Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Naamini walionewa ni wengi tu, na hiyo inatokana na hulka ya Bosi wao na wao sasa wanamuiga.Kwa kweli amemuonea sana sioni kosa lake
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naamini walionewa ni wengi tu, na hiyo inatokana na hulka ya Bosi wao na wao sasa wanamuiga.Kwa kweli amemuonea sana sioni kosa lake
Hii nchi ilipofika ili mambo yakae sawa inabidi CCM itoke kwa gharama yeyote ile. Huu uonevu si wa kawaida kwa kweli. Unatisha. Kutoka kuwa Chama cha kutetea wafanyakazi hadi kuwa Chama cha kukandamiza wafanyakazi.Akafungue nyingine aone kama sisi wananchi tutakuja.Kwanza tutakuja kufanya nini saa za kazi.Ni kweli huu ni ukatili na uonevu mbaya.Taratibu za kumsimamisha kazi mtumishi wa umma Tanzania jamani ziko wapi? Sasa hivi ni kufukuzana kazi tu bila kujali utu wa mtumishi wa Umma.
Wizara ya kazi Utumishi,mko wapi,mtumishi huyu ana haki zote za utumishi kama alivyo waziri.Kama kakosea,kuna utaratibu wa kufuata ambao Serikali ya Mh.Dr.Mwal.Julius Kambarage Nyerere aliheshimu na kuufuata kwa nguvu zake zote lakini leo hii ni ubabe tu.Hii ni Tanzania ya wapi,Uonevu mtupu.
Kwanza tunashangaa sana kilichotokea,barabara ni kodi zetu,ni haki yetu kuwa na barabara nzuri,tumeshazitumia zote,unataka tuje kuimbia barabara iliyotengenezwa kwa kodi zetu ili iweje.Uonevu huu hata Mungu hapendi.
Huyu meneja sio mwanasiasa,yeye ni mtaalamu.Kazi ya kutuita sisi wananchi sio yake.Hii ni kazi ya balozi wa nyumba kumi akishirikiana na mwenyekiti wa mtaa.Na hata kama angekuja kutuita tuone barabara ikifunguliwa tungemuuliza,kwani ilifungwa lini.Siku zote si ipo tu.Labda ifungwe kwanza kwa miezi kadhaa,halafu ije ifunguliwe ndo watuambie tukaone ile iliyofungwa inafunguliwa tungewaelewa kidogo.Lakini barabara tunapita kila siku leo corona imetuachia umaskini tuache kutafuta ada ya mtoto ya shule tuje? kuona barabara za lami.Inasikitisha sana sana.Tenda haki ili taifa liinuke.Haki huinua taifa.
Haiwezekani jamaa akafanye kazi ya kukusanya wanachi ili hali yeye kaajiriwa kwa taaaluma sio kisiasaNaamini walionewa ni wengi tu, na hiyo inatokana na hulka ya Bosi wao na wao sasa wanamuiga.
Ndio ukitaka kuwa bingwa wa mipango ya taifa wala usiumize kichwa shika tu ilani ya chama tawala na sera zake soma wanataka nini chukua lile linalokuhusuKwa iyo kwa akili yako unadhani tume ya mipango inasubirigi ilani ya Chama na ndo inapanga mipango???
mbona wakulima walisharuhusiwa siku nyingi kuuza popote ndani ya nchi na nje ya nchi wewe sio mkulima ungekuwa mkulima ungelijua hilo ilisharuhusiwa siku nyingi kauze popoteKaribu Ruvuma tufanye kilimo ingawa sera za Chama chako kimenifanya nikose hela kwa kuzuia mahindi kuuzwa nje.
Ukiona hivyo,uje ndio utaratibu uliopo wa kutumia rasilimali zilizoko serikalini kukibeba chama fulani cha siasa, sasa huenda huyo Meneja hakufanya aliyotakwa kufanya.Haiwezekani jamaa akafanye kazi ya kukusanya wanachi ili hali yeye kaajiriwa kwa taaaluma sio kisiasa
Usiku mwema kwa mara nyingine tena comradeNdio ukitaka kuwa bingwa wa mipango ya taifa wala usiumize kichwa shika tu ilani ya chama tawala na sera zake soma wanataka nini chukua lile linalokuhusu
mfano ilani ya 2015 hadi 2020 ilisema kuwa itahakikisha inarasimisha ardhi na kuondoa rushwa kwenye
kwa hiyo ukiwa unapanga mipango ya taifa unatakiwa moja ya mambo kujielekeza kwenye land use na planning na urahisi wa kupata hati nk na kubana mianya ya rushwa
ILANI pia inatamka kuhusu kuongezeka matumizi ya teknolojia kwa hiyo mipango inatakiwa ijielekeze huko pia kuhusu utumiaji wa teknolojia kila eneo mfano la mapato ya serikali nk
ilani inatamka kuhusu miundombinu na huduma za jamii kuwafikia watu wengi zaidi hivyo mpanga mipango ya taifa huanzia hapo wa afya ,wa elimu,Tanroads,TARURA nk kila mtu kwenye eneo lake anapanga kufikia hilo linatakiwa na chama tawala nk
MPANGA mipango ya Taifa usipokuwa na ilani utaishia kujitungia vitu ambavyo vikienda bungeni waziri wa fedha aki present vitapigwa chini na wabunge sababu haviko kwenye ilani ya chama chao!!! na utatutumbuliwa kwa kujijia na vyako vya kujitungia chumbani!!
lazima mipango yote i allign na ilani na sera za chama tawala
Huwa wanasema wananchi wamesimamisha msafara kumbe wamewakusanya wenyeweKama unajua unajua tu,hauhitaji kujieleza sana watu wenyewe wataona tu
Mfano hauhakisi kabisa na uhalisia....hao wananchi hyo barabara wangeiona tu,mbona zamani hakukuwa na haya mambo, shida ya hii awamu wanapenda sifa Yani that is the problem hio sababu ni za kitoto sana mi nikajua meneja kaiba hela za barabara haijakamilikaMimi nadhani ni Sawa tu,
Maana yake halisi ni Sawa na Baba kujenga nyumba ya pili Halafu asiimbie familia yake kuwa amejenga nyumba nyingine mahali, Halafu akaweka wapangaji wasijue hata familia yake
Swali watu wakialikwa na wasipohudhuria uzinduzi haufanyiki?Yuko sahihi na alichoongea kizito sana
Uzinduzi wa barabara wananchi wengi wanatakiwa kuhudhuria mfano mialiko ilitakiwa iende kwa wadau wa barabara mfano umoja wa wenye mabasi,magari ya mizigo , daladala,boboda,waananchi ambao hizo barabara zinapita ambao walifaidi ajira ,kuuzia vyakula vibarua ,wajenzi nk ,makondractor ,wafanyabiashara wa maeneo hayo barabara inapita wakiwemo wa vituo vua mafuta vilivyoko hayo maeneo walio supply mafuta na watakaofaidi uwepo nk ambao wengine walifaidika kwa kuuza vifaa mbalimbali kwenye mradi
Pia viongozi wa maeneo barabara inapita mfano wajumbe wa nyumba kumi,madiwani,wabunge ,viongozi wa serikali za mitaa,viongozi wa dini nk
Viongozi wa vyama na serikali na mashirika ya umma kama TRA ambako hukusanya kodi , taasisi za kijamii
Uzinduzi maana yake ni kukabidhi mradi kwa wananchi kuwa kodi zenu jamani hizo hapo na kazi mlitupa kwa kodi zenu hiyo.Sasa waziri hawezi kabidhi barabara kwa meneja wa Tarura anakabidhi kwa wananchi
Hilo tukio ni la TARURA lakini alitakiwa kushiriksha wadau mbalimbali .Ahakikishe wadau wakabidhiwa wapo
Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo amemuondoa kwenye nafasi yake Meneja wa TARURA Jijini Arusha, Podia Mwankenja kwa kushindwa kukusanya Wananchi kushuhudia barabara zilizokamilika alizokuwa akizitembelea.
Waziri Jafo amesema, “Mnataka Serikali ionekane haijafanya kitu wakati Wananchi ndio barabara yao? Kama ni barabara ya Wananchi mbona Wananchi hawapo hapa? Au unataka Serikali ionekane haijafanya kitu katika maeneo yao?”
Waziri Jafo amemuhoji Meneja huyo ambaye pia ndio Mratibu wa barabara za Jijini humo “Kwanini hii tunazindua barabara hii Wananchi hawapo? Unataka Rais aonekane hajafanya kitu? Rais ameweka fedha hapa. Mmeficha halafu kesho na kesho kutwa mseme Rais hajafanya kitu?”
Aidha, Meneja huyo alipoanza kujitetea na kusema kuwa alidhani Mtendaji (Mkurugenzi) amefanyia kazi suala hilo, Waziri Jafo alimwambia “Wewe si barabara zako? Unafanya sabotage ili Rais aonekane hajafanya kitu halafu kesho Wananchi waseme hakuna lolote Rais amefanya?”
Waziri Jafo amemalizia “Ninyi ndio wataalamu mnaofanga Serikali ionekane haijafanya jambo wakati sisi hapa Arusha tumewekeza fedha nyingi. Mji wa Arusha tumetandaza Barabara ila wewe unaficha hata Wananchi hapa jirani wasijue tumeweka barabara”
Jafo nampenda lakini hapo kakosea. Watu wa Arusha ni tofauti serikali kwao ni kazi yake kujenga hawawezi kukusanyika tu kuangalia barabara badala ya kufanya biashara zao ndogondogo, au kutafuta watalii mtaani, n.k ni mji wa wahangaikaji hakuna magenge kama ya Dar..