Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Waziri Dkt. Gwajima D salam,
Moja ya tukio kubwa wiki hii ni suala la wanafunzi zaidi 100 kukutwa na simu shuleni na baadhi yao kufukuzwa baada ya kupiga picha za utupu na picha hizo kusambaa.
Katika kushughulika na suala hili busara inahitajika zaidi kuliko kukurupuka. Kwanza tuelewe hawa na watoto na wapo katika hatua ya ukuaji, na katika hatua mengi hutokea ikiwemo kufuata mikumbo na kujaribu mambo mbalimbali kutokana na vichocheo vya miili yao pamoja na shauku ya kutaka kujua na kujaribu mambo mbalimbali.
Kwa tulipita na kuonja shule za bweni hata kidogo tunajua mambo za simu shuleni, na siyo kwamba kuna mambo ya maana yanafanyika mengi ni kwaajili ya kupiga picha, kuwasiliana na viboifrendi, kuonesha kwamba na wewe una simu, nk. Pamoja na sheria kali shuleni wanafunzi watapata njia tu ya kufikisha simu shuleni na hii si kwa wote wavulana na wasichana.
Pia soma:
Tabora: Wanafunzi wafukuzwa kwa kujirekodi picha za utupu na kuzisambaza
Inapotokea suala kama hili imefikia mpaka wamejipiga picha na kusambaza, ndio wapewe adhabu lakini iwe ya kuwajenga. Wanatakiwa kupewa elimu kwa udogo wao huo huo waelewe kwanza kufuata utaratibu wa kutopeleka simu shuleni, lakini pia wafundishwe matumizi salama ya simu.
Ifanyike open discussion waelewe mtandaoni kuna mambo mengi, lakini unatakiwa kutumia njia hii, lakini pia waelezwe athari ya kupiga picha hizo na kuziweka mtandaoni, waelewe mtandao hausahau na jinsi inavyoweza kuwaharibia mbeleni, na hili siyo tu kuathiri kwao bali hata kwa wazazi/walezi wao, familia na hata inavyoweza kuwaathiri wenzao.
Lakini pia hili lisiishie tu kwao, hata wazazi wa watoto hawa wapate elimu hiyo pia (huko mbeleni unaweza kutengeza program zinazowakutaisha wazazi na walezi kwenye masuala ya matumizi salama ya digitali).
Wamefukuzwa shule jua tu na huko nyumani moto utaenda kuwaka na mzazi anaweza hata kuua mtoto kwa kipigo. Naomba Waziri Dkt. Gwajima D uende na jambo hili kwa busara sana.
Pia kuna baadhi ya page kwenye mitandao ya kijamii wameweka picha za wanafunzi hawa, umetagiwa kwenye baadhi, picha hizo zinatakiwa kuondolewa, ni kuendeleza udhalilishaji kwa watoto hawa na kwenda kinyume pia na sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi na haki za watoto.
Waziri Gwajima ametoa update hapa >> Waziri Dorothy Gwajima: Wanafunzi waliojirekodi picha za utupu na kusambaza kurekebishwa tabia na kurudi shule