Waziri Jafo amuondoa kwenye nafasi yake Meneja wa TARURA jijini Arusha kwa kushindwa kuita Wananchi kushuhudia ufunguzi wa barabara

Waziri Jafo amuondoa kwenye nafasi yake Meneja wa TARURA jijini Arusha kwa kushindwa kuita Wananchi kushuhudia ufunguzi wa barabara

Leo ndo nimeamini ccm haikubaliki.. kumbe msipowakusanya wananchi hawaji?
 
Hapo hakuna hoja, waziri kateleza. Mhandisi kafanya sehemu yake, kasimamia barabara kwa ubora na kiwango kinachotakiwa.
Ingekuwa kazi yake haikufanyika kwa kiwango, hapo angekuwa na sababu ya kutoa adhabu.
Lakini kwa hilo, wala mhandisi asihofu.

Anyway huyo manager hajui maana ya team work ilibidi awasiliane na viongozi wenzie kuhusu ujio wa waziri na kuwaalika rasmi kwenye uzinduzi na kuomba magari ya matangazo yazunguke mjini kutangaza uzinduzi nk

Vyeo vyote vya uteuzi ni vya kisiasa sababu raisi mfano huzunguka nchi nzima jua lake mvua yake mbu wake,VUMBI LAKE ,TOPE LAKE kutafuta kura kwa wananchi wakati hao watendaji huwa wako majumbani mwao wanakula viyoyozi kwenye ofisi na magari yenye VIYOYOZI

Raisi ambaye ni mwanasiasa akishaumia kwa yote hayo anasema ninakuteua ushike nafasi fulani halafu unaanza kujitia ohh mimi sio mwanasiasa sisikilizi wanasiasa huyo aliyekuteua ni nani? Akakufanya unakaa jumba kubwa yenye viyoyozi na gari yenye kiyoyozi .Bila huyo mwanasiasa ungekuwa hapo ulipo? TARURA yenyewe ilianzishwa na wanasiasa kwa sheria ya bunge iliyopitishwa na wanasiasa.Bila wanasiasa mtu angekuwa meneja wa TARURA?

Wanasiasa waweza hata kesho wakaamua kuifuta TARURA yeye atakuwa meneja wa wapi? Wanasiasa ndio wanawaweka mjini hao wanaojiita wataalamu watendaji.Wanatakiwa kuwa na adabu ya hali ya juu kwa wanasiasa
 
Meneja ameshindwa kusoma alama za nyakati
Arusha ni mji wa kimkakati,ni kosa kubwa sana kushindwa kuhamasisha wananchi wajitokeze kwenye uzinduzi
 
Anyway huyo manager hajui maana ya team work ilibidi awasiliane na viongozi wenzie kuhusu ujio wa waziri na kuwaalika rasmi kwenye uzinduzi na kuomba magari ya matangazo yazunguke mjini kutangaza uzinduzi nk

Vyeo vyote vya uteuzi ni vya kisiasa sababu raisi mfano huzunguka nchi nzima jua lake mvua yake mbu wake,VUMBI LAKE ,TOPE LAKE kutafuta kura kwa wananchi wakati hao watendaji huwa wako majumbani mwao wanakula viyoyozi kwenye ofisi na magari yenye VIYOYOZI

Raisi ambaye ni mwanasiasa akishaumia kwa yote hayo anasema ninakuteua ushike nafasi fulani halafu unaanza kujitia ohh mimi sio mwanasiasa sisikilizi wanasiasa huyo aliyekuteua ni nani? Akakufanya unakaa jumba kubwa yenye viyoyozi na gari yenye kiyoyozi .Bila huyo mwanasiasa ungekuwa hapo ulipo? TARURA yenyewe ilianzishwa na wanasiasa kwa sheria ya bunge iliyopitishwa na wanasiasa.Bila wanasiasa mtu angekuwa meneja wa TARURA?

Wanasiasa waweza hata kesho wakaamua kuifuta TARURA yeye atakuwa meneja wa wapi? Wanasiasa ndio wanawaweka mjini hao wanaojiita wataalamu watendaji.Wanatakiwa kuwa na adabu ya hali ya juu kwa wanasiasa
Nilitegemea kama mwanasiasa unayetetea CCM humu jamvini ungepinga vikali jambo alilolifanya jaffo.

utetezi mfu unaozidi kuutoa humu dhidi ya tabia chafu ya ubaguzi na uonevu wa wazi alioufanya waziri wa chama chako unaonesha si tu CCM mmekosa uhalali wa kuongoza hii nchi bali hamfai kabisa kuongoza hii nchi.

Kwa iyo vyombo vya serikali vibaanzishwa kwa utashi wa wanasiasa na si sera na mikakati ya kitaifa???

Kweli nimekudharau sana we mtu.
 
Kwa iyo vyombo vya serikali vibaanzishwa kwa utashi wa wanasiasa na si sera na mikakati ya kitaifa???

Kweli nimekudharau sana we mtu.
Sera za nchi huanzia kwenye chama tawala kwenye ilani ya chama tawala ndipo hupelekwa kwenye serikali kupitia wizara yake ya uchumi na mipango haziibuki tu hewani kuanzia kwa watendaji huanzia kwenye chama tawala

Ukiona ndege zinanunuliwa sio ubunifu wa AIR tanzania ni wa wanasiasa kupia ilani kuwa tutafufua usafiri wa anga serikali baada ya kushika ndio inatekeleza nk
 
Meneja ana wajibu wa kuhakikisha anamkumbusha MKURUGENZI AANDAE uwepo huo wa watu....

MKURUGENZI naye Ana MAKOSA kwa sababu yeye ndiye mtendaji na msimamizi mkuu wa shughuli za MAENDELEO....

Think thrice
Hili ni ingizo bovu kabisa la mwezi Juni! Kajifunze hata kwa Pierre Liquid utakuwa na afadhali.
 
Mimi nadhani ni Sawa tu,

Maana yake halisi ni Sawa na Baba kujenga nyumba ya pili Halafu asiimbie familia yake kuwa amejenga nyumba nyingine mahali, Halafu akaweka wapangaji wasijue hata familia yake
Kwahiyo hiyo bara bara amejenga Rais kwa kutumia pesa zake?
Hao wananchi wana akili maana wanajua kodi zao ndiyo zimefanikisha ayo.Jafo ,hivi nae anaenda Msikitini?
 
Kwahiyo hiyo bara bara amejenga Rais kwa kutumia pesa zake?
Hao wananchi wana akili maana wanajua kodi zao ndiyo zimefanikisha ayo.Jafo ,hivi nae anaenda Msikitini?
Msikitini na kazi za wananchi wapi na wapi mkuu!!

Ni pesa za wananchi na ndiyo maana ilipaswa wakusanywe waambiwe zimetukuka pesa zao kiasi gani kujenga barabara yao
 
🤣🤣🤣🤣🤣 wameficha!
Hao wananchi waache shughuli za maendeleo wakaee wakiaangalia barabara. Ntaona anaakili kama akitoa na mikataba wananchi waihakikishe.
 
Sera za nchi huanzia kwenye chama tawala kwenye ilani ya chama tawala ndipo hupelekwa kwenye serikali kupitia wizara yake ya uchumi na mipango haziibuki tu hewani kuanzia kwa watendaji huanzia kwenye chama tawala

Ukiona ndege zinanunuliwa sio ubunifu wa AIR tanzania ni wa wanasiasa kupia ilani kuwa tutafufua usafiri wa anga serikali baada ya kushika ndio inatekeleza nk
Ndo umejifunza wapi hayo???

Hivi ulikuwa unajua kazi ya tume ya mipango?? Unajua pia kuwa saivi imeamishiwa wizara ya fedha??! Unajua wanafanyaga nini??!!

Unajua taasisi za Serikali nazo huwa zinakuwaga na mipango yao??? Kuanzia miaka 5 hadi kumi????

Kweli CCM mna vilaza. Acha tu mwenyekiti wenu achukue vijana Chadema
 
Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo amemuondoa kwenye nafasi yake Meneja wa TARURA Jijini Arusha, Podia Mwankenja kwa kushindwa kukusanya Wananchi kushuhudia barabara zilizokamilika alizokuwa akizitembelea.

Waziri Jafo amesema, “Mnataka Serikali ionekane haijafanya kitu wakati Wananchi ndio barabara yao? Kama ni barabara ya Wananchi mbona Wananchi hawapo hapa? Au unataka Serikali ionekane haijafanya kitu katika maeneo yao?”

Waziri Jafo amemuhoji Meneja huyo ambaye pia ndio Mratibu wa barabara za Jijini humo “Kwanini hii tunazindua barabara hii Wananchi hawapo? Unataka Rais aonekane hajafanya kitu? Rais ameweka fedha hapa. Mmeficha halafu kesho na kesho kutwa mseme Rais hajafanya kitu?”

Aidha, Meneja huyo alipoanza kujitetea na kusema kuwa alidhani Mtendaji (Mkurugenzi) amefanyia kazi suala hilo, Waziri Jafo alimwambia “Wewe si barabara zako? Unafanya sabotage ili Rais aonekane hajafanya kitu halafu kesho Wananchi waseme hakuna lolote Rais amefanya?”

Waziri Jafo amemalizia “Ninyi ndio wataalamu mnaofanga Serikali ionekane haijafanya jambo wakati sisi hapa Arusha tumewekeza fedha nyingi. Mji wa Arusha tumetandaza Barabara ila wewe unaficha hata Wananchi hapa jirani wasijue tumeweka barabara”

Watu walikuwa makazini leo siku ya kazi. Viongozi kufungua barabara ni kazi yao wamelipwa mshahara kwa kodi za wananchi ili waifanye
 
Msikitini na kazi za wananchi wapi na wapi mkuu!!

Ni pesa za wananchi na ndiyo maana ilipaswa wakusanywe waambiwe zimetukuka pesa zao kiasi gani kujenga barabara yao
Wananchi walikuwa makazini, hawahitaji kukusanywa kupewa mahesabu ya pesa zao. Huyo jafo angetumia mic ya hao waandishi wa habari kuwatangazia watu mahesabu ya pesa badala ya kuwaambia meneja kufukuzwa.
 
Msikitini na kazi za wananchi wapi na wapi mkuu!!

Ni pesa za wananchi na ndiyo maana ilipaswa wakusanywe waambiwe zimetukuka pesa zao kiasi gani kujenga barabara yao
Ina maana wananchi hiyo bara bara wameiona leo?
Ina maana wakati wa ujenzi wananchi walikua wamehama apo?
Mwisho,Jafo amesema bara bara kajenga Rais wewe unasema wananchi,Nani ni mkweli?
Hivi ,Jafo anaenda Msikitini?
 
Back
Top Bottom