#COVID19 Waziri Gwajima: Viongozi wa Serikali wasiochanjwa waachie ngazi

#COVID19 Waziri Gwajima: Viongozi wa Serikali wasiochanjwa waachie ngazi

Pesa za Mkopo wamepokea wenyewe wanataka kulazimisha
Hakuna kitu cha bure hata Mkopo nao unakuja na vigezo
 
Corona ana vituko..duh..kashakuja kivingine kutisha watu..
Huyu ni mdudu mwenye kujitambua na ni pepo kamili
Mkianza kusahau anakuja kivingine..ameshindwa kwa jina la Yesuuu
 
Waziri wa afya Dr Dorothy Gwajima amewataka viongozi wite wa serikali ambao hawajachanjwa chanjo ya Corona waavhie ngazi mara moja.

Waziri Gwajima amesema kiongozi asiyechanja hawezi kuwa na hamasa ya kushswishi watu wengine Wachanjwe ndio maana mimi kama waziri natoa ushauri wajiuzulu nafasi zao mara moja.

Source: ITV habari
Haya mambo ya kipuuzi kabisa. Unataka watu wachanje kwa lazima ! Chanjo ambayo haiwezi kumkinga mtu na kirusi kipya! Au waziri hujasika hata huko kwa wenye chanjo kirusi kipya kinapeta tu. Tulia mama ,kama ni mapesa yao warejesheeni tu.
 
Madaraka mwana malevya na dharau kubwa sana kwa watanzania. Huyu anachokiongea sio yeye ametumwa na viongozi wake wakubwa atamke hivyo. Hiari na ulazima unatokea wapi?

Anguko la serikali liko karibu sana kutokea muda sio mrefu kwa Mungu hataniwi.
Kwa hiyo wewe kuumwa ni hiari.
Na kuanguka kwa serikali kwa sababu wewe hutaki kuchanja kunatoka wapi?
 
Naunga mkono hoja, hiki alichokisema Waziri Gwajima, ni kitu cha kweli, kama serikali yako imekubali chanjo na rais wako kachanja, wewe kiongozi wa umma, lazima uonyeshe uongozi kwa vitendo na kwa mfano, kwa viongozi wote wakuu wa umma lazima wachanje hadharani, ule uhiari, hauwahusu viongozi wa umma, kwa viongozi wa umma kuchanja ni lazima, asiyechanja aachie ngazi!.

Niliwahi kusema mahali, chanjo ya Korona japo inasemwa kuwa ni hiyari, hii ni hiyari ya lazima, kuna nchi mtu huruhusiwi kuingia bila cheti cha chanjo ya Corona. Hivyo sasa tunaanza mdogo mdogo kwa viongozi wa umma, chanjo sio hiyari ni lazima,
kama wewe ni kiongozi wa umma na huamini chanjo, achia ngazi!.
P.
P
Hata mi naunga mkono wakati nchi nyingine kama Botswana waliagiza chanjo moderna
wakati omicron inaanza lakini hawakupata na wananchi wao wanataka chanjo uku TZ watu bado wako brain washed kuwa chanjo mbaya ndio maana hatuendelei sababu uelewa wetu wa vitu vidogo tu ni tatizo Raisi na viongozi wametuonyesha mfano bado ni wabishi.

Hongera sana Mama Gwajima kwa hatua nzuri uliyochukua.
 
Kwani ameshaletewa chanjo za omicron? Bibi haeleweki
 
Duuh! Mbona rais alisema kuwa NI HIARI? Viongozi hawana haki ya kutumia hiyo hiari?

Huyu waziri akiambiwa kuwa kauli yake ni NONSENSE atalalamika?
Kwenye vyombo vya usafiri bado barakoa zina valiwa kweli
 
VIONGOZI AMBAO HAWAJACHANJWA CORONA ACHIENI NGAZI
Waziri wa Afya Dkt.Dorothy Gwajima amewataka viongozi wa umma na watendaji wa Serikali ambao hawajapata chanjo ya Corona kujiuzulu nafasi zao kwani hawawezi kuwashawishi wananchi kuchanjwa wakati wao wamegoma kupokea chanjo hiyo https://t.co/LBOdtnjnzI
View attachment 2028595
hapo pichani naona waziri kachukua tahadhari zote za kujikinga na korona
 
Za kunyapia nyapia ni kwamba hakuna cha mutation wala baba yake na mutation, kirusi kinaendelea kukarabatiwa maabara na kuachiwa kikiwa na nguvu mpya........wacha tuendelee kuhesabu mawimbi.
Mkuu hata mimi naamini hawa virusi wanafyatulia sehem husika.
Yani kuna wajinga wanafanya kufyetua tu, leo wanaleta sample hii, ikiisha nguvu wanafyatua kingine chenye nguvu zaidi ya kile cha awali.
 
Mbowe aliwahi kusema tena kwa jazba kuwa, Serikali ilete chanjo na watu wachanjwe kwa lazima....Huenda sasa tuko kwenye utekelezaji. Kila kiongozi anafanya lake kama kwamba hatuna kiongozi mkuu??. 😳
Tena hili swala la chanjo limewatia haibu mpaka viongozi wa Chadema.
Maana kipindi serkali iliyo pita iligomea chanjo, wapinzani wake ambao ndio Chadema wao walikua wakiilazimisha serkali ilete chanjo.
Sasa chanjo imekuja na hatuoni msaada wowote kutoka kwenye hiyo chanjo.
 
Huyo mama me kunasiku nilimsikia akisema kua baada ya yeye kuchanjwa, mumewe alitest mitambo akakuta iko poa.

Tangu hapo huyo mama me namchukulia tofauti na mnavyo mchukulia wenzangu.
 
bibitozo alisema ni hiari sasa huku kuwajibishana wapi na wapi
 
Back
Top Bottom