Kabisa ila sababu ni za kijinga sanaJafo namkubali ila sababu alizotoa kwa meneja wa TARURA ni za kijinga na kishamba kupindukia.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kabisa ila sababu ni za kijinga sanaJafo namkubali ila sababu alizotoa kwa meneja wa TARURA ni za kijinga na kishamba kupindukia.
Kuna hawataki lami, ni sahani ya wali maharage na kanga ya kijani inatosha.Waende kanda ya ziwa, ndiyo kuna makondoo mengi na mazuzu ya kumwaga.
Hapo hakuna hoja, waziri kateleza. Mhandisi kafanya sehemu yake, kasimamia barabara kwa ubora na kiwango kinachotakiwa.
Ingekuwa kazi yake haikufanyika kwa kiwango, hapo angekuwa na sababu ya kutoa adhabu.
Lakini kwa hilo, wala mhandisi asihofu.
Nilitegemea kama mwanasiasa unayetetea CCM humu jamvini ungepinga vikali jambo alilolifanya jaffo.Anyway huyo manager hajui maana ya team work ilibidi awasiliane na viongozi wenzie kuhusu ujio wa waziri na kuwaalika rasmi kwenye uzinduzi na kuomba magari ya matangazo yazunguke mjini kutangaza uzinduzi nk
Vyeo vyote vya uteuzi ni vya kisiasa sababu raisi mfano huzunguka nchi nzima jua lake mvua yake mbu wake,VUMBI LAKE ,TOPE LAKE kutafuta kura kwa wananchi wakati hao watendaji huwa wako majumbani mwao wanakula viyoyozi kwenye ofisi na magari yenye VIYOYOZI
Raisi ambaye ni mwanasiasa akishaumia kwa yote hayo anasema ninakuteua ushike nafasi fulani halafu unaanza kujitia ohh mimi sio mwanasiasa sisikilizi wanasiasa huyo aliyekuteua ni nani? Akakufanya unakaa jumba kubwa yenye viyoyozi na gari yenye kiyoyozi .Bila huyo mwanasiasa ungekuwa hapo ulipo? TARURA yenyewe ilianzishwa na wanasiasa kwa sheria ya bunge iliyopitishwa na wanasiasa.Bila wanasiasa mtu angekuwa meneja wa TARURA?
Wanasiasa waweza hata kesho wakaamua kuifuta TARURA yeye atakuwa meneja wa wapi? Wanasiasa ndio wanawaweka mjini hao wanaojiita wataalamu watendaji.Wanatakiwa kuwa na adabu ya hali ya juu kwa wanasiasa
Sera za nchi huanzia kwenye chama tawala kwenye ilani ya chama tawala ndipo hupelekwa kwenye serikali kupitia wizara yake ya uchumi na mipango haziibuki tu hewani kuanzia kwa watendaji huanzia kwenye chama tawalaKwa iyo vyombo vya serikali vibaanzishwa kwa utashi wa wanasiasa na si sera na mikakati ya kitaifa???
Kweli nimekudharau sana we mtu.
Hili ni ingizo bovu kabisa la mwezi Juni! Kajifunze hata kwa Pierre Liquid utakuwa na afadhali.Meneja ana wajibu wa kuhakikisha anamkumbusha MKURUGENZI AANDAE uwepo huo wa watu....
MKURUGENZI naye Ana MAKOSA kwa sababu yeye ndiye mtendaji na msimamizi mkuu wa shughuli za MAENDELEO....
Think thrice
Kwahiyo hiyo bara bara amejenga Rais kwa kutumia pesa zake?Mimi nadhani ni Sawa tu,
Maana yake halisi ni Sawa na Baba kujenga nyumba ya pili Halafu asiimbie familia yake kuwa amejenga nyumba nyingine mahali, Halafu akaweka wapangaji wasijue hata familia yake
Msikitini na kazi za wananchi wapi na wapi mkuu!!Kwahiyo hiyo bara bara amejenga Rais kwa kutumia pesa zake?
Hao wananchi wana akili maana wanajua kodi zao ndiyo zimefanikisha ayo.Jafo ,hivi nae anaenda Msikitini?
Ndo umejifunza wapi hayo???Sera za nchi huanzia kwenye chama tawala kwenye ilani ya chama tawala ndipo hupelekwa kwenye serikali kupitia wizara yake ya uchumi na mipango haziibuki tu hewani kuanzia kwa watendaji huanzia kwenye chama tawala
Ukiona ndege zinanunuliwa sio ubunifu wa AIR tanzania ni wa wanasiasa kupia ilani kuwa tutafufua usafiri wa anga serikali baada ya kushika ndio inatekeleza nk
Watu walikuwa makazini leo siku ya kazi. Viongozi kufungua barabara ni kazi yao wamelipwa mshahara kwa kodi za wananchi ili waifanye
Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo amemuondoa kwenye nafasi yake Meneja wa TARURA Jijini Arusha, Podia Mwankenja kwa kushindwa kukusanya Wananchi kushuhudia barabara zilizokamilika alizokuwa akizitembelea.
Waziri Jafo amesema, “Mnataka Serikali ionekane haijafanya kitu wakati Wananchi ndio barabara yao? Kama ni barabara ya Wananchi mbona Wananchi hawapo hapa? Au unataka Serikali ionekane haijafanya kitu katika maeneo yao?”
Waziri Jafo amemuhoji Meneja huyo ambaye pia ndio Mratibu wa barabara za Jijini humo “Kwanini hii tunazindua barabara hii Wananchi hawapo? Unataka Rais aonekane hajafanya kitu? Rais ameweka fedha hapa. Mmeficha halafu kesho na kesho kutwa mseme Rais hajafanya kitu?”
Aidha, Meneja huyo alipoanza kujitetea na kusema kuwa alidhani Mtendaji (Mkurugenzi) amefanyia kazi suala hilo, Waziri Jafo alimwambia “Wewe si barabara zako? Unafanya sabotage ili Rais aonekane hajafanya kitu halafu kesho Wananchi waseme hakuna lolote Rais amefanya?”
Waziri Jafo amemalizia “Ninyi ndio wataalamu mnaofanga Serikali ionekane haijafanya jambo wakati sisi hapa Arusha tumewekeza fedha nyingi. Mji wa Arusha tumetandaza Barabara ila wewe unaficha hata Wananchi hapa jirani wasijue tumeweka barabara”
Wananchi walikuwa makazini, hawahitaji kukusanywa kupewa mahesabu ya pesa zao. Huyo jafo angetumia mic ya hao waandishi wa habari kuwatangazia watu mahesabu ya pesa badala ya kuwaambia meneja kufukuzwa.Msikitini na kazi za wananchi wapi na wapi mkuu!!
Ni pesa za wananchi na ndiyo maana ilipaswa wakusanywe waambiwe zimetukuka pesa zao kiasi gani kujenga barabara yao
Ina maana wananchi hiyo bara bara wameiona leo?Msikitini na kazi za wananchi wapi na wapi mkuu!!
Ni pesa za wananchi na ndiyo maana ilipaswa wakusanywe waambiwe zimetukuka pesa zao kiasi gani kujenga barabara yao
Yaan.wamesahau kabisa kwamba watu wanalipa kodi. Amewekeza hela kazitoa wapi?Eti "rais amewekeza pesa hapa alafu unafanya sabotage wananchi wajue rais hajafanya kitu"
Kwa kweli Jafo nyungu zimemlevya.
Anatekeleza majukumu yakeJafo namkubali ila sababu alizotoa kwa meneja wa TARURA ni za kijinga na kishamba kupindukia.