Waziri Jafo apendekeza Stendi mpya ya Mbezi ipewe jina la Dkt. John Magufuli

Waziri Jafo apendekeza Stendi mpya ya Mbezi ipewe jina la Dkt. John Magufuli

Tayari jina la mbezi latosha kwa maoni yangu lakini msini nukuu vibaya tafadhalini.
 
Kwani ikuitwa stendi kuu ya mabasi jiji la Dar es Salaam kuna mtu atatumbuliwa?
 
yaani nchi kila mradi unapewa jina la magufuli au nyerere. wangeita hata dar es salaam bus terminal ili kwani ni kama sura ya dar.
 
Yaani kuna watu wajinga sana ukita jina la mtu hii stand lazima kwenye mazungumzo utaje Dar. mfano stand ya mabasi ya magufuli ya dar es salaam. Huwez sema stand ya mabasi ya Magufuli mtu akakuelewa.

Daraja la Nyerere hapa Dar bila ya kutaja neno Kigamboni mtu hakuelewi na mpaka leo jina la Nyerere limebaki kwenye maandishi tu pale juu. Haya ndio madhara ya mihemko bila ya kifanya tafiti.
 
Habari za wakati huu JamiiForums.

Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo amesema na Stendi mpya ya Mbezi Luis kuwa na hadhi ya Kimataifa na kwa heshima ya Rais Magufuli anapendekeza iitwe Magufuli Bus Terminal

kama sehemu ya shukrani na kuthamini jitihada alizofanya JPM ambapo amesema atamuomba aridhie ombi hilo. "Japo Rais hapendi vitu kuitwa majina yake.


NANUKUU...Stand hii kwa heshima yake inatakiwa iitwe Magufuli Bus Terminal, ukija Dar es salaam unakutana na Julius Nyerere International Aiport.

hapa unakuta Magufuli Bus Terminal, lazima tuache alama kwa Watu wanaohangaikia Nchi hii, lazima tumuombe, akatae yote ila hii aridhie iitwe jina lake. Jafo
millardayo-___CKgCOXjg9Me___-.jpg


Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Spora Liana amesema kazi zinazoendelea kwa sasa kwenye Stand hiyo ni ufungaji wa viyoyozi, lifti, ufungaji wa taa na vifaa vya matangazo, uunganishwaji wa maji kwenye vyoo na miundombinu mingine ambayo nayo ipo hatua ya mwisho kukamilika na kusisitiza kuwa kwa sasa Stand inaweza kuanza kutumika.

Chanzo Millardayo
 
Kwaio mabus yatakua yanaandikwa morogoro to magufuli[emoji1787][emoji23][emoji23]
 
Kusifu na kuabudu.
Sio stand mpy atu! Mimi napendekeza hata jina la Dar es Salaam libadirisuwe na kuitwa "Pombe Magufuli city." CHADEMA kama mnawivu na Maendeleo aliyotuletea Magufuli, mjue hakuna Raisi aliyetuletea Maendeleo kama huyu tangu tupate Uhuru.
 
Kuna baadhi ya majina hayaendani kabisa na kitu husika.Majina yanabeba tabia husika.

Ipo haja ajae aje ayafute mfano jina linalosound daraja la tazara,sasa kuita mfugale ndo nn hata mgeni tu kutamka hawezi,si KILA kitu kilazimishwe majina husika bila kupima lipi linasound.

Stand ya mabus mbezi inasound zaidi kuliko msibabishe wengine wenye allergies na majina mabaya yaliyowaumiza yakatumika.
Mtu mwenye kidonda cha kubomolewa nyumba yake anajisikiaje.Kuna baadhi ya majina yasilazimishwe hayasound.

Zipo shule zilipewa majina ya watu zimereflect hivyo kushika mkia
 
Back
Top Bottom