Waziri Jaffo hao Wakurugenzi walikuwa wanasimamia uchaguzi, huo ushuru wangekusanya muda gani? Usiwafute kazi tafadhali!

Waziri Jaffo hao Wakurugenzi walikuwa wanasimamia uchaguzi, huo ushuru wangekusanya muda gani? Usiwafute kazi tafadhali!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Tunakumbushana tu waziri wa Tamisemi Mh Jaffo kwamba 2020 ulikuwa ni mwaka wa uchaguzi na hao wakurugenzi ni wasimamizi wa uchaguzi.

Kusema kwamba wasipofikisha 50% ya lengo la makusanyo ya mwaka ifikapo Devember 31 wajitathmini kama wanatosha kubaki ofisini ama uwatimue ni kuwaonea bure.

Kwa ile pressure ya uchaguzi huo ushuru wangekusanya saa ngapi?

Naomba niishie hapo.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kumbe wakurugenzi personally ndo huwa wanakusanya ushuru? Mi nilikuwa sijui hilo, nilikuwa nadhani wao ni wasimamizi!
Ama kweli: If you didn't know, now you know!
Wewe humuoni kamishna wa TRA anavyopita madukani kusaka kodi?

Kuna wakati hata waziri wa fedha hutimba kitaa kukagua.

Kusimamia ni pamoja na kufuatilia wewe mwenyewe hii ni awamu ya 5 bwashee usiishi kwa kukariri!
 
Kwa hiyo walikuwa kwenye kusimamia uchaguzi 24/7 all year long? Mkuu acha kufurahisha jamvi basi.
 
Kumbe wakurugenzi personally ndo huwa wanakusanya ushuru? Mi nilikuwa sijui hilo, nilikuwa nadhani wao ni wasimamizi!
Ama kweli: If you didn't know, now you know!
Kwa mawazo yako ni kwamba shughuli zinaweza kwenda vizuri kabisa hata mkurugenzi asipokuwepo.

Kwahiyo Basi kumbe hakuna hata umuhimu wa kuwa na wakurugenzi.

Lakini umesahau kwamba uchaguzi unapokaribia mambo hulegezwa kuwahadaa wananchi ambayo inaweza kuwa ni sababu ya kushuka makusanyo?
 
Kwanini mnawajibia,??? Waacheni wapambane na hali yao. Serikali ni system na haimaanishi ikiconcentrate kwenye kitu fulani then vingine vizorote.
 
Kwa mawazo yako ni kwamba shughuli zinaweza kwenda vizuri kabisa hata mkurugenzi asipokuwepo
Kwahiyo Basi kumbe hakuna hata umuhimu wa kuwa na wakurugenzi
Kama watu/wasomi wetu hamuwezi kujisimamia wenyewe kwa majukumu mliyokabidhiwa, mnasubiri mpaka mkurugenzi awepo kuwasimamia ndipo mambo yaende, basi tuna moral issue kubwa sana 😪😢😢
 
Kama watu/wasomi wetu hamuwezi kujisimamia wenyewe kwa majukumu mliyokabidhiwa, mnasubiri mpaka mkurugenzi awepo kuwasimamia ndipo mambo yaende, basi tuna moral issue kubwa sana 😪😢😢
Kimsingi wakurugenzi hawana kazi ya maana.Kila idara pale halmashauri,manispaa au jiji ina mtu(watu).Matumizi mabaya ya pesa,hawa wangefutwa tu (kicheo).
 
Back
Top Bottom