali tu. Utakuta hospital zote zitakuwa ''in chaos'', vurugu mechi, huduma mbovu mpaka watu waseme ni bora tulipokuwa tunatibiwa kwa malipo. Uzoefu unaonyesha serikali za kitawala kama yetu zinazotumia top botton approach kutawala kila zinapojaribu kutatua tatizo, ndivyo zinavyozidi kuongeza tatizo.
 
Kuwapa uhakika wa Tiba ? Au tuambiane ukweli ni kwamba kuhakikisha kila mtu anachangia / anakatwa pesa.....

Uhakika wa Tiba ni jambo lingine (as kuna mambo mengi, tiba ambazo hazipo kwenye Bima, Huduma kulingana na pesa uliyotoa n.k.) na kwa mwenendo wa hawa mabwana sidhani kama hapa kutakuwa na value for money...
Unaelewa maana ya Bima ya afya kwa wote?!
 
Na siyo magonjwa ya ghali tu. Utakuta hospital zote zitakuwa ''in chaos'', vurugu mechi, huduma mbovu mpaka watu waseme ni bora tulipokuwa tunatibiwa kwa malipo. Uzoefu unaonyesha serikali za kitawala kama yetu zinazotumia top botton approach kutawala kila zinapojaribu kutatua tatizo, ndivyo zinavyozidi kuongeza tatizo.

Exactly.
 
Unaelewa maana ya Bima ya afya kwa wote?!
Cha maana kwa Serikali inayojali ni kuhakikisha kuna Afya kwa wote.. yaani Health Care ifike within reach ya kila raia (no matter circumstances zao)..

Kitakachotokea hapa utakutana na BIMA ambazo ni profit oriented na mwisho wa siku utapata Models kama za US na sio UK..., utakuta BIMA ambayo unalipia ila mambo kadha wa kadha hayapo covered kwenye hio BIMA na huduma yako inategemea aina ya BIMA yako..., ingawa as usual kwenye vitabu itaonekana kwamba serikali inajali na inatoa Afya kwa Wote, kama tu ilivyo Elimu Bure...
 
Na siyo magonjwa ya ghali tu. Utakuta hospital zote zitakuwa ''in chaos'', vurugu mechi, huduma mbovu mpaka watu waseme ni bora tulipokuwa tunatibiwa kwa malipo. Uzoefu unaonyesha serikali za kitawala kama yetu zinazotumia top botton approach kutawala kila zinapojaribu kutatua tatizo, ndivyo zinavyozidi kuongeza tatizo.
You said it all
 
Upuuzi mtupu
Apeleke na mswaada wa sheria kila mtu lazima ajifukuze nyungu ya Jaffo na Musukuma
Nina NHIF juzi nimeenda JKCI hakuna dawa za matibabu ya moyo kwenye hospitali kubwa kuliko yote ya maradhi ya moyo nchini
 
Kama bima yenyewe ndio itabaki kuwa hii Ichf,heri waachane tu na mswada wenyewe.
 
Utopole mtupu .mtu anayeshadadia ichif naona kwanza hajielew hujui mfumo wetu wa afya ulivyo
 
Back
Top Bottom