Waziri Jafo aagiza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tarime kusimamishwa kazi kwa kusafirisha mwili wa mtumishi juu ya carrier ya gari

gari ipo,alitakiwa awekwe ndani hapo mlango wa nyuma uende wazi,kwani mbona maiti nyingi zinasafirishwa kwa mtindo huo!!!

mambo mengine tunatetea akili mgando za watu.
 
Lengo la adhabu huwa ni kuwaonya wengine wasirudie.

Marehemu bado anayoheshima yake
 
Watu wengine mna UJINGA wa kuzaliwa nao?Au unamtetea ndugu yako aliesimamishwa kazi?Usitake dunia yote ione ujinga wako.
 
Nikosa Ila huyu waziri Kuna Mambo ya muhimu zaidi hatolei kauli.
 
Lakini pia tujiulize hilo jeneza linatosha ndani?

Ni magari mangapi yalitolewa kwenda?
 
Kwani shida iko wapi?mbona kwenye ndege wanaweka kwenye buti na spare tyre .
Huo ni mzigo kama mizigo mingine mbona.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni sawa kwenye ndege wanaweka kwenye mizigo lakini kuna sababu nzuri ya kufanya hivyo na si vinginevyo. Huku kwenye magari tunatakiwa kuonyesha utu japo kidogo basi.
 
Hivi kosa hapo nini?maana mbona mwili umewekwa kwenye sanduku

Ova
 
Asilaumiwe anaigiliza "ukatili" wa mabosi wake hasa Jiwe.
 
Kaimu Mkurugenzi kaonewa. Yeye alitoa usafiri kama taratibu za Utumishi zinavyotaka, hakuelekeza marehemu abebwe juu ya carrier.

Inawezekana watumishi wenzake ndo waliosababisha. Walitaka wakae ndani ya gari ili wamsindikize marehemu kwao.

Hao waliobeba mwili na kuuoandisha huko ndo watuambie nani aliwaamuru na kwanini.

Muhimu tujifunze tu, maisha yana thamani ukiwa hai, ukifariki huwezi kuchagua treatment ya mwili wako. Tumtafute tu Mungu, huko mbeleni inawezekana hata ukifa wakapiga tu kiberiti mchezo ukaisha bila kufikishwa kwenu.
 
Ni sawa kwenye ndege wanaweka kwenye mizigo lakini kuna sababu nzuri ya kufanya hivyo na si vinginevyo. Huku kwenye magari tunatakiwa kuonyesha utu japo kidogo basi.

Inawezekana Kaimu Mkurugenzi alilazimika kumsafirisha marehemu namna hiyo kutokana na ufinyu wa bajeti.

Labda idara husika haina magari ya kutosha kusafirisha wanafamilia pamoja na mwili wa marehemu.

Ni kweli sote tungependa mwili wa marehemu usafirishwe kwa heshima zaidi ya ilivyofanyika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…