Waziri Jafo amuondoa kwenye nafasi yake Meneja wa TARURA jijini Arusha kwa kushindwa kuita Wananchi kushuhudia ufunguzi wa barabara

Waziri Jafo amuondoa kwenye nafasi yake Meneja wa TARURA jijini Arusha kwa kushindwa kuita Wananchi kushuhudia ufunguzi wa barabara

This is the
Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo amemuondoa kwenye nafasi yake Meneja wa TARURA Jijini Arusha, Podia Mwankenja kwa kushindwa kukusanya Wananchi kushuhudia barabara zilizokamilika alizokuwa akizitembelea.

Waziri Jafo amesema, “Mnataka Serikali ionekane haijafanya kitu wakati Wananchi ndio barabara yao? Kama ni barabara ya Wananchi mbona Wananchi hawapo hapa? Au unataka Serikali ionekane haijafanya kitu katika maeneo yao?”

Waziri Jafo amemuhoji Meneja huyo ambaye pia ndio Mratibu wa barabara za Jijini humo “Kwanini hii tunazindua barabara hii Wananchi hawapo? Unataka Rais aonekane hajafanya kitu? Rais ameweka fedha hapa. Mmeficha halafu kesho na kesho kutwa mseme Rais hajafanya kitu?”

Aidha, Meneja huyo alipoanza kujitetea na kusema kuwa alidhani Mtendaji (Mkurugenzi) amefanyia kazi suala hilo, Waziri Jafo alimwambia “Wewe si barabara zako? Unafanya sabotage ili Rais aonekane hajafanya kitu halafu kesho Wananchi waseme hakuna lolote Rais amefanya?”

Waziri Jafo amemalizia “Ninyi ndio wataalamu mnaofanga Serikali ionekane haijafanya jambo wakati sisi hapa Arusha tumewekeza fedha nyingi. Mji wa Arusha tumetandaza Barabara ila wewe unaficha hata Wananchi hapa jirani wasijue tumeweka barabara”

View attachment 1502024
This is the highest degree of stupidity na ni uonevu wa watumishi wa kiwango cha juu kabisa kuwai kutokea.
Bado natafakari kama nilichokiona hapa ni kweli kimetokea nchi ya Tanzania. Nchi inayojisifu kuwa nchi ambayo haina ubaguzi wa rangi, vyama na makabila. Nchi ambayo kiongozi wake muda wote akienda kanisani anashikaga mike na kusema kuwa nchi ya Tanzania tumtangulize Mungu.

Nasema tena huu ni uonevu wa kiwango cha juu kabisa niliowai kuushuhudia hapa Tanzania.
 
Chuga mji wa wagumu.
hawashobokei mambo ya kijinga, eti kukusanyana kisa mtu anazindua barabara...kwa Arusha wakija na mtindo wa namna hio mbona watafukuzana sana?
 
Amemfukuza mtu kazi kwa sababu za hovyo kabisa nilikua namkubali Jafo kwa hilo hapana watu bara bara Arusha si wanaziona na ishu ya sasa hivi utamwita nani aangalie bara bara wakati ana shughuli za kufanya na serikali ni kazi yake kujenga bara bara...yaani hao tarura walivyo busy na hizo bara bara harafu unamtimua mtu bila sababu sio kabisa...labda kama alikua anamtafutia sababu lakini sio hiyo ya wananchi....
 
Arusha kwenda kumshangaa kiongozi wa Ccm hadi wakusanywe. Tena kwa kupewa hela.
Sasa huyu meneja ange andikia fungu gani?
 
uonevu uliopitiliza jamani duu magufuri aingilie kati
Hahah kwani unadhani wakina Jaffo wanafanya hivyo kumridhisha nani?Mbona enzi za kina JK&Mkapa yalikua hayafanyiki haya?Au barabara zilikua hazizinduliwi.
 
Hah hah Mh. Jafo hasira za nini ?

Tuliwaambia wananchi wanataka Maendeleo ya Watu siyo Maendeleo ya Vitu.

Ona sasa CCM Mpya wananchi hawaonekani wamekwenda kutafuta Maendeleo (Watu) yao hawana muda wa kushangaa vitu wakati muda huo ni wa kutafuta fedha wajiendeleze .
 
Du hii kali ya mwaka yaan afisa wa TARURA afanye public advertisement kuwaalika wananchi kuja kuangalia barabara ilivyojengwa? Kweli siasa za Tanzania ni maji taka tena yanayotoka Kwenye chemba ya choo. Jafo hapo umebugi sana pia umetumia madaraka vibaya sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wananchi hawa wasioishi wala kutumia Maendeleo ya Vitu mfano wa ma flyovers , bombadier ndege, Stendi Mpya Kubwa za Mabasi kama Dodoma n.k hata mjaribu vipi kuwalazimishe waone kazi hizi za CCM Mpya zisizo na mahusiano na shughuli zao za Maendeleo ya Watu ni sawa na kumpigia gitaa mbuzi.
 
Hapo hakuna hoja, waziri kateleza. Mhandisi kafanya sehemu yake, kasimamia barabara kwa ubora na kiwango kinachotakiwa.
Ingekuwa kazi yake haikufanyika kwa kiwango, hapo angekuwa na sababu ya kutoa adhabu.
Lakini kwa hilo, wala mhandisi asihofu.
 
uonevu mkubwa sana huu,unaweza kumrukia mtu kichwa ukafungwe.
sijui jamaa ataiangaliaje familia yake leo.halafu kijamaa kinachofoka kakizidi umri
 
Back
Top Bottom