Waziri Gwajima, wanafunzi kufukuzwa shule sababu ya picha za utupu siyo suluhisho na haiwasaidii, wanatakiwa kupewa mwongozo na kuelewa athari zake

Mkuu una shida mahali fulani...
Yaani kama upo serious kutetea hili una matatizo wewe...

Kitendo cha kufukuzwa tuu ni kusaidiwa kwenyewe huko...
Upate msaada haraka, vingenevyo kama nilivyosema hapo juu utakuwa disaster kubwa kama mzazi.

Mtoto akinyea mkono huukati, unaosha, unamsafisha na kumuweka vizuri unaendelea na kazi nyingine.

Kama hivyo ndivyo ulikuzwa, badili hilo kwa watoto wako usije kuendeleza disaster nyingine
 
Ilipaswa mtu akikamatwa na simu bila kujali thamani yake inataifishwa moja kwa moja bila kurudishiwa na kupewa onyo kali,

Na endapo mtu akikamatwa na simu na tena basi ndio afukuzwe
Kufukuzwa ni hatua ya mwisho kabisa, huku mwanzo atapewa dhabu nyinginr kama ulivyosema lakini pia ni muhimu watoto hawa kufundishwa matumizi salama ya vifaa hivi, maana siyo porn tu hata trafficking zinafanyika huko na moja ya kundi linalokuwa targeted sana ni watoto
 
Mkuu mimi sina strong point kutetea hili suala ila kiufupi hatua ya kufukuzwa hao watoto shule watu hawajakurupuka..
 
Mkuu mimi sina strong point kutetea hili suala ila kiufupi hatua ya kufukuzwa hao watoto shule watu hawajakurupuka..
Huna strong point na bado unajitetea😹😹😹, mkuu pata msaada wa haraka... unakuwa kama hujapita shule na hili ndio mara ya kwanza kulisikia. Wanahitaji msaada, wapewe adhabu ya kuelewa walichofanya ni kosa, lakini wasaidie kuelewa ukubwa wa tatizo hili
 
Nadhani hapo kwenye red bold ndiyo nchi inatakiwa iweke mkazo, kuenrol watoto wengi kwenda secondary wakati quality ya elimu ya msingi ni tatizo, hapo unakuwa hujafanya kitu. Elimu yetu ni mbovu kwanzia kwenye shule ya msingi, ukichunguza vizuri unaweza kukuta wanafunzi wengi wa kidato cha kwanza ukiwapa mtihani standard wa darasa la 5 wanafeli. Ni bora waboreshe elimu ya msingi na mchujo ufanyike wa maana kwenda secondary, the rest wapelekwe vocational trainings
 
Ni kwasababu siyo mtoto wako ndio maana, akiwa wako utatafuta njia za kumsaidia kuhakikisha anarudi kwenye mstari.... badala ya kuwashukia watoto inabidi tuangalie mzizi wa tatizo na kuanzia hapo
Mzizi hamjaona kwani mpk sahvi
Vitoto hivyo vishakata kamba
Haviambiliki havisiki

Ova
 
Hivi hizo connection huwa,mnazipatia wapi? Kweli kila mtu ana koneksheni zake
 
Kwa hiyo ww kama ulikuwa muhuni shuleni basi unadhani na wengine walikuwa wahuni kama ww?
Nyinyi wazazi ndo mzizi wa tatizo kwa kuendekeza malezi ya kizungu yaliyo jaa upumbavu mwingi, mtoto wa sekondari unamnunulia smartphone ya kazi gani kama sio upumbavu ?
Mwenye jukumu la kuhakikisha mtoto ana maadili mazuri ni mzazi na sio kazi ya serikali,kazi ya serikali ni kukuadhibu pale utakapo vunja sheria za nchi.

Africa mpaka sasa tumeshindwa kuendelea kwa kuendekeza na kuleana kwenye mambo ya kipuuzi.
 
😂😂😂😂😂😂😂😂😂 Sawa sawa ngoja tuone...
thank you but education is better than money i sapport due to following point BICHWA KOMWE -
 
Video Iko wapi,tuone hayo maadili yanavovunjwa?
 
Kuwakufuza 'was not right judgement'. Wailitakiwa waelekezwe tu kwamba kufanya hivyo si vizuri, lakini kuwafukuza ni kuharibu future yao. Sasa picha za ngongo na kuharibu future ya mtu wapi na wapi? Ningeelewa kama ni suspension ya muda ili baadaye waweze kuendelea tena, lakini kama it is for good, ni wrong!
 
Acha unafki we mbuzi, nyie ndio wale mnamchangia mhalifu
Hakuna sehemu nilipokutukana wala kukudhalilisha Mkuu, hili pia linaonesha upeo wako ni finyu, na unahitaji darasa la kutosha usije kuwa disaster kama mzazi huko mbeleni, na kama ni mzazi tayari Muumba akusaidie
 
Mwanafunzi mpaka afanye kosa gani ndio afukuzwe SHULE? Au adhabu ya kufukuzwa nayo ifutwe
 
Mm naungana nae kwa upande Fulani linapotokea tatizo tusikimbilie upande mmoja tuangalie na uapnde mwingine ,,Hapo watoto wamefuzwa sawa huko wanakoenda si watafanya hayo hayo cha msingi ni kuwaelimisha na wabishi wanakula kwata la kijeshi
 
Mzizi hamjaona kwani mpk sahvi
Vitoto hivyo vishakata kamba
Haviambiliki havisiki

Ova
Watoto hao wanajilea wenyewe? Sisi si ndio wazazi na walezi, wajomba, mashangazi kaka na dada, wao ni matokeo ya sisi, hivyo ni kuandalia wapi tunakosea turekebishe ili matokeo yawe mazuri
 
Hivi hizo connection huwa,mnazipatia wapi? Kweli kila mtu ana koneksheni zake
Wewe katika yote hayo umeona connection tu? Ndio pedophiles mnaoenda haribu hawa watoto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…