Waziri Jafo apendekeza Stendi mpya ya Mbezi ipewe jina la Dkt. John Magufuli

Stendi za mabasi ni alama ya miji husika ndio maana hazipewi majina ya viongozi.

Napendekeza amuombe ule uwanja wa ndege ndio upewe jina lake.

Tangu tupate uhuru hakuna na wala sijaskia stendi ya basi kupewa majina ya viongozi.

Tunafahamu nia ya kila mteule kumfurahisha mkubwa,ikianza utaratibu huu, utashangaa hata Wakuu wa Mikoa na Wilaya wataiga kubadilisha majina ya stendi za mabasi zilizo katika maeneo yao!
Ombi kwako Waziri achana na pendeķezo hili, mkubwa alishasema msubiri akishastaafu ndio mpe upendeleo sio sasa.
 
😬😬😬
 
Pale Mpanda kuna mizengo pinda bus stand
Itakuwa "Isolated case", nitakupa mfano kuanzia Arusha mpaka Dar es Salaam

(i) Stand ya Mkoa Arusha
(ii) Stand ya Tengeru ( Wilaya ya Arumeru)
(iii) Stand ya Boma (Wilaya ya Hai)
(iv) Stand ya Moshi (Mkoa wa Kilimanjaro)
(v) Stand ya Njia Panda (Vunjo)
(vi) Stand ya Mwanga (wilaya)
(vii) Stand ya Same (wilaya)
(viii) Stand ya Mombo
(ix) Stand ya Korogwe
(xi) Njia panda ya Korogwe
(xii) Stand ya mkoa wa Dar es Salaam.

Kuanzia Arusha mpaka Dar es Salaam stand zote zinaakisi majina ya sehemu stand iliko
 
Lakin Mpanda kuna mizengo pinda stand
 
Assume kibao cha gari kinasomeka Dodoma to Magufuli
 
Swaziland ilibadilishwa jina ikaitwa Eswatini. Kwanini Tanzania isiwe Magufulini?
 
maaana kabla yake tulikuwa hata hatuvuti hewa lakini toka kuingia yeye madarakani tunavuta oxygen kwa wingi, mvua zimeongezeka na hata ardhi imekuwa na rutba zaidi.
😀😀😀😀😀 'Mimi ndimi bwana Mungu wako. Usiabudu miungu wengine.'
 
Ombi kwako Waziri achana na pendeķezo hili, mkubwa alishasema msubiri akishastaafu ndio mpe upendeleo sio sasa.
Akishastaafu itawezekana kweli? El bashir, Yahaya Jameh, Trump, B. Compaore etc walipostaafu sijasikia maeneo ktk nchi zao yalipewa majina yao.
 
Uwanja wa Ndege Chato ndiyo uitwe Magufuli International Airport - MIA
 
Mimi napendekeza waiite Samial Suluhu Hassan. JPM wanamlundikia vingi mno mwishowe atakakuwa anavikataa halafu matokeo yake watavipa majina hata yasiyostahili. JPM yuko na Majaliwa na Samia, why many things be in his name? Mimi ningefurahi sana safari hii kama stand hiyo wataiita Samia iwe kumbukumbu kwa vizazi vyote kwamba huyu mama aliwah kuwa Makamu wa kwanza wa Rais mwanamke, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 
Halafu Kuna pimbi mmoja anaotea eti jafo awe rais wa tz 2025. Ujinga wa hali ya juu sana
 
Kwani ikiitwa Mbezi Bus Terminal kama ilivyo kwa Ubungo Bus Terminal kuna nongwa gani?

Tupunguze kuendekeza mambo ya kijinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…