Habari za wakati huu JamiiForums.
Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo amesema na Stendi mpya ya Mbezi Luis kuwa na hadhi ya Kimataifa na kwa heshima ya Rais Magufuli anapendekeza iitwe Magufuli Bus Terminal
kama sehemu ya shukrani na kuthamini jitihada alizofanya JPM ambapo amesema atamuomba aridhie ombi hilo. "Japo Rais hapendi vitu kuitwa majina yake.
NANUKUU...Stand hii kwa heshima yake inatakiwa iitwe Magufuli Bus Terminal, ukija Dar es salaam unakutana na Julius Nyerere International Aiport.
hapa unakuta Magufuli Bus Terminal, lazima tuache alama kwa Watu wanaohangaikia Nchi hii, lazima tumuombe, akatae yote ila hii aridhie iitwe jina lake. Jafo
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Spora Liana amesema kazi zinazoendelea kwa sasa kwenye Stand hiyo ni ufungaji wa viyoyozi, lifti, ufungaji wa taa na vifaa vya matangazo, uunganishwaji wa maji kwenye vyoo na miundombinu mingine ambayo nayo ipo hatua ya mwisho kukamilika na kusisitiza kuwa kwa sasa Stand inaweza kuanza kutumika.
Chanzo Millardayo