Waziri Hussein Bashe aagiza Mshindo Msola akamatwe

Ametoa agizo hilo baada ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Njombe kwa kushirikiana na wale wa kamati ya siasa ya mkoa huo wakiongozwa na mkuu wa mkoa huo Antony Mtaka kufika katika ghala hilo na kukuta shehena ya mifuko ya mchanga katikati ya mifuko ya mbolea ya Minjingu.
Ufisadi huu...
 
watengenezaji wa mbolea ya minjingu huu ujinga hawajaanza leo wemekuwa na skendo hii miaka mingi ila zilikuwa zinafunikwa

bashe nae mbabaishaji tu, anakomaa na mbolea za ruzuku wakati wa kulima wa tumbaku mbolea bei juu na ruzuku kwao imekuwa ndoto

mkulima wa tumbaku mbolea ananunua Tsh 177,000 wakati wengine wananunua 70,000
 
Yeye mwenyewe ni walewale. Aliwapa viashiria mapema alivyoingia madarakani. Hataki ukali, kamtupa sabaya lupango na kuwarejesha waliyotemwa na jpm, kawaambia vigogo wale kwa urefu wa kamba zao za malisho. Kampiga jpm vijembe.
Unataka maelezo gani zaidi.😎😆
Kama hili la kuwaambia viongozi wale kwa urefu wa kamba zao kama kuna Mtanzania alilipokea kwa furaha, basi tuna safari ndefu kuyafikia maendeleo!
 
Wajinga dizaini hii wanapaswa kunyongwa napema sana na hela ya kununua kamba wachangishwe wana familia wa huyu mpuuzi.
Ndo wale wale walimkaribisha waziri kufungua mradi wa maji kumbe wamejaza maji kwenye tanki kubwa limefichwa mlimani, baada ya waziri kuondoka raia wamechota maji jioni tu maji yamekata
Hahaha binadamu kazi sana.
 
Haya mambo ndo tulitegemea vyombo vyetu vya dola (vikiwemo vya usalama), kushughulikia na kuyabaini mapema kabla hata raia hawajaathirika nayo, lakini kwa bahati mbaya sana, baadhi yao wameamua na wameridhika kabisa kuwa chawa wa viongozi badala ya kusimamia maslahi ya nchi na watu wake!
 
Nimeona kwenye taarifa ya habari mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka akiagizwa na Waziri wa kilimo Hussein Bashe kumkamata Rais wa zamani wa Yanga dkt Mshindo Msolla kwa kusambaza mifuko 776 ya mbolea ya minjingu iliyojaa michanga badala ya mbolea halisi.

Msolla alikuwa anatia huruma, hata hivyo ameiomba serikali imsamehe kwa hoja kuwa wafanyakazi wake ndio wamefanya uhuni huo na yuko tayari kutoa ushirikiano kwao ili wafanyakazi hao wakamatwe.

Pole sana Msolla
 
Wazir wa Kilimo ameagiza Mshindo Msolwa na wafanyakazi wengine wanosimamia ghala la kuhifadhi Mbolea wakamatwwe baada ya kubainika wamehifadhi mchanga unaofhaniwa unatumika aidha kama bosheni au kuchakachua Mbolea inayopelekwa Kwa wakulima.

Mifuko zaidi ya 700 imekutwa ndani ya ghala Hilo......

My Take; TUNA WATANZANIA WENYE FEDHA NA MADARAKA LAKINI WANA ROHO ZA KIKATILI SANA. KAMA UNAWEZA WAWEKEA WAKULIMA MCHANGA BADALA YA MBOLEA UNASHUNDWA KUFANYA UKATILI MKUBWA ZAIDI SIRINI?

MHE. RAIS UNA SAFARI NDEFU NA HAWA VIONGOZI WAKO WA CCM.....TAFUTA NAMNA YA KUWAJENGEA UZALENDO

===========

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ameagiza kukamatwa na kuhojiwa Meneja Masoko wa Kampuni ya mbolea ya Minjingu Dkt. Mshindo Msola, msimamizi wa ghala la mbolea ya Minjingu mkoa wa Njombe na Meneja wa Kanda wa Nyanda za Juu Kusini wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Michael Sanga kwa tuhuma za kukutwa na mifuko 776 ya mchanga katika ghala la kampuni ya mbolea ya Minjingu ambayo inadhaniwa huenda inatumika kuchakachua mbolea inayouzwa na kampuni hiyo.

Bashe amesema tukio hilo ni hujuma ambayo haivumiliki, ambapo atahakikisha waliohusika wanachukuliwa hatua.

Ametoa agizo hilo baada ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Njombe kwa kushirikiana na wale wa kamati ya siasa ya mkoa huo wakiongozwa na mkuu wa mkoa huo Antony Mtaka kufika katika ghala hilo na kukuta shehena ya mifuko ya mchanga katikati ya mifuko ya mbolea ya Minjingu.
Kwahiyo mbolea halisi ya minjingu ikoje?
 
Bila Rais kufuta ile kauli ya watu wale kwa urefu wa kamba zao, kila mtanzania atatafuta njia yake ya kulamba asali
Kula kwa urefu wa kamba haimaanishi kufanya uwizi na hujuma kaka hizo. Kura kwa urefu wa kamba ni kula vile unavyostahili, mfano mshahara, posho na marupurupu. Wakati wa yule katili hakukuwa na posho wala marupurupu warsha za kujengeana uwezo hazikuwepo, safari hazipo. Kulikuwa na njaa na dhiki tu.
 
Wazir wa Kilimo ameagiza Mshindo Msolwa na wafanyakazi wengine wanosimamia ghala la kuhifadhi Mbolea wakamatwwe baada ya kubainika wamehifadhi mchanga unaofhaniwa unatumika aidha kama bosheni au kuchakachua Mbolea inayopelekwa Kwa wakulima.

Mifuko zaidi ya 700 imekutwa ndani ya ghala Hilo......

My Take; TUNA WATANZANIA WENYE FEDHA NA MADARAKA LAKINI WANA ROHO ZA KIKATILI SANA. KAMA UNAWEZA WAWEKEA WAKULIMA MCHANGA BADALA YA MBOLEA UNASHUNDWA KUFANYA UKATILI MKUBWA ZAIDI SIRINI?

MHE. RAIS UNA SAFARI NDEFU NA HAWA VIONGOZI WAKO WA CCM.....TAFUTA NAMNA YA KUWAJENGEA UZALENDO

===========

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ameagiza kukamatwa na kuhojiwa Meneja Masoko wa Kampuni ya mbolea ya Minjingu Dkt. Mshindo Msola, msimamizi wa ghala la mbolea ya Minjingu mkoa wa Njombe na Meneja wa Kanda wa Nyanda za Juu Kusini wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Michael Sanga kwa tuhuma za kukutwa na mifuko 776 ya mchanga katika ghala la kampuni ya mbolea ya Minjingu ambayo inadhaniwa huenda inatumika kuchakachua mbolea inayouzwa na kampuni hiyo.

Bashe amesema tukio hilo ni hujuma ambayo haivumiliki, ambapo atahakikisha waliohusika wanachukuliwa hatua.

Ametoa agizo hilo baada ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Njombe kwa kushirikiana na wale wa kamati ya siasa ya mkoa huo wakiongozwa na mkuu wa mkoa huo Antony Mtaka kufika katika ghala hilo na kukuta shehena ya mifuko ya mchanga katikati ya mifuko ya mbolea ya Minjingu.
HAPA PANA KESI LUKUKI, HUJUMA KWA UMMA, HUJUMA KWA KIWANDA!
 
Back
Top Bottom