Waziri Gwajima, wanafunzi kufukuzwa shule sababu ya picha za utupu siyo suluhisho na haiwasaidii, wanatakiwa kupewa mwongozo na kuelewa athari zake

Wewe katika yote hayo umeona connection tu? Ndio pedophiles mnaoenda haribu hawa watoto
Dada jishikilie usiharibu mada yako nzuri...unajua kwanini nimeuliza hivyo?? Mm sio muumini wa hizo video chafu ndo maana nimeuliza huwa wanazipatia wapi..naona unakuja ku ni attack heee...
 
Hapa ndio ndio ujue kwamba nchi ime fail sasa kuwafukuza si ndio kuongeza tatizo juu ya tatizo.
 
Nilivyosikia wamefukuzwa kisha watapelekwa kwenye vituo vya kurekebisha tabia kisha watatufutiwa shule nyingine.
Wamefukuzwa ili wasiambukize wenzao ujinga.
Pia kama onyo kwa watoto wengine.
 
Hawa wafukuzwe wakatafute shule nyingine, wenzao wakiona hakuna kufukuzwa, nao wataiga hizi mambo.
 
Ujumbe mzuri sana.
Sisi tunatumia nguvu kubwa mno kudhibiti badala ya kuelimisha.
Mwanafunzi anapomaliza kidato cha nne, anayekwenda kidato cha tano haruhusiwi kumiliki na kutumia simu awapo shuleni.
Mwenzake anayekwenda chuo cha kati (tabibu, afisa ugani, ufundi nk) anaruhusiwa kumiliki simu wakati wowote.
Kwa nini kuna ubaguzi huu?
Hata hivyo hatujui manufaa ya simu katika kujifunza?
Je, ni hatua gani ya elimu iliyojikita kufunza matumizi bora ya simu na matumizi yasiyofaa.
Iwapo tutaendelea na tabii hii ya kudhibiti badala ya kufunza na.kuelekeza, tujiandae kwa maafa makubwa zaidi.
Hawa ni waliofahamika. Wapo wengi mno ambao hawajakamatwa. Si ajabu shule nyingine ni wanafunzi wote.
Iwapo tunaandaa nchi ya wasomi, yaani wananchi waungwana, tuachane na kuwaza kufukuzafukuza kwa kila kosa.
Tunao viongozi mbalimbali wanaofanya kazi zao vema sasa lakini wakiwa shuleni waliwahi kukengeuka. Walisaidiwa kurekebika badala ya kufukuzwa.
 
Dada jishikilie usiharibu mada yako nzuri...unajua kwanini nimeuliza hivyo?? Mm sio muumini wa hizo video chafu ndo maana nimeuliza huwa wanazipatia wapi..naona unakuja ku ni attack heee...
Nimerudisha statement yangu Mkuu, kwa ulivyoweka ni kama ulikuwa unaulizia connection
 
Nilivyosikia wamefukuzwa kisha watapelekwa kwenye vituo vya kurekebisha tabia kisha watatufutiwa shule nyingine.
Wamefukuzwa ili wasiambukize wenzao ujinga.
Pia kama onyo kwa watoto wengine.
Ametoa statement baada ya kelele kuwa nyingi, mwanzo walifukuzwa
 
Kama hawaelewi athari zake basi hawafai kuendelea kuwa wanafunzi. Wapewe muda wa kufanya hiyo michezo huko nje ya shule.
 
Kama hawaewi athari basi hawafai kuendelea kuwa wanafunzi. Wapewe muda wa kufanya hiyo michezo huko.
Soma tena uelewe na kufuatilia mdajala, halafu uje ucomment tena, nina imani utajifunza kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…