#COVID19 Waziri Gwajima: Viongozi wa Serikali wasiochanjwa waachie ngazi

#COVID19 Waziri Gwajima: Viongozi wa Serikali wasiochanjwa waachie ngazi

Naunga mkono hoja, hiki alichokisema Waziri Gwajima, ni kitu cha kweli, kama serikali yako imekubali chanjo na rais wako kachanja, wewe kiongozi wa umma, lazima uonyeshe uongozi kwa vitendo na kwa mfano, kwa viongozi wote wakuu wa umma lazima wachanje hadharani, ule uhiari, hauwahusu viongozi wa umma, kwa viongozi wa umma kuchanja ni lazima, asiyechanja aachie ngazi!.

Niliwahi kusema mahali, chanjo ya Korona japo inasemwa kuwa ni hiyari, hii ni hiyari ya lazima, kuna nchi mtu huruhusiwi kuingia bila cheti cha chanjo ya Corona. Hivyo sasa tunaanza mdogo mdogo kwa viongozi wa umma, chanjo sio hiyari ni lazima,
kama wewe ni kiongozi wa umma na huamini chanjo, achia ngazi!.
P.
P

Daaa sasa Mkuu Hadharani tena?
Cha Msingi si Cheti cha Chanjo?
Mambo ya Hadharani tena[emoji30][emoji15][emoji24]
 
Si ni hiari au......alafu yeye ni mamlaka yao ya uteuzi? Au anabwabwaja kujionesha
Waziri Mkenda amuulize alichoambiwa na Raisi aliingilia eneo la Raisi la biashara za mambo nje ambayo sio eneo lake akalitolea tamko bila kupewa idhini na Raisi

Gwajima haajiri mtu hata kwenye wizara yake ya afya Ni utumishi Ndio huajiri .Yeye anatoa tamko Kama Nani? Waziri wa utumishi au Raisi ndie alitakiwa kutoa Hilo tamko japo lingekuwa challenged mahakamani kwa sababu kwenye barua na mkataba wa ajira hakukuwa na kipengele Cha kusema utaacha kazi au kuachishwa kwa kutochanja chanjo!!!! Gwajima akasome mikataba ya ajira inasemaje na barua za kuajiriwa zinasemaje kuhusu kuacha kazi nk
 
Hizo chanjo mkachanje mbwa na kuku ila binadamu zinaua Kinga asili ya mwili
 
Huyo mama me kunasiku nilimsikia akisema kua baada ya yeye kuchanjwa, mumewe alitest mitambo akakuta iko poa.

Tangu hapo huyo mama me namchukulia tofauti na mnavyo mchukulia wenzangu.

Hebu tudokeze kidogo, wewe unamchukuliaje?
 
Waziri wa Afya, Dorothy Gwajima karudi na rungu.

Ametoa rai kuwa viongozi ambao mpaka sasa hawajachanjwa, watatakiwa waachie ngazi kwani hawawezi kusimamia kampeni ya kusimamia uchanjwaji dhidi ya corona.

Waziri wa Afya amesema kama Rais kachanja ili iwe mfano, sasa hao viongozi hawatetei msimamo wa Serikali

Tulisha liona hili huko nyuma: #COVID19 - Kuchanja sasa kuwe lazima, hasa wafanyakazi serikalini. Chanja au achia ngazi

View attachment 2028866
Nnaona mambo 2

1) viongz wa serikali wata fake hzo taarifa(vyeti)
4)wanatafuta gia ya kuwaingiza watu kwa lazima kutoka kwenye maamz ya Mwili wa mtu(self control) kwenda kwenye maamzi ya mtu mwingine( secondary control) na kwenye hyo stage ya pili, mwanadam anakuwa Hana maamzi yake mwenyewe ila anaamliwa na mtu mwingine ambae ana mcontrol body system... Ni hatari kuu
 
Jee wale Viongozi waliopiganisha na kupata vyeti vya chanjo japo hwakuchanja wanataka waachie ngazi au waendelee kushikilia hizo ngazi?
 
Chama kimerudi kwa wenyewe-Kigwangala.

 
Wanyonge wenzangu msipuuze Tiba zetu za Nyungu na zile tangawizi na malimao japo tumekwjeliwa sana
 
Mliochanja mnatuonea wivu sana tusiotaka hizi chanjo zenu
Tatizo sio kutaka tatizo ni tz sio kisiwa,
So ni suggests tu kama ambavyo inchi zinafunga mipaka na sie daslamu pia tunafunga ili wageni wetu wasidhurike au wasitudhuru
 
Hakuna cha hiyari hapa,
Chanja au tuachie kazi yetu,
Chanja au baki nyumbani,
Chanja au usije mjini
Huo ndio ukweli
 
Waziri wa Afya, Dorothy Gwajima karudi na rungu.

Ametoa rai kuwa viongozi ambao mpaka sasa hawajachanjwa, watatakiwa waachie ngazi kwani hawawezi kusimamia kampeni ya kusimamia uchanjwaji dhidi ya corona.

Waziri wa Afya amesema kama Rais kachanja ili iwe mfano, sasa hao viongozi hawatetei msimamo wa Serikali

Tulisha liona hili huko nyuma: #COVID19 - Kuchanja sasa kuwe lazima, hasa wafanyakazi serikalini. Chanja au achia ngazi

View attachment 2028866
Mental disorder
 
Mliochanja mnatuonea wivu sana tusiotaka hizi chanjo zenu
Kweli!! Walikinga mabega kuiga Ulaya, sasa ulaya wanapata ya 3 na ya 4 bila mafanikio. Waziri naye kichwa kibovu. Atueleze wapi chanjo ilipofanikiwa. Corona inapotea na kuibuka kwa sababu za hali ya hewa. munalo tu!
 
Mheshimiwa waziri anapata wasaa wa kupitia maandishi ya wataalamu wenzake waloko field kufanya utafiti?



 
Back
Top Bottom