Waziri Hussein Bashe aagiza Mshindo Msola akamatwe

Ufisadi huu...
 
watengenezaji wa mbolea ya minjingu huu ujinga hawajaanza leo wemekuwa na skendo hii miaka mingi ila zilikuwa zinafunikwa

bashe nae mbabaishaji tu, anakomaa na mbolea za ruzuku wakati wa kulima wa tumbaku mbolea bei juu na ruzuku kwao imekuwa ndoto

mkulima wa tumbaku mbolea ananunua Tsh 177,000 wakati wengine wananunua 70,000
 
Kama hili la kuwaambia viongozi wale kwa urefu wa kamba zao kama kuna Mtanzania alilipokea kwa furaha, basi tuna safari ndefu kuyafikia maendeleo!
 
Hahaha binadamu kazi sana.
 
Haya mambo ndo tulitegemea vyombo vyetu vya dola (vikiwemo vya usalama), kushughulikia na kuyabaini mapema kabla hata raia hawajaathirika nayo, lakini kwa bahati mbaya sana, baadhi yao wameamua na wameridhika kabisa kuwa chawa wa viongozi badala ya kusimamia maslahi ya nchi na watu wake!
 
Nimeona kwenye taarifa ya habari mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka akiagizwa na Waziri wa kilimo Hussein Bashe kumkamata Rais wa zamani wa Yanga dkt Mshindo Msolla kwa kusambaza mifuko 776 ya mbolea ya minjingu iliyojaa michanga badala ya mbolea halisi.

Msolla alikuwa anatia huruma, hata hivyo ameiomba serikali imsamehe kwa hoja kuwa wafanyakazi wake ndio wamefanya uhuni huo na yuko tayari kutoa ushirikiano kwao ili wafanyakazi hao wakamatwe.

Pole sana Msolla
 
Kwahiyo mbolea halisi ya minjingu ikoje?
 
Bila Rais kufuta ile kauli ya watu wale kwa urefu wa kamba zao, kila mtanzania atatafuta njia yake ya kulamba asali
Kula kwa urefu wa kamba haimaanishi kufanya uwizi na hujuma kaka hizo. Kura kwa urefu wa kamba ni kula vile unavyostahili, mfano mshahara, posho na marupurupu. Wakati wa yule katili hakukuwa na posho wala marupurupu warsha za kujengeana uwezo hazikuwepo, safari hazipo. Kulikuwa na njaa na dhiki tu.
 
HAPA PANA KESI LUKUKI, HUJUMA KWA UMMA, HUJUMA KWA KIWANDA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…