Waziri Jafo asema atabandika majina hata ya wale waliojitoa na kura zitapigwa

Hawa ni wagombea binafsi sio?
 
Anatakiwa atangaze mgombea aliyechukua fomu ndie atangaze kujitoa sio Chama.Chama hakikuomba popote kugombea.Hivyo hakina mandate ya kusema kinajitoa kwani chenyewe ndicho kilijaza fomu kuomba kugombea?
Anagombea kwa kupitia chama fulani. Ndo maana hata kuna zile fomu zilizokosewa majina ya chama according to wahusika zilikua disregarded. Huyo mgombea akiambiwa leo sio mwanachama means hawezi kuendelea kuwa mgombea wa kile chama kwenye chaguzi.so yes chama kikijitoa automatic mgombea lazma atoke. Ridhaa ya chama.....!!!!
 
Umekosa akili. Kuna mtu anaruhusiwa kugombea bila kupitia kwenye chama? Na hao walioenguliwa si tumeambiwa ni kwa sababu wamejaza CHADEMA na ACT? Kama vyama havina nafasi si wangewapitisha tu kama wagomvea huru? Kwa nini wanasema wamewaondoa kwa kukosea kujaza majina ya vyama vyao?
 

Mdhamini wa mgombea ni chama mdhamini akijitoa mgombea hana guvu yoyote lakini uchaguzi huu hauna mgombea binafsi
 
Anatakiwa atangaze mgombea aliyechukua fomu ndie atangaze kujitoa sio Chama.Chama hakikuomba popote kugombea.Hivyo hakina mandate ya kusema kinajitoa kwani chenyewe ndicho kilijaza fomu kuomba kugombea?
Unaelewa maana ya tamko la chama kushiriki uchaguzi au kutoshiriki? Kabla ya processes za wagombea, chama kinachoshiriki uchaguzi ni lazima kitamke. Kama chama kina uwezo wa kutamka kuwa kitashiriki, kwa nini kisiwe na uwezo wa kutamka kuwa kimejitoa au hakitashiriki?
 

Hivi kweli kweli waliochukua fomu kupitia vyama pinzani ni vilaza kuliko wanaccm wote waliochukua fomu?
Nauliza tu kwa sababu sijasikia mwana ccm aliyeenguliwa haet kwa kujaza fomu vibaya.

Inamaana kama kuna semina na maelekezo yaliyotolewa, basi yalitolewa kwa wanaccm tu na vyama pinzani watu wao awakupewa hayo maelekezo?

Nigeshauri Fomu zote ziwekwe wazi ili watu wajiridhishe kuwa wamekosea au wameonewa.
 
Swala la kujitoa ni mgombea,lakini wakati wa kuchukua form chama ni mdhamini?
 
Anatakiwa atangaze mgombea aliyechukua fomu ndie atangaze kujitoa sio Chama.Chama hakikuomba popote kugombea.Hivyo hakina mandate ya kusema kinajitoa kwani chenyewe ndicho kilijaza fomu kuomba kugombea?

Tz hatujawa na wagombea binafsi tujifunze siasa
 
HIV unaelewa maana ya kudhaminiwa?au unakata viuno tu hapo?
 
Sio lazima Kutamka vyama kibao havikutoa matamko ya kushiriki lakini fomu vilichukua Sheria ya uchaguzi haitamki.popote kusema lazima Chama kitamke kwanza kuwa kitashiriki au la ili wagombea wake wapewe fomu
 
HIV unaelewa maana ya kudhaminiwa?au unakata viuno tu hapo?
Kudhamini ni issue binafsi Kama Chama kinajitoa udhamini kilitakiwa kiwaambie wagombea wake na wao ndio waseme tunajitoa sababu mdhamini wetu kajitoa tunaomba msimamizi Kama una fomu ya mdhamini kujitoa nipe nimpelekee akajaze alete kwa maandishi.

Fomu za kudhamini wagombea vyama vilijaza kujitoa pia vijaze fomu vipeleke kutengua fomu zao za mwanzo.othetwise huko.kujitoa kwenye press ni matangazo tu ya vijiweni ambayo sio official.Jafo Yuko sahihi wote waliopitishwa watapigiwa kura
 
Sawa yupo sahihi haya tangazen ushind wa kimbunga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…