Waziri Jafo amuondoa kwenye nafasi yake Meneja wa TARURA jijini Arusha kwa kushindwa kuita Wananchi kushuhudia ufunguzi wa barabara

Waziri Jafo amuondoa kwenye nafasi yake Meneja wa TARURA jijini Arusha kwa kushindwa kuita Wananchi kushuhudia ufunguzi wa barabara

Akafungue nyingine aone kama sisi wananchi tutakuja.Kwanza tutakuja kufanya nini saa za kazi.Ni kweli huu ni ukatili na uonevu mbaya.Taratibu za kumsimamisha kazi mtumishi wa umma Tanzania jamani ziko wapi? Sasa hivi ni kufukuzana kazi tu bila kujali utu wa mtumishi wa Umma.

Wizara ya kazi Utumishi,mko wapi,mtumishi huyu ana haki zote za utumishi kama alivyo waziri.Kama kakosea,kuna utaratibu wa kufuata ambao Serikali ya Mh.Dr.Mwal.Julius Kambarage Nyerere aliheshimu na kuufuata kwa nguvu zake zote lakini leo hii ni ubabe tu.Hii ni Tanzania ya wapi,Uonevu mtupu.

Kwanza tunashangaa sana kilichotokea,barabara ni kodi zetu,ni haki yetu kuwa na barabara nzuri,tumeshazitumia zote,unataka tuje kuimbia barabara iliyotengenezwa kwa kodi zetu ili iweje.Uonevu huu hata Mungu hapendi.

Huyu meneja sio mwanasiasa,yeye ni mtaalamu.Kazi ya kutuita sisi wananchi sio yake.Hii ni kazi ya balozi wa nyumba kumi akishirikiana na mwenyekiti wa mtaa.Na hata kama angekuja kutuita tuone barabara ikifunguliwa tungemuuliza,kwani ilifungwa lini.Siku zote si ipo tu.Labda ifungwe kwanza kwa miezi kadhaa,halafu ije ifunguliwe ndo watuambie tukaone ile iliyofungwa inafunguliwa tungewaelewa kidogo.Lakini barabara tunapita kila siku leo corona imetuachia umaskini tuache kutafuta ada ya mtoto ya shule tuje? kuona barabara za lami.Inasikitisha sana sana.Tenda haki ili taifa liinuke.Haki huinua taifa.
Hii nchi ilipofika ili mambo yakae sawa inabidi CCM itoke kwa gharama yeyote ile. Huu uonevu si wa kawaida kwa kweli. Unatisha. Kutoka kuwa Chama cha kutetea wafanyakazi hadi kuwa Chama cha kukandamiza wafanyakazi.

Chadema tunaitaji nguvu ya umma kwenye kulinda kura na kuhesabu kura. Haya ni zaidi aliyofanya mkoloni miaka ya 1950
 
Kwa iyo kwa akili yako unadhani tume ya mipango inasubirigi ilani ya Chama na ndo inapanga mipango???
Ndio ukitaka kuwa bingwa wa mipango ya taifa wala usiumize kichwa shika tu ilani ya chama tawala na sera zake soma wanataka nini chukua lile linalokuhusu

Mfano ilani ya 2015 hadi 2020 ilisema kuwa itahakikisha inarasimisha ardhi na kuondoa rushwa kwenye upatikanaji huduma mbalimbali

Kwa hiyo ukiwa unapanga mipango ya taifa unatakiwa moja ya mambo kujielekeza kwenye land use na planning na urahisi wa kupata hati nk na kubana mianya ya rushwa

ILANI pia inatamka kuhusu kuongezeka matumizi ya teknolojia kwa hiyo mipango inatakiwa ijielekeze huko pia kuhusu utumiaji wa teknolojia kila eneo mfano la mapato ya serikali nk

ilani inatamka kuhusu miundombinu na huduma za jamii kuwafikia watu wengi zaidi hivyo mpanga mipango ya taifa huanzia hapo wa afya ,wa elimu,Tanroads,TARURA nk kila mtu kwenye eneo lake anapanga kufikia hilo linatakiwa na chama tawala nk

MPANGA mipango ya Taifa usipokuwa na ilani utaishia kujitungia vitu ambavyo vikienda bungeni waziri wa fedha aki present vitapigwa chini na wabunge sababu haviko kwenye ilani ya chama chao!!! na utatutumbuliwa kwa kujijia na vyako vya kujitungia chumbani!!

Lazima sio hiari mipango yote ya taifa inayopangwa lazima i allign na ilani na sera za chama tawala
 
Kama wanapenda vigelegele kitu kilichowawasha kumtoa mpiga debe wao (mkuu wa mkoa) ambae angewaandalia umati mkubwa wa kupigia makofi porojo zao kilikuwa nini.

Si yalikuwa maamuzi yao kupeleka watendaji ambao sio wana siasa sasa watu ambao awajazoea kulamba miguu na kujipendekeza utawalaumu vipi usipokuta umati wa kukupigia makofi.

The whole thing is pathetic; ukitaka umati hadi kwenye ufunguzi wa dampo weka Mkuu mkoa mwanasiasa hao ndio wanafahamu mambo ya fitna za siasa.
 
Karibu Ruvuma tufanye kilimo ingawa sera za Chama chako kimenifanya nikose hela kwa kuzuia mahindi kuuzwa nje.
mbona wakulima walisharuhusiwa siku nyingi kuuza popote ndani ya nchi na nje ya nchi wewe sio mkulima ungekuwa mkulima ungelijua hilo ilisharuhusiwa siku nyingi kauze popote
 
Jafo leo amepotea kama Liverpool na Manchester city,

Meneja ameonewa sana.
 
Kwa uonevu niliouona Leo na ubaguzi wa waziwazi kabisa, sidhani kama kuna mtumishi anayejielewa ataibeba CCM mwaka huu, si kwa kuipigia kura au kuifanyia fitna ishinde uchaguzi mwaka huu.
 
Haiwezekani jamaa akafanye kazi ya kukusanya wanachi ili hali yeye kaajiriwa kwa taaaluma sio kisiasa
Ukiona hivyo,uje ndio utaratibu uliopo wa kutumia rasilimali zilizoko serikalini kukibeba chama fulani cha siasa, sasa huenda huyo Meneja hakufanya aliyotakwa kufanya.
 
Ndio ukitaka kuwa bingwa wa mipango ya taifa wala usiumize kichwa shika tu ilani ya chama tawala na sera zake soma wanataka nini chukua lile linalokuhusu

mfano ilani ya 2015 hadi 2020 ilisema kuwa itahakikisha inarasimisha ardhi na kuondoa rushwa kwenye

kwa hiyo ukiwa unapanga mipango ya taifa unatakiwa moja ya mambo kujielekeza kwenye land use na planning na urahisi wa kupata hati nk na kubana mianya ya rushwa

ILANI pia inatamka kuhusu kuongezeka matumizi ya teknolojia kwa hiyo mipango inatakiwa ijielekeze huko pia kuhusu utumiaji wa teknolojia kila eneo mfano la mapato ya serikali nk

ilani inatamka kuhusu miundombinu na huduma za jamii kuwafikia watu wengi zaidi hivyo mpanga mipango ya taifa huanzia hapo wa afya ,wa elimu,Tanroads,TARURA nk kila mtu kwenye eneo lake anapanga kufikia hilo linatakiwa na chama tawala nk

MPANGA mipango ya Taifa usipokuwa na ilani utaishia kujitungia vitu ambavyo vikienda bungeni waziri wa fedha aki present vitapigwa chini na wabunge sababu haviko kwenye ilani ya chama chao!!! na utatutumbuliwa kwa kujijia na vyako vya kujitungia chumbani!!

lazima mipango yote i allign na ilani na sera za chama tawala
Usiku mwema kwa mara nyingine tena comrade
 
Mimi nadhani ni Sawa tu,

Maana yake halisi ni Sawa na Baba kujenga nyumba ya pili Halafu asiimbie familia yake kuwa amejenga nyumba nyingine mahali, Halafu akaweka wapangaji wasijue hata familia yake
Mfano hauhakisi kabisa na uhalisia....hao wananchi hyo barabara wangeiona tu,mbona zamani hakukuwa na haya mambo, shida ya hii awamu wanapenda sifa Yani that is the problem hio sababu ni za kitoto sana mi nikajua meneja kaiba hela za barabara haijakamilika
 
Wananchi wanaitwa na Mkurugenzi wa Halmashauri husika kupitia viongozi wa Kata na si wataalam. Huyu Meneja ameonewa mno. Jamani nafikiri kila mtu sasa ajitafutie biashara ujipatie Cheo hivyo vya kupewa ni masimango tu. Hata ukiwa na ajira hakikisha una mradi wako unaokupa cheo.
 
Yuko sahihi na alichoongea kizito sana
Uzinduzi wa barabara wananchi wengi wanatakiwa kuhudhuria mfano mialiko ilitakiwa iende kwa wadau wa barabara mfano umoja wa wenye mabasi,magari ya mizigo , daladala,boboda,waananchi ambao hizo barabara zinapita ambao walifaidi ajira ,kuuzia vyakula vibarua ,wajenzi nk ,makondractor ,wafanyabiashara wa maeneo hayo barabara inapita wakiwemo wa vituo vua mafuta vilivyoko hayo maeneo walio supply mafuta na watakaofaidi uwepo nk ambao wengine walifaidika kwa kuuza vifaa mbalimbali kwenye mradi

Pia viongozi wa maeneo barabara inapita mfano wajumbe wa nyumba kumi,madiwani,wabunge ,viongozi wa serikali za mitaa,viongozi wa dini nk

Viongozi wa vyama na serikali na mashirika ya umma kama TRA ambako hukusanya kodi , taasisi za kijamii

Uzinduzi maana yake ni kukabidhi mradi kwa wananchi kuwa kodi zenu jamani hizo hapo na kazi mlitupa kwa kodi zenu hiyo.Sasa waziri hawezi kabidhi barabara kwa meneja wa Tarura anakabidhi kwa wananchi

Hilo tukio ni la TARURA lakini alitakiwa kushiriksha wadau mbalimbali .Ahakikishe wadau wakabidhiwa wapo
Swali watu wakialikwa na wasipohudhuria uzinduzi haufanyiki?
 
Kazi ya meneja wa TANROADS sio kubeba watu na kuwaleta kwenye kufungua barabara. Sijasikia Jafo akizungumzia UBORA wa barabara hiyo bali amejikita kwenye wingi wa watu kushuhudia ufunguaji. Je UBORA wa barabara anamwachia nani? UVCCM?!
 
Jaffo aondolewe kwa kosa gani? kosa ni la huyo meneja kushindwa kualika watu, hata kwenye harusi watu wasipohudhuria makosa ni ya waandaaji, sio wenye harusi.
 
Wengi tumeona ile video ambapo waziri Jafo anamtumbua meneja wa TARURA Arusha kwasababu eti ameshindwa kuleta watu wengi kushuhudia ufunguzi wa barabara hiyo. Waziri Jafo anadai meneja wa TARURA anasaliti juhudi za JPM na kwamba kufungua barabara hiyo kimya kimya ni kuficha juhudi za JPM na hivyo akaamuru atumbuliwe.

Cha ajabu hakuzungumzia UBORA wa barabara ambalo ndilo jukumu haswa la meneja na sio wingi wa watu. Je, ni haki kwa meneja na mhandisi kukemewa kwa kutoleta umati wa watu katika ufunguzi huo? Ni haki kwa meneja kutumbuliwa tena hata baada ya kuomba msamaha kwa kosa ambalo si lake?
 

Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo amemuondoa kwenye nafasi yake Meneja wa TARURA Jijini Arusha, Podia Mwankenja kwa kushindwa kukusanya Wananchi kushuhudia barabara zilizokamilika alizokuwa akizitembelea.

Waziri Jafo amesema, “Mnataka Serikali ionekane haijafanya kitu wakati Wananchi ndio barabara yao? Kama ni barabara ya Wananchi mbona Wananchi hawapo hapa? Au unataka Serikali ionekane haijafanya kitu katika maeneo yao?”

Waziri Jafo amemuhoji Meneja huyo ambaye pia ndio Mratibu wa barabara za Jijini humo “Kwanini hii tunazindua barabara hii Wananchi hawapo? Unataka Rais aonekane hajafanya kitu? Rais ameweka fedha hapa. Mmeficha halafu kesho na kesho kutwa mseme Rais hajafanya kitu?”

Aidha, Meneja huyo alipoanza kujitetea na kusema kuwa alidhani Mtendaji (Mkurugenzi) amefanyia kazi suala hilo, Waziri Jafo alimwambia “Wewe si barabara zako? Unafanya sabotage ili Rais aonekane hajafanya kitu halafu kesho Wananchi waseme hakuna lolote Rais amefanya?”

Waziri Jafo amemalizia “Ninyi ndio wataalamu mnaofanga Serikali ionekane haijafanya jambo wakati sisi hapa Arusha tumewekeza fedha nyingi. Mji wa Arusha tumetandaza Barabara ila wewe unaficha hata Wananchi hapa jirani wasijue tumeweka barabara”



Jafo nampenda lakini hapo kakosea. Watu wa Arusha ni tofauti serikali kwao ni kazi yake kujenga hawawezi kukusanyika tu kuangalia barabara badala ya kufanya biashara zao ndogondogo, au kutafuta watalii mtaani, n.k ni mji wa wahangaikaji hakuna magenge kama ya Dar..
 
Jafo nampenda lakini hapo kakosea. Watu wa Arusha ni tofauti serikali kwao ni kazi yake kujenga hawawezi kukusanyika tu kuangalia barabara badala ya kufanya biashara zao ndogondogo, au kutafuta watalii mtaani, n.k ni mji wa wahangaikaji hakuna magenge kama ya Dar..


Magu au waziri mkuu anatakiwa amrudishe jamaa kazini.
 
Back
Top Bottom